Tahadhari: Mafuriko makubwa kutokea Tanzania

Inaonyesha kama mvua ya kimbunga lakini sidhani kama itakuwa kubwa kama ya majuzi..
 
Kama hiyo tahadhari imetolewa na mamlaka ya hali ya hewa ya nchi hii, hata haina haja ya kuhofia kwani wanaweza wakasema mvua itanyesha badala yake bonge la jua linatandika.
Nimezoea kuwasikia wakitabiri post-tukio, wameanza lini kutabiri pro-tukio?. Anyway tuchukue tahadhari
 
hata wiki iliyopita walisema kuwa mvua itanyesha had jumamosi ya tarehe 24 but likaja jua la maana. Hao hali ya hewa nahsi hawana uhakika na kaz yao.
 
Kha,dar pwani dodoma,ina maana mvua ikifika Moro itaganda then itaenda Dodomaaaa
Kuna taarifa imetolewa na Mamlaka ya Hali ya Hewa kuwa watu wawe na tahadhari kwani kuna uwezekano wa kunyesha mvua kubwa sana kama ilivyotokea hv majuzi.

Mvua hizo zitaathiri mikoa ya Dar es Salaam, Pwani, Mtwara, Lindi, Unguja, Mbeya, Iringa, Dodoma, Singida, Rukwa, Tabora na Kigoma.

Kwa wale wanaoishi Dar watakubaliana na hili hasa ukiangalia upande wa Magharibi kuna wingu kubwa limetanda.

Source: Clouds FM
 
Kuna taarifa ambayo TBC1 wameitoa kama habari mpasuko usiku huu nafikiri. inahusu mvua maana nimekuta inaishilia. Maneno ya mwisho niliyoyasikia ni kuwa watu wa mabondeni wachukue tahadhari. Kuna yeyote aliyeisikia taarifa kamili atujuze?

Jenga tabia ya kusoma walioandika wenzio kabla hujatoa hoja yako..._
 
Wamechemka huku DSM jua kali ndo kwanza saa moja jua kali kama la saa sita,wajipange hao TMA washachemka hakuna cha mvua wala nini.
 
Kama hiyo tahadhari imetolewa na mamlaka ya hali ya hewa ya nchi hii, hata haina haja ya kuhofia kwani wanaweza wakasema mvua itanyesha badala yake bonge la jua linatandika.

lakini si unaweza kulinganisha na taarifa za mamlaka nyingine au kupitia vyazo mbalimbali vya habari kuona kama utabiri ni sahihi au la !!! Mimi nadhani tuchukulie kila taarifa kwa uzito wake, tusiwahi kuzipunguza uzito.
 
Hata hivyo utabiri huu hauhusishi maeneo ya Magogoni!!!!! Kule mvua haifiki ila maji yaweza kupita tu!!!
 
Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania, imetoa taarifa kua kuanzia kesho mpaka Mwaka mpya kunatarajia kuanza kunyesha mvua kubwa kuliko maelezo! Mikoa itakayokubwa na kadhia hyo ni Dar km kawa, Kgm, Singda, Ddma, Iringa, Mtwara, Pwani, Tanga, Mbeya, Morgr. Wakazi wa mabondeni hasa wale wabishi wanatakiwa kuyaaga makazi yao mara moja kabla ya kukutwa na hiyo noma!
Nawasilisha. (Source; TBC1)

Kitengo hiki cha utabiri wa hali ya hewa kipo hoi' sijaelewa kama wanasema kweli au wanawatishia wananchi maana wamekuwa hawasemi kweli tena' wanababaisha tu!
 
Update ya mara kwa mara juu ya hali ya hewa ni muhimu kutoka Mamlaka ya hali ya hewa Sijui wanakwama wapi wakati wana mitambo ya kisasa?Kama ni kweli basi Dar itazama kwani ardhi imelowana na maji kutokana na mvua zilizokuwa zikinyesha,na kama tide ya bahari itakuwa kubwa wakati ikinyesha basi ni hatari tupu maeneo ya pwani tambalale kama Jangwani na kwinginepo,kibaya zaidi miundo mbinu imeishajeruhiwa kinachosubiriwa ni little push tufunge kazi.
 
mtwara jua ni kali sana xmass, boxing day hadi leo hii hali ni shwari kabisa...ingawa kuna kawingu cha kizushi
 
Utukuzwe Mungu wetu, Bwana wa Mabwana na Mfalme wa Wafalme. Utukufu, Ukuu, na Mamlaka vina wewe Mungu Wetu. Hakika tunaungana na wale Wazee 24 na wengine Wanne wenye Uhai mbele ya Kiti Chako cha Enzi tukisema: WASTAHILI BWANA.

Majira, Nyakati, na Enzi vyote ni mali yako. Ni nani alijuaye kusudi lako Mungu Wetu, au ni nani awezaye kayasoma Mawazo ya Moyo Wako Bwana? Tujalie basi kuzihesabu siku zetu; na hata kuyatambua majira ili tusije tukaangamia kwa upumbavu wetu.
 
Lakini hawa TMA wakitabiri leo mpaka baada ya miezi 3...walitabiri September ikatokea December....sasa wametabiri December....tuangalie March mwanzoni hivi...au isiwepo kabisa...huu ndio ubaya wao...na ndio maana wale watu wanakaidi kuondoka....kama wangekuwa wakisema kweli inatokea nani angekaa mabondeni.....
 
Waungwana,
kuna wingu zito sana limeanza kutanda Dsm,watu wameanza kuingia hofu kufuatia tahadhari iliyotolewa jana...zidisheni sala maafa yasijiludie.
Wale wa mabondeni tuanze kuwastua ndugu zetu wakimbie,maana wengi tuliludi kufukua vitu vyetu..

Msiseme sikusema.
 
Back
Top Bottom