Tahadhari: CCM, Msikilizeni Sumaye

Aanze kujihukumu yeye na serikali yao alipokua madarakani kwa kuacha nyufa na kudharau kuiziba sasa ukuta ndo ushamwangukia ananyooshea watu kidole

Mtanganyika naunga mkono maneno yako. Alikuwa wapi kabla au kwa sababu amekosa nafasi? Sitetei SISIEMU bali nawasaidia watanzania wengi kama si wote waliosahau kuhusu uongozi mbaya uliopita na ambao upo sasa haya yote ni matokeo ya kina Sumaye na wenziye waliopita kama wangeona na kuondoa mapema tusingefika hapa tulipo. Kila jambo lina mwisho wake, sababu mwanadamu anayeweza kugundua na kuweka mambo ili maisha yaende ANAKUFA je kilichogunduliwa na kuwekwa kwa nini kisife. FUNGUKA MTANZANIA UNAWEZA KUJIKOMBOA UKIAMUA BILA KUPTEZA AMANI. Ila tusikubali kudanganywa tena na WAROHO WA MADARAKA.
 
KWA NINI CCM KITAFUNWE KWA KASI KUBWA AJABU NA MBINU ZAKE ZENYEWE ZA UCHAKACHUAJI ULIOTUKUKA KATIKA CHAGUZI ZAKE NDANI AU NDIO KUSEMA UNABII JUU YA HATIMA YA CHAMA HIKI NDIO SASA KUTIMIA??

Mkuu asante kwa kupenda kuona CCM kisichochakachua manbo kila wakati.

Nasema asante kwa kutamani kuona DEMOKRASIA katika uhalisia wake isiobughudhiwa hata kidogo na saratani za UDINI, UANAMTANDAO, UKANDA NA UKABILA.

Nashukuru pia ulivyoonyesha mpenzi makubwa kwa kutoa maoni yako yaliojawa uchungu mkali toka kwenye sakafu la moyo wako na kuwataka viongozi wako wwe ni wenye KUWAFUATA WANANCHI WALIPO NA KUSHUGULIKIA MALALAMIKO YAO HUKO HUKO bila kuendeleza umangimeza na kiburi cha kukaa kitako kwenye viyoyozi maofisini KUTEGEMEA KUFIKISHIWA KILA KITU HUKO HUKO.

E baba weeee, kidogo hadi hapo naona kama vile uko kwenye usingizi mzito ukidhania ya kwamba hiki CCM-Ukoloni Mamboleo ambacho hivi sasa kiko rasmi katika udhibiti wa lile kundi hatari la MAFISADI eti unakichukulia kuwa sawa na ile CCM ya Mwalimu Nyerere ya miaka ile; pole sana hadi hapo.

HULKA na tabia mbaya ya ukabila, ukand, udini pamoja n uanamtandao kuwa ni misingi rasmi ya watu KUCHAKACHUANA hakika ndio sanda na jeneza la chama hiki pachaka kutoboka jumla hivi karibuni kote nchini.

Nasema kama CCM ni kile kile kilichojaa kiburi cha kobe, UFISADI wa jogoo kujihisi kila tetea ni halali yake, nasema kama CCM ni kile kile chenye 'U-MIMI' kwa na mslahi ya umma wa Tanzania badaye, kamwe hakutosikilizwa mtu hapa; si Mhe Sumaye wala melf ya wanachama wengine kibao ambao nao wamefikwa na madhila kama haya haya.

Mkuu, hadi hivi sasa ni kwamba ombi lako limefikia patupu patupu na kamwe hiki CCM tunachokifahamu vema sana tu wala hakiwezi kubadilika hata kwa dawa kwa kuwa fitina na majungu ndio sala zao za kila siku iwe ni asubuhi, mchana au usiku.

Mwisho, nimalizie kwa kusem ya kwamba unabii wa kale juu ya chama hiki kikongwe sasa waja kwa kasi ajabu leo hii kuliko hata hapo jana.

