Tahadhari kwa wanaume wanaosafiri nje ya nchi...

Mtoboasiri

JF-Expert Member
Aug 6, 2009
5,101
1,946
Wana JF,

Hii ni maalum kwa wanaume wanaosafiri nje ya nchi yetu ama kikazi au kimasomo hasa safari za muda mfupi (mwezi na chini ya hapo). Kuna tukio limetokea usiku wa kuamkia leo. Samahani sitataja jina la muhusika wala mji yalikomkuta, ila nimehakikishiwa na chanzo cha kuaminika kilicho kwenye sehemu ya tukio. Kisa kiko namna hii:

Kuna Mtanzania mwenzetu (ni mtu wa makamo na kiongozi kwenye moja ya taasisi zetu za fedha) alikuwa na safari kwa short course ya wiki moja. Jana (siku moja kabla ya shule kwisha) akaenda na mwenyeji wa hiyo nchi na mji usiku kwenye masanga, huko akapata timu pinzani ya mechi ya mchangani na akamleta hotelini alipofikia. Binti akang'ang'ana kuwa hawezi kwenda peke yake, ni lazima aende na mwenzie. Mzee akamshirikisha na mwenzie (Mbongo pia) ili akubali kuondoka na ule mzigo mwingine. Jamaa namba mbili akakubali, wakawachukua hao "Chips funga" kama Watani zetu wa jadi (Wakenya) wanavyowaita.

Asubuhi ya leo walinzi wa hoteli (ona tofauti ya hoteli zetu na wenzetu) wakawasimamisha wale wadada getini kwa upekuzi na wakawakuta na laptops za jamaa. Wakawashitukia, (hoteli hiyo ina utaratibu kuwa mgeni akija na laptop inasajiliwa, ukitoka unaonyesha risiti ya laptop uliyopewa wakati wa kuingia). Kuangalia details, ni laptops za Wabongo. Walinzi wakawashikilia wadada ili kuhakikisha usalama wa wateja wao. Piga simu za vyumbani weee! Hakuna majibu, wakaita polisi (wadada wakiwa bado wamezuwiwa wasiondoke), kufungua milango kwa master key, HAMAD! Jamaa wako uchi wa mnyama hoooi wanakoroma, kuwaamsha hawaamki. Kuwapekua wadada wana dola 3,500 na Shilingi kadhaa za kibongo (mbali na laptops).

FUNDISHO

Wanaume kwani ni lazima tutafute totoz ughaibuni hata ukimwacha mamsap kwa wiki moja tu?

NA NYIE WADADA,

Kwani ni lazima ukombe kila kitu? Si angalau tunza utu wa huyo unaemkomba ukichukulia ulipata "service" hata kama haikuwa ya kuridhisha?
 
...mtoboasiri acha hizo bana, unamwaga punje kwa kuku wengi.
mgeni kukarimiwa ni kawaida, hata wao wakija Bongo wanapewa
'escorts'

Anyway, thanks kwa tahadhari.
 
Duh!
Mijanaume mingine haiwezi kuvumilia hata siku moja. Kama vile wana kale kapepo.
 
Du asante kuliweka wazi hilo ni kweli hasa mademu wa hapo bondeni usiguse mi iliwatoke jamaa wanne tukiwa nao na mmoja tu ndo vitu vyake vilipona, please watanzania tuwe makini na tujiepushe make wale vikuku walikuwa wanasema ''Tanzanian are very kind'' pengine walimanisha warahisi kukamata who knows? Cha ajabu hata mwenyeji wetu ambae ni mtanzania lkn anaishi huko siku nyingi nae chaaliii
 
Wandugu hilo haliko Ughaibuni pekee, mbona hata hapa Bongo yanafanyika sana? Ni mtindo kwa akina dada wenye njaa kali!
 
Back
Top Bottom