Tahadhari kwa Serikali kuhusu mradi wa Mikaratusi wa Mtwara

Tikerra

JF-Expert Member
Sep 3, 2008
1,702
146
Serikali imerithia upandwaji wa ekari 50,000 za mikaratusi kwa ajili ya kusafirisha magogo kwenda Japan.Sina hakika kama maslahi ya Taifa yalizingatiwa na wahusika kwa vile mradi huu ni hatari kwa mazingira ya nchi yetu.Hakuna mtaalam wa udongo asiyejua athari ya mikaratusi katika mazingira,na kuukubali mradi huu ni jambo lisilo kubalika kabisa.

Nomba nitoe matokeo ya utafiti wa hivi karibuni kabisa,2003,ambao umefanywa kule Uruguay kwa kipindi cha miaka 20 mfululizo.Kikundi hiki kiliongozwa na mtaalam Carrasco,L. Matokeo ya utafiti huu(kwa kingereza) yalikuwa kama ifuatavyo:

"The results show a statistical significant soil acidification,diminution of soil organic carbon,increase of alipaticity degree of humic substances,and increase of affinity and capacity of hydrolytic activity from soil microbial communities for forested sites with Eucalyptus sp.but also,tendency of podzolization and/or mineralization by this kind of cover changes,with a net soil organic matter loss of 16.6 ha per hectare in the Au horizon of soil under Eucalyptus sp.compared to non Ecalyptus planted land."

Matokeo haya ni mabaya na yanahakikisha matokeo ya miaka mingi kwamba kweli mikaratusi inakausha maji na inafanya udongo husika usifae tena kwa kilimo kwa ujumla na hata kusababisha mmomonyoko wa ardhi kwa vile udongo hauna tena uwezo wa kuhifathi maji.

Katika mazingiza haya, sijui Serikali ilitumia vigezo gani kupitisha mradi huu hatarishi kwa mazingira yetu.Nashawishika kusema kwamba kitu kidogo kilitolewa na Serikali ya Japan ili kuukubali mradi huu.

Namuomba Rais Kikwete auangalia tena mradi huu kwa vile hauna maslahi kabisa kwa taifa letu.Nomba tujiulize,kwa nini wao wasipande kwao, kama miti hii ni mizuri?
 
Mkuu, hii ni moja ya project ambayo tuliwahi izungumzia kuwa haifai japo serikari inawakumbatia wawekezaji wa mradi huu. Achana na utafiti wa Uruguay, NEMC walisha toa tamko kupingana na mradi huu sasa sijui nao hawana meno or? maana mambo yanaendelea, Miradi kama hii ipo mingi sasa bongo na waweezaji wengi wamechukua mashamba makubwa maeneo ya morogoro, msanga, Kisarawe, ''pembezoni mwa Dar''. Serikali pia ilifanya uhamasishaji kwa wananchi kuukubali mradi huu kama money making project. Nadhani kama speed tuliyonayo kwenye dili nyingine za kifisadi, tuiwekeze kwenye miradi hii inayo lenga kuleta baa la njaa endelevu Tanzania
 
Thanks Tikerra;

Pia tuna live example kule kondoa ambapo kuna baadhi ya maeneo ilipandwa mikaratusi na ardhi imeharibika kabisa na vyanzo vingi vidogo vidogo vya ardhi kukauka... i think HADO na UDSM wana technical report ya hali ile

All in all... its not late we can stop this now thorugh public education and strategic campaigns
 
Last edited:
Back
Top Bottom