Ajabu zaidi leo hii ni kwamba hata zile salam za wanacha wakulima na wafanyakazi wa miaka hiyo kwa kusema
'KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI' leo hii imebadilika kabisa huku matajiri wachache wakiwa ndio wamekihodhi chama humu wakijibunia salam yao mpya ya 'KIMUDU CHAMA CHA MAPINDUZI' ambapo mtokeo yake ndio kama hivyo dhuluma kwa kwenda mbele kwa kila kitu wanchoweza kukitia mikononi na kukimudu vilivyo kwa faida ya wachche.

Kama watu mlikua hamjui bado tu; CCM ya leo 'KINA WENYEWE' na wenyewe hao si MKULIMA wala MFANYAKAZI tena hivyo unapolia kilio cha mtu mzima hivi mbele ya kandamnasi wengine huku tujajiuliza eti 'kwani bado alikua hajui tu CCM ya leo hati miliki yake kuwa chini ya makucha ya MAFISADI ORIGINAL without apology???????'

Maoni yaliyotolewa na Mh F Sumaye, pamoja na kushindwa kupata U-NEC, ni wake up call kwa CCM.
Sina uhakika kama Mh Sumaye angetoa maoni hayo kama angeshinda kinyang'anyiro hicho cha kugombea U-NEC.

Hata hivyo kwa wanacha waaminifu wa CCM aliyosema Mh Sumaye ni common knowledge, ufisadi utaiangamiza CCM kama chama cha siasa makini.

Nimeona maoni kama haya haya ya mtoa mada ambaye vile vile inaelekea ni mwana CCM:

Nimesoma gazeti la NIPASHE leotarehe 9 Oct. 2012, Katibu Mkuu Mukama akijibu tuhuma za Sumaye kuwa azipeleke kwenye vikao husika.Tunasahau kuwa waamuzi wa mustakabali wa chama ni wanachama wanaoona yanayoendelea hukohuko mitaani.
Tumeona jana ngumi na kurushiana viti katika kikao cha uchaguzi huko Musoma, sababu ikiwa hiyohiyo rushwa.

Mukama akisubiri kuletewa hoja ofisini, basi uhalali wa chama kwa wanachama wake utaendelea kushuka.

Wahenga walisema mwenye masikio na asikie!
 
KWA NINI CCM KITAFUNWE KWA KASI KUBWA AJABU NA MBINU ZAKE ZENYEWE ZA UCHAKACHUAJI ULIOTUKUKA KATIKA CHAGUZI ZAKE NDANI AU NDIO KUSEMA UNABII JUU YA HATIMA YA CHAMA HIKI NDIO SASA KUTIMIA??

Mkuu asante kwa kupenda kuona CCM kisichochakachua manbo kila wakati.

Nasema asante kwa kutamani kuona DEMOKRASIA katika uhalisia wake isiobughudhiwa hata kidogo na saratani za UDINI, UANAMTANDAO, UKANDA NA UKABILA.

Nashukuru pia ulivyoonyesha mpenzi makubwa kwa kutoa maoni yako yaliojawa uchungu mkali toka kwenye sakafu la moyo wako na kuwataka viongozi wako wwe ni wenye KUWAFUATA WANANCHI WALIPO NA KUSHUGULIKIA MALALAMIKO YAO HUKO HUKO bila kuendeleza umangimeza na kiburi cha kukaa kitako kwenye viyoyozi maofisini KUTEGEMEA KUFIKISHIWA KILA KITU HUKO HUKO.

E baba weeee, kidogo hadi hapo naona kama vile uko kwenye usingizi mzito ukidhania ya kwamba hiki CCM-Ukoloni Mamboleo ambacho hivi sasa kiko rasmi katika udhibiti wa lile kundi hatari la MAFISADI eti unakichukulia kuwa sawa na ile CCM ya Mwalimu Nyerere ya miaka ile; pole sana hadi hapo.

HULKA na tabia mbaya ya ukabila, ukand, udini pamoja n uanamtandao kuwa ni misingi rasmi ya watu KUCHAKACHUANA hakika ndio sanda na jeneza la chama hiki pachaka kutoboka jumla hivi karibuni kote nchini.

Nasema kama CCM ni kile kile kilichojaa kiburi cha kobe, UFISADI wa jogoo kujihisi kila tetea ni halali yake, nasema kama CCM ni kile kile chenye 'U-MIMI' kwa na mslahi ya umma wa Tanzania badaye, kamwe hakutosikilizwa mtu hapa; si Mhe Sumaye wala melf ya wanachama wengine kibao ambao nao wamefikwa na madhila kama haya haya.

Mkuu, hadi hivi sasa ni kwamba ombi lako limefikia patupu patupu na kamwe hiki CCM tunachokifahamu vema sana tu wala hakiwezi kubadilika hata kwa dawa kwa kuwa fitina na majungu ndio sala zao za kila siku iwe ni asubuhi, mchana au usiku.

Mwisho, nimalizie kwa kusem ya kwamba unabii wa kale juu ya chama hiki kikongwe sasa waja kwa kasi ajabu leo hii kuliko hata hapo jana.

Ajabu zaidi leo hii ni kwamba hata zile salam za wanacha wakulima na wafanyakazi wa miaka hiyo kwa kusema
'KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI' leo hii imebadilika kabisa huku matajiri wachache wakiwa ndio wamekihodhi chama humu wakijibunia salam yao mpya ya 'KIMUDU CHAMA CHA MAPINDUZI' ambapo mtokeo yake ndio kama hivyo dhuluma kwa kwenda mbele kwa kila kitu wanchoweza kukitia mikononi na kukimudu vilivyo kwa faida ya wachche.

Kama watu mlikua hamjui bado tu; CCM ya leo 'KINA WENYEWE' na wenyewe hao si MKULIMA wala MFANYAKAZI tena hivyo unapolia kilio cha mtu mzima hivi mbele ya kandamnasi wengine huku tujajiuliza eti 'kwani bado alikua hajui tu CCM ya leo hati miliki yake kuwa chini ya makucha ya MAFISADI ORIGINAL without apology???????'
Asante mkuu Uwezo Tunao kwa kuonyesha kukerwa kwako na mwenendo wa rushwa ndani ya chama chetu.

Ni vema tunaokitakia mema chama chetu tusipokata tamaa, kukumbushia mwenendo sahihi wa chama kwa maoni ya wanachama wa kawaida kabisa.
Maana historia inatufundisha perseverence ya good governance ndio njia ya kubaki na uhalali wa kuitwa chama cha wananchi.

Dalili za kuwa mambo si mema ni kule kutishiana bastola, kurushiana viti na ngumi na hata kudhulumiana-yote haya eti kwa ajili ya kumtumikia mwananchi.

Je , ni kwa ajili ya kumtumikia mwananchi au kwa ajili ya matumbo ya watu wanaopigana cheo kufa na kupona ili apate nafasi ya kujineemesha?

Dalili za nje za rushwa zimekwisha jitokeza, na hata TAKUKURU wakiwekwa man-to-man tatizo hili halitakwisha, mpaka mizizi yake ing'olewe, na ionekane inag'olewa.
 
Mwisho wa CCM ni uchaguzi ujao, baada ya michezo michafu itakayo fanyika katika kuteua wagombea wa ubunge uchaguzi ujao na kama siasa zao zitakuwa zilezile za kifisadi. CCM ishinde au ishindwe uchaguzi ujao ndio mwisho wao, unless hiki chama kweli kirudi kwenye maadili ya uongozi vinginevyo hili ni sikio la kufa..........
 
Majuzi Fredrick Sumaye, Waziri Mkuu Mstaafu wa Jamhuri ya Mwungano wa Tanzania, aliwaita waandishi wa habari kuwaelezea kile kilichoitwa rushwa mpya katika chaguzi za ndani za CCM. Katika kulijadili hili, tuiangalie dhamira na uadilifu wa SUMAYE, na kisha nafasi ya SUMAYE katika kuenzi au kuipiga vita rushwa.

Katika mkutano wake na waandishi, SUMAYE alitaka kuwaaminisha waandishi na watanzania kuwa yeye ni mtu safi, mtu asiyependa rushwa. Na kwa maneno yake alitamka kuwa atapigana ndani ya CCM kuondoa mfumo unaopalilia uongozi wa rushwa.

Katika kuitafakari kauli hiyo ya SUMAYE, tumjadili SUMAYE kama kweli ni mtu mwenye uwezo wa kupigana na rushwa, na pia tuangalie, na kisha tujiulize: Je, SUMAYE atapigana na rushwa za ndani ya CCM ili yeye SUMAYE asiye na uwezo wa kupata hela ya kutosha kuhonga aweze kushinda, au atapiga vita rushwa kwa sababu anaichukia rushwa?

Napenda kuwakumbusha wachambuzi kuwa ni huyu SUMAYE akiwa waziri mkuu ndiye aliyekuwa mtetezi mkuu wa ile rushwa walioianzisha CCM na kuiita TAKRIMA. Hakuna aliyekuwa mtetezi mkuu wa TAKRIMA wakati ule kumzidi SUMAYE. Ni huyu SUMAYE ndiye aliyewaambia vijana na wafanyabiashara mara kadhaa kuwa, 'ukitaka biashara yako istawi, lazima uwe ndani ya CCM'. Ni wakati wake vijana wengi ili wasisumbuliwe na polisi, askari wa jiji na TRA waliamua kuchomeka bendera za CCM ili kuepuka usumbufu. Na kwa upande mwingine, kauli yake ilidhihirika kwa wale wafanyabiashara ambao walionekana kushabikia upinzani, baadhi yao walifilisiwa kwa kuitumiaa TRA, na wengine kupitia mamlaka za miji.

Ndani ya CCM hakuna kiongozi hata mmoja ambaye hajawahi kupokea rushwa au malipo yasiyo halali. Ni CCM ndiyo walioasisi malipo ya kukaa (sitting allowance), ambao ni wizi uliopewa kanuni ya kuulinda. Ni CCM ndiyo walioasisi malipo anayopewa Rais, Makamu wa Rais, Waziri Mkuu, Mawaziri na Manaibu, ambayo wanaiita officiation allowance. Hii ni posho ya kukata utepe wanapofungua miradi au kuizindua. Huu nao ni wizi wa hela ya Watanzania unaolindwa na nyaraka zilizoandaliwa na wezi wenyewe, akiwemo Sumaye.

UKWELI: Sumaye hana tofauti na viongozi wengine wa CCM. Hakuwahi kuwa na tofauti na hata sasa haonekani kuwa ni tofauti. Kauli alizozitoa ni za chuki kwa wana-CCM wenzake watoa/wapokea rushwa baada ya kuona hana uwezo wa kuwashinda. Ni vema Watanzania na waandishi wa habari mngemwuliza ushiriki wake wa kuanzishwa na kupalilia rushwa kwa kuipamba kwa neno, 'TAKRIMA'. Tunamshukuru Mtikila aliyeipinga kwa nguvu zote, na kueleza wazi kuwa TAKRIMA ni rushwa, na kisha mahakama kuridhia kuwa kinachoitwa na CCM TAKRIMA, ndicho watu waadilifu hukiita RUSHWA.
 
Sumaye ni mnafiki alipokuwa PM aliwataka wafanyabiashara wajiunge na na CCM ili mambo yao yawanyookee! pia CCM na RUSHWA ni pete na kidole!! Inamaana anajua leo??
 
Nafikiri nilesema toka mwanzo kuwa, sina uhakika kama Sumaye angetoa tamko hilo KAMA angeshinda U-NEC.
Pengine hayo aliyoyatamka yangefagiliwa chini ya carpet na kuyasahau.
Uongozi mara zote ni mtamu, na unapumbaza uwezo wa kuyaona machungu ya wananchi wa chini.
Mifano mkuu Bamsa uliyotoa ni ya kweli kabisa, na Sumaye alitamka hilo.

