TAHADHARI - Dawa bandia za malaria Afrika

Absolute

JF-Expert Member
Jan 19, 2007
333
61
Dawa bandia za malaria zaongeza madhara

111019004447_malaria_patient_304x171_afp_nocredit.jpg
mgonjwa wa malaria

Wanasayansi katika Chuo Kikuu cha Oxford nchini Uingereza wamesema kuwa ongezeko la dawa bandia barani Afrika, ni pigo kubwa katika juhudi zinazoendelea za kupambana na maradhi ya Malaria.
Malaria huwaua karibu watu milioni moja kila mwaka katika bara la Afrika.

Wanasayansi wa chuo hicho wamesema kuwa kuuzwa kwa dawa hizo bandia huwadhuru wagonjwa mbali mbali na kusababisha wagonjwa hao kutoweza kupata tiba kamilifu wanapotumia dawa sahihi.
''dawa bandia zatoka Uchina''

Wataalamu hao wa dawa walisema baadhi ya dawa hizo bandia zinatoka Uchina.
Wameshauri kuwa wataalamu wa maswala ya afya katika bara la Afrika wanapaswa kuchukua hatua kambambe za kusitisha kuenea kwa dawa hizo bandia katika bara la Afrika au sio mamilioni ya watu watafariki.
Watu walio taabani sana kutokana na dawa hizo bandia ni watoto na wanawake waja wazito.

SOURCE: BBC Swahili - Habari - Dawa bandia za malaria zaongeza madhara
 
Haya ndio madhara ya soko huria, serikali ya Tanzania, ichukue hatua kwani dawa hizo zipo sokoni, na madaktari wengi wanashawishi wagonjwa kuzitumia kwenye maduka yao binafsi yaliyo karibu na vituo vya Afya.
 
Waambie TFDA na Wizara ya afya waache kuruhusu makampuni yasiokuwa na hadhi kudump madawa yasiokuwa na standard. Wao huruhusu kampuni yeyote ilimradi % wapate.
 
Dawa bandia za malaria zaongeza madhara

111019004447_malaria_patient_304x171_afp_nocredit.jpg
mgonjwa wa malaria

Wanasayansi katika Chuo Kikuu cha Oxford nchini Uingereza wamesema kuwa ongezeko la dawa bandia barani Afrika, ni pigo kubwa katika juhudi zinazoendelea za kupambana na maradhi ya Malaria.
Malaria huwaua karibu watu milioni moja kila mwaka katika bara la Afrika.

Wanasayansi wa chuo hicho wamesema kuwa kuuzwa kwa dawa hizo bandia huwadhuru wagonjwa mbali mbali na kusababisha wagonjwa hao kutoweza kupata tiba kamilifu wanapotumia dawa sahihi.
''dawa bandia zatoka Uchina''

Wataalamu hao wa dawa walisema baadhi ya dawa hizo bandia zinatoka Uchina.
Wameshauri kuwa wataalamu wa maswala ya afya katika bara la Afrika wanapaswa kuchukua hatua kambambe za kusitisha kuenea kwa dawa hizo bandia katika bara la Afrika au sio mamilioni ya watu watafariki.
Watu walio taabani sana kutokana na dawa hizo bandia ni watoto na wanawake waja wazito.

SOURCE: BBC Swahili - Habari - Dawa bandia za malaria zaongeza madhara

ndio maana mimi kesi ya malaria huwa naimaliza kwa Aloevera chugu... Hii midawa hii?
 
Back
Top Bottom