Tahadhari na 'showstopper'!!!

chiko

JF-Expert Member
Feb 24, 2010
580
245
Showstopper... ni wale warembo ambao, wakipita barabarani waaacha waume domo zege, waume lazima wapinde shingo. Mwenyezi mungu kawaumba kwa MAKINI zaidi, nao wanajua, huongezea madaha. Warembo dizaini hii ni hatari sana sana!!!.

Napenda kutoa kisa kilinipata na pia ni ushauri kwa kina kaka, kwani damu ikiwa yachemka mtu akili hutupa jaani.

Ilikuwa wakati kama huu wa December, miaka kadhaa iliopita, kazini kwetu aliandikwa msichana mmoja 'Showstopper', kama mpokezi wa wageni na secretari. Wakati huo mimi sijao na damu yanichemka. Katokea mzee mmoja twafanya nae kazi, katika maongezi ya kazini, akatuasi..."Vijana wangu, mimi ni meishi sana na nimeona mengi, Wasichana kama huyu 'Showstopper', mchunge sana, watu hawa ni balaa!!.

Mimi nikiwa kwenye mashindano na wenzangu, nikajua hawanipati, ushauri nikatupa mbali, nikaanza kunyemelea, muda haukupita, 'showstopper' akawa wangu, tukirusha roho na kufunga mwaka. Haikuchukua muda, mimi pia nilikua si kidogo, nikaona mbio zake si wezi, nikamwachilia.

Kumbe Bosi wetu nae alikua ananyemelea, akaingia kwenye mtego!, Bosi alipelekwa mbio, kiasi hata kutumia hela za kampuni kumstarehesha kimwana. Mwisho Bosi na 'Showstopper' walipatikana na scandal ilio wafuta kazi.

Hii hadithi yoote, ni kwa masharobaro, wasichana hawa 'Showstopper' ni moto wakuotea mbali...chungeni sana , waweza kukupa kifo cha haraka, akufanye uibe ama kuachishwa kazi!!!

MWAKA MPYA MWEMA!!!!!
 
sasa kama mie mzuri sana, nijibonde bonde?
Tamaa zenu na tabia mbaya za baadhi ya watu isiwe sababu ya kuvictimise wanawake wote wazuri

hebu ngoja nikapake mascara mie.
 
sasa kama mie mzuri sana, nijibonde bonde?
Tamaa zenu na tabia mbaya za baadhi ya watu isiwe sababu ya kuvictimise wanawake wote wazuri

hebu ngoja nikapake mascara mie.

Kongosho umenifurahisha sana.KWELI KABISA SIO WOTE LAKINI.Mtoa thread umelenga kuwacomfort wasichana wasio wazuri ki sura(tena haswa wanaowaogopa wasichana wakali)UMEFANIKIWA KUBOOST MARKET YA WASICHANA WALIO SIO WAKALI.
 
Wamekusikia hao masharobaro..#Sio vyote ving'aavyo ni dhahabu...!
 
Laiti kama ungenisikiliza yasingalikukuta yaliyo kukuta,
pole sana kijana,
hata huyo pia nilimweleza ula hakusikia.
 
sasa kama mie mzuri sana, nijibonde bonde?
Tamaa zenu na tabia mbaya za baadhi ya watu isiwe sababu ya kuvictimise wanawake wote wazuri

hebu ngoja nikapake mascara mie.

Hahahhhhhhh kongosho umenifurahisha sana! Hizi thread za hivi bana! Zinanifanya nijiulize hivi hakunaga namna ambayo mwanaume anawezamdhibiti mwanamke asimwache? Yaani amchengue kiasi cha kumfanya wengine woote awaone kaka zake?
 
sasa kama mie mzuri sana, nijibonde bonde?
Tamaa zenu na tabia mbaya za baadhi ya watu isiwe sababu ya kuvictimise wanawake wote wazuri

hebu ngoja nikapake mascara mie.
Hahahaaa hii imetulia nimeipenda lol. . .
 
sasa kama mie mzuri sana, nijibonde bonde?
Tamaa zenu na tabia mbaya za baadhi ya watu isiwe sababu ya kuvictimise wanawake wote wazuri

hebu ngoja nikapake mascara mie.

Siku sema hawafai, ni tahadhari kabla ya hatari!!!!, kwani weye Kongosho ni 'showstopper'????
 
Back
Top Bottom