Tahadhari: Aina mpya ya utapeli yazuka Dar

MwanaHaki

R I P
Oct 17, 2006
2,401
705
Moderators, sijui kama hapa ni mahala pake, lakini mtajua wenyewe pa kuipeleka hii. Nimeinyaka sasa hivi!

Kuna aina mpya ya utapeli ambayo imeingia jijini Dar. Kuna wajanja fulani ambao wanatumia fursa ya kwamba kila anayepigiwa kelele za Mwizi Mwizi Mwizi hadharani atasulubiwa bila ya kuhojiwa, wamezua mtindo wa kuwaomba watu simu zao, wajifanye wanabip, kisha wanapigiwa, wanawaomba waliowapigia wawatajie namba ya simu waliyoitumia - kwa kuwa ni washirika wenzao katika dili - ili baadaye waje kudai kuibiwa simu.

Katika purukushani ya kumtafuta Mwizi huyo wa simu, ambaye si mwizi, ila yule ambaye anayedai kuibiwa ndiye mwizi halisi, inatajwa namba ya simu inayodaiwa kuibiwa. Inapolia, inaita kwa mtu ambaye si mhusika, hapo hapo anaanza kusulubiwa bila kuhojiwa.

Hii tabia mbaya yetu sisi kuamua kuchukua sheria mkononi pasi na kuhoji ukweli wa tuhuma sasa inawafikia pabaya raia wema. Kaeni chonjo, msije kuitwa wezi. Ushauri: Mtu usiyemfahamu akikuomba simu yako akabip kataa kata kata, mwambie simu yako haibip hata siku moja, anakushusha hadhi! Akisema si wewe unayebip, unamwambia hata kama si wewe! Akileta za kuleta unamkata kibano cha nguvu na kumpigia kelele za Mwizi Mwizi, wamsulubu yeye!

./Mwana wa Haki
 
Hii ni ya zamani ..labda kama wadau wengine mlikuwa hamjaipata. Watch out guyz..
 
"Mtindio wa Ubongo" sikubaliani na hoja yako kwa kuwa kila mara masuala haya yanahitaji kuwakumbusha watu wachukue tahadhari. Kama ni wa zamani inakuwaje aliyeleta anaona ni utapeli mpya? Inakupunguzia nini kuweka msisitizo? Mwanahaki uko katika mstari achana na longolongo za watu wengine.
 
"Mtindio wa Ubongo" sikubaliani na hoja yako kwa kuwa kila mara masuala haya yanahitaji kuwakumbusha watu wachukue tahadhari. Kama ni wa zamani inakuwaje aliyeleta anaona ni utapeli mpya? Inakupunguzia nini kuweka msisitizo? Mwanahaki uko katika mstari achana na longolongo za watu wengine.

Sijaelewa kwa nini unakuwa hysterical.

Nilichosema ni kuwa aina hii ya wizi si mpya kihivyo,ni uwizi ambao una zaidi ya miaka 2! na hata hivyo nikasisitiza watu wawe waangalifu na kujihadhari..Kama hujaelewa kitu ni vizuri uulize na sio kukurupuka kama mtu aliyemwagiwa ndoo ya barafu wakati akiota anapaa angani.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom