TAHADHARI: ATM ZA Standard Chartered Bank

Kachanchabuseta

JF-Expert Member
Mar 8, 2010
7,269
675
WanaJF nawapa tahadhari na ATM hizi za SCB.

Jana mida ya sa 5 asubuhi nilienda kudraw hela kutoka ATM ya SCB HQ, nilicommand laki 3 ATM machine ikarun HAIKUTOA HELA ikanipa list kwamba nimetoa LAKI TATU. Nilikaa nimeduwaa kilichotokea ikabidi niwambia wanaonifuata wasitoe hela, niliingia ndani kumueleza Bank officer what happen.

Bank offer kwa Jeuri ananiambia mimi tapeli hela nimechukua ikabidi nimshike mkono mpaka kwa wale mashuhuda niliowaacha kwenye foleni wakamwambia hela hazijatoka.

Long story......

Mwisho tukafika kwa Branch manager nikapewa hela Yangu

Swali:

1. Kama ATM zinakosea kihivi je ukipata tatizo siku ya weekend ndo hutapata hela yako??
2. Je inawezekana huu ni mradi mdogo kwa baadhi ya Mabank officer??
 
mkuu pole sana, nilihama standard 2003, niliacha atm zao zikiwa bomba, sasa nipo kcb hayo mambo unayoyasema huko kcb ya kawaida kila kukicha wanafanya mambo ya kustaajabisha. mwe! pole sana
 
Writing fiction is great. You can say anything you want.

Kwa nini unamwambia mwenzako hivyo? Ikiwa wewe haijawahi kukutokea haina maana kwamba huwa haitokei.

Azungumzie fiction ya kitu kama hicho kwa manufaa ya nani, au una shares katika hiyo bank?
 
Hicho kitu nadhani sio kigeni kwenye ATM sekend hand za kibongo.

Nakumbuka CRDB kilishanitokea kitu kama hicho, bahati ilikuwa weekday kwenda ndani wakaniambia watanirudishia hela yangu baada ya masaa 24.

Bongo tambarareeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee
 
Same experience from NBC. Walikula hela zangu na nilikuwa safarini siku ya weekend. Nilipofika Dar es salaam niliriport kwenye branch ya benk yangu akanambia natakiwa niifuatilie kwenye tawi husika. Kwa hiyo ikawa imekula kwangu. In general, benk zetu zina shida.
 
Hicho kitu nadhani sio kigeni kwenye ATM sekend hand za kibongo.

Nakumbuka CRDB kilishanitokea kitu kama hicho, bahati ilikuwa weekday kwenda ndani wakaniambia watanirudishia hela yangu baada ya masaa 24.

Bongo tambarareeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee

Abdulhalim nadhani nilisoma hapa hapa Jamii. Jamaa alikuwa na kawaida ya kutoa mabulungutu kupitia ATM na bila kuhesabu kuzitia mfukoni na kuendelea na hamsini zake. Siku hiyo alikuwa anakwenda kununua kitu kama nakumbuka vizuri kilikuwa ni laki nne, akapitia bank kwenye ATM na kutoa pesa hizo kufika huko akalipa hela alizotakiwa kuzilipa akijua zimetimia lakini mwenye duka akamwambia kulikuwa na upungufu wa 80,000 jamaa alipigwa na mshangao wa mwaka. Alipoandika akasema basi kishaabiwa sana maana yeye hakuwa na kawaida ya kuhesabu pesa kila anapotoa toka ATM. Huziweka mfukoni na kunaza kunyofoa kidogo kidogo kila alipohitajika kununua kitu. Kwenye hizo ATM muwe waangalifu mno hasa mnapotoa kiasi kikubwa cha pesa. Hakikisha unahesabu na kama kuna tatizo uombe waliyo nyuma yako wawe mashahidi wako vinginevyo unaweza kabisa kuibiwa.
 
Jamani poleni mie NBC niliomba kutoa 30,000/= ndiyo ilikuwa imebakia, lakini ATM ikanipa 300,000/= hawajashtuka hadi leo!!!!!
 
Abdulhalim nadhani nilisoma hapa hapa Jamii. Jamaa alikuwa na kawaida ya kutoa mabulungutu kupitia ATM na bila kuhesabu kuzitia mfukoni na kuendelea na hamsini zake. Siku hiyo alikuwa anakwenda kununua kitu kama nakumbuka vizuri kilikuwa ni laki nne, akapitia bank kwenye ATM na kutoa pesa hizo kufika huko akalipa hela alizotakiwa kuzilipa akijua zimetimia lakini mwenye duka akamwambia kulikuwa na upungufu wa 80,000 jamaa alipigwa na mshangao wa mwaka. Alipoandika akasema basi kishaabiwa sana maana yeye hakuwa na kawaida ya kuhesabu pesa kila anapotoa toka ATM. Huziweka mfukoni na kunaza kunyofoa kidogo kidogo kila alipohitajika kununua kitu. Kwenye hizo ATM muwe waangalifu mno hasa mnapotoa kiasi kikubwa cha pesa. Hakikisha unahesabu na kama kuna tatizo uombe waliyo nyuma yako wawe mashahidi wako vinginevyo unaweza kabisa kuibiwa.

Benki za bongo ni full loaded comedy.

Last year nilienda kwene branch yangu ya CRDB nikamuuliza mhusika ni procedure gani za kufuata ili kupata credit card, akadai eti CRDB haitoi credit cards. Nikasema these people are recruiting funny faces, yaani huyu ndio reliable person kwene hili tawi anasema CRDB haitoi credit cards??? Hivi hawa jamaa huwa wanapewa crash course walau kuijua kampuni wanayoifanyia kazi??

Kama ni hivi bora waje wazungu na mabenki yao waje kuchuma.
 
Ungemuuliza na kama wanatoa 'debit card' pia?
 
ni jana tu hapo arusha, nimeingia kwenye atm ya crdb hata cjaingiza kadi yangu nikakutana 35 elfu, inaelekea mashine ilikuwa na shida na mtu alienda kutoa 35 elfu may b akasubri kwa muda akaona hazitoki akaondoka, kumbe nyuma zimejitoa...hakukuwa na mtu hata mmoja zaidi yangu!
 
Nyamayao,

Hiyo pesa ulirudisha kwa Banki au ndo hivyo tena ulisepa nayo?
 
Hicho kitu nadhani sio kigeni kwenye ATM sekend hand za kibongo.

Nakumbuka CRDB kilishanitokea kitu kama hicho, bahati ilikuwa weekday kwenda ndani wakaniambia watanirudishia hela yangu baada ya masaa 24.

Bongo tambarareeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee

True, mimi ilishanitokea kama mara tano hivi but ni mara moja nilicomplain wakaniambia itarudishwa then hizo nyingine nilisubiri baada ya muda wanarudisha. Wanasema baada ya reconciliation zinarudi.. well zinarudi lakini why inakuwa hivi ndo sina jibu.
 
Back
Top Bottom