Lakini turudi nyuma na kuangalia facts, je aliyosema hayafanyiki?
Si nayeye Sumaye yuko nje ya madaraka ndiyo anyaona?
Angepeta na kujiunga na wenzake angeyaonaje hayo aliyoyatamka.

Sasa kwa vile Sumaye, akiwa pro-CCM, akitamka kuwa rushwa ipo na inagwawiwa ili kupata uongozi , hilo ni kweli si kweli.
Na wewe Bams, unaisapoti au la, kwa vile kasema Sumaye basi suala hilo halipo!
Mhukumuni Sumaye kwa yake na lakini ukweli utabaki kuwa pale pale. Sumaye naye anajua kuwa misingi walioijenga tokea TAKRIMA sasa imegeuka kuwa dudu kubwa limaloitwa Rushwa mtandao, dudu hili sasa limemmeza hata Sumaye mwenuewe!!

Lakini tahadhari iko pale pale, rushwa itabaki kuwa adui wa haki kwa wanyonge, na uongozi sasa ni gulio.
 
Mwambieni Fredrick Tluway Sumaye that he should not cry wolf; Sumaye is the longest serving prime minister in Tanzanias History; na kama kiongozi wa shughuli za serikali bungeni kwa kipindi cha miaka 10 alisimama kidete na spika wa bunge la 9 Pius msekwa kutetea TAKRIMA; wakidai kuwa sio hongo bali ni bhakshishi au asante au pole kwa kazi; wapinzani walipata wakati mgumu sana kujenga hoja ya kuonyesha uovu wa takrima katika siasa za nchi yetu wakati huo na walikwamishwa pamoja na wengine akiwemo Sumaye.
leo hii haiingii akilini kwamba Sumaye ndiye analalamikia rushwa na ghiliba katika chaguzi za CCM? huo ndio utaratibu wa CCM na modus operandi yao ambayo akiwa madarakani waliitumia kuwaghilibu wenzake wengi tu!

leo ameonja shubiri ya takrima anapiga kelele, hatudanganyiki. kiendacho hurudi.
 
Sumaye ni mnafiki mkubwa sana.

Rushwa na Ufisadi ni kitu cha kawaida ndani ya CCM, kwa sasa ndio Operating System ya chama.

Sasa Sumaye hawataji hao wala rushwa, hapeleki mashtaka TAKUKURU, hapeleki malalamiko kwenye chama, wakati huo huo anasema anaendelea kuwa na imani kubwa na CCM na serikali yake!!!

Huyu jamaa atakuwa ni mtambo tu.
 
Nina choweza kusema hapa ni kwamba CCM ilipofikia kwa sasa ni utimizaji wa ule msemo wa:

SIKIO LA KUFA HALISIKII DAWA!

R.I.P.
BORN: 5/2/1977
DIED:_/10/2015
 
Mkuu unaipa tahadhari CCM dhidi ya rushwa? Unatilia maanani kauli ya Sumaye? Bado hujakubali kuwa motisha (incentive) inayowavutia wengi kugombea nafasi za uongozi katika chama hicho ni fursa kadhaa za kifisadi ikiwemo rushwa, ukwepaji kodi, dili za kila aina, n.k. bila kuguswa na sheria wala kubugudhiwa na taasisi za dola? Basi angalau mkumbushe kwanza Sumaye aikane kauli yake maarufu kwa wafanyabiashara kama "wanataka mambo yao yawanyokee ...". Ukiondoa fursa hizo za kifisadi, CCM haipo! Hakuna ndani ya CCM asiyejua madhara ya rushwa na umuhimu wa kuipiga vita kwa mustakabali mwema wa chama lakini ndio hivyo tena; anayeipiga vita rushwa kwa dhati SI MWENZAO!
 
Mkuu huo ndio ukweli wenyewe, sasa nimkuwa nikitafakari sana juu ya kilio ch viongozi wetu juu ya utawala bora.

I dont know what the hell that means now!
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom