Tahadhari: Kuna maji ya Kilimanjaro feki!

white wizard

JF-Expert Member
May 18, 2011
8,314
13,278
maji ya kunywa ya nayotengenezwa na bonite bottlers ltd,aina ya kilimanjaro nayo yameisha anzwa kuchakachuliwa!kwani ni maji pekee yaliyokuwa yakiaminika kuwa ni salama,ila cha ajabu kwa sasa yapo fake kibao hususani sumbawanga,na mpanda!leo nilikuwa sumbawanga nikaagiza maji kilichonishitua ni kuona mbona haya shingo yake ni fupi!na mfuniko umepauka,na hata neno kilimanjaro juu ya mfuniko ni kama wameriandika kwa ki2 chenye ncha kali!na hata ndani maji ukiangalia c meupe kama yale tuliyoyazoea!ndio nikamuuliza muhudumu kulikoni naye anashangaa kuwa mbona kuna wa2 kama wa 3,nao wameshayarudisha,kuwa ni fake!nikaenda mpanda nako hali ni ile ile,ila yale original yanakuwa na shingo ndefu na mifuniko yake imekolea sana,na cha ajabu hata kwenye maduka ya jumla yanauzwa bei tofauti,ila kwa rejareja bei ni moja tu 1500".hivyo kuweni waangalifu mnaponunua maji ya kilimanjaro nayo yapo yaliyochakachuliwa!wahusika fuatilieni kwani kwa sasa wa2 wameshaanza kuyaogopa ukizingatia ndio maji yanayouzwa bei ya juu kulinganisha na mengine
 
Tumekwisha! Na maji ya Kilimanjaro nayo! Tutakunywa maji gani sasa? Lisebene la ARV feki bado liko uwanjani limepamba moto, SIRIKALI inasema zirudishwe waliko zitoa' je hayo maji feki yatarudishwa wapi? Hivi kweli hii SIRIKALI yetu imeshinda kusimamia, mpaka tunaletewa hadi MAJI bandia. Kindumbwedumbwe cha dawa za ARV feki zinazosambazwa wao wenyewe hadi kwa watumia, zikipitishwa kwenye taasisi hizihizi zinazo simamiwa nawao wenyewe SIRIKALI - wanashindwa kuzibiti, baada yakuwa tumeanza kutumia wanatutangazia kuwa ni ARV feki, TUFANYEJE SASA! tena tunagaziwa hizo dawa feki zirudishwe kwa DR. aliyekupatia, madudu juu ya madudu kila kukicha. Je nahaya Maji feki tuyarudishe kwa nani? Mimi ninahisi ni miradi ya WENYEWE, WA WALIO SHIKILIA MPINI. Wadau naomba tutafute dawa ya haya matatizo, tumechezewa vyakutosha miaka nenda rudi. MIMI KUANZIA LEO NITAKUWA NINAKUNYWA MAJI YA MADAFU TU, au wadau mnasemaje?
 
Asante kwa taarifa mkuu. Maji ya Kilimanjaro yamekuwa tishio kwa watengenezaji wengine na sasa wanatumia mbinu kuyaharibu. Pia viko viwanda mitaani vinatengeneza maji hasa ya makampuni mengine. Bonite Bottlers umefika wakati pandikizeni watu ili mjue mchawi wenu. Najua Mangi kazi hii ni ndogo kwako sana na ukweli utaupata. Kilimanjaro is the best drinking water so far ukiacha yale ya Iringa kipingi kile sijui yaliishia wapi.
 
Hata huku moshi yanakotengenezewa yako yamejaa tele,mi nilidhani labda wamebadilisha chupa na mifuniko, hebu tufanye uchunguzi zaidi
 
Wabongo noma kwa kuharibu.kila kitu tunachakachua! Hii ni hali ya hatari sana wajomba.
 
Hata huku moshi yanakotengenezewa yako yamejaa tele,mi nilidhani labda wamebadilisha chupa na mifuniko, hebu tufanye uchunguzi zaidi

BONITE bottlers KAMA WAMEBADILI brand au packages ya MAJI YA KILIMANJARO Walitakiwa kuwatangazia wananchi ambao ndiyo sisi wateja wao, ILI KUEPUKA USUMBUFU NA WASIWASI KWA WATUMIAJI. Naomba wadau walio karibu na utawala Bonite B. tufatilie ili kujua kama wamebadili packages,
 
Mleta Uzi ungekua muungwana sana endapo ungetuletea picha ya hiyo chupa hapa ukumbini!
 
Mh! Kweli hata mi shahidi pande za iringa mbeya hd 2ndma yapo tena ukiuliza mhudumu anakwambia nayo ni product yao wamebadili chupa na lebo tu.
 
hata arusha ndo hayo tunakunywa mkuu...nafikiri wamebadilisha brand....though walitakiwa watujulishe...
 
Hakuna pa kukimbilia kwakweli! tbs mpo?
Hivi tbs wana matawi wilayani? Yaani unauliza tbs wilayani wakati mkoani tu kwenyewe hakuna. Kwanza tbs kazi yao ni kugonga mihuri tu kwenye bidhaa. Sidhani kama kila bidhaa inapotegenezwa wanakuwepo na kufanya ukaguzi.
 
Kuzaliwa kwa chama kipya tarehe tano mwezi wa pili sabini na saba, ehe mungu kipe.......Hatua zisipochukuliwa nani atabaki ili apige kura 2015. Kura za waathirika wa VVU nazo hazitakiwi? Mbona mnawapa dawa feki au wafuasi wa Dr Mbulu? Je watu wameamua kumpunguzia kura zake?
 
Haya maji jamani vipi? Profesa Mbwete wa Chuo kikuu Huria Tz naye alishawahi kuelezea dosari za maji ya kunywa yanayouzwa hapa nchini katika chupa watu wakambishia, haya sasa mwingine huyo....!
 
Back
Top Bottom