Tafuteni umaarufu bungeni kwa kujenga hoja si vurugu

singidadodoma

JF-Expert Member
Nov 11, 2013
4,394
1,531
NI wiki nyingine muhimu katika ulingo wa siasa za hapa nchini. Mkutano wa pili wa Bunge la 11 unatarajiwa kuanza keshokutwa. Tunasubiri kushuhudia kasi ya Bunge hili ndani ya Serikali ya Awamu ya Tano. Bila shaka litaendana na kasi ya Serikali ya Awamu ya Tano chini ya kaulimbiu ya ‘Hapa Kazi Tu’.

Matamanio yangu ni kuona kasoro zilizowahi kujitokeza katika mikutano iliyopita, hususani vurugu zinazoambatana na zomea zomea, vijembe, matusi na kususa, zikiwekwa kando katika Bunge hili. Naomba Mungu, Bunge hili lenye watu wa rika na taaluma mbalimbali, lioneshe nidhamu, weledi, busara na utendaji uliotukuka.

Kwa mujibu wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) , wabunge wenye umri kati ya miaka 21 na 35 wako 47, wenye umri kati ya miaka 36 na 50, wako 112 na walio na umri wa zaidi ya miaka 51, wako 91.Natamani damu changa iliyoingia katika Bunge la sasa, iwe chachu ya kufanya kile ambacho wananchi wamewatuma wawafanyie. Kwa kuwa tunaambiwa ‘utu uzima dawa’, pia wabunge wenye umri mkubwa, wawe chachu siyo tu ya utendaji uliotukuka, bali pia wawe mfano bora wa maadili na nidhamu bungeni.

Idadi kubwa ya vijana iwe chachu ya kufanya vizuri na iondolee jamii dhana potofu iliyojengeka kwamba wanaweza kugeuza Bunge uwanja wa kujipima ubavu wa kuongea badala ya kujenga hoja.Upo ukweli kwamba, baadhi ya wabunge bila kujali rika, wamekuwa wakitafuta sifa na umaarufu kwa gharama yoyote ikiwemo kufanya vitendo visivyofaa bungeni.

Matokeo yake, huligeuza uwanja wa mapambano, jazba, mipasho na matusi. Kwao kutukana, kubeza na kudhalilisha wengine, huchukulia ndiyo umahiri wa siasa jambo ambalo si sahihi. Huwa inashangaza kuona mtu mzima, msomi, mwenye familia na aliyeaminiwa na wananchi, anafanya mambo ya kitoto na ya ajabu.

Ukiuliza sababu za kufanya hivyo, utajibiwa eti hizo ndizo siasa na sifa ya mabunge ya mfumo wa vyama vingi! Baadhi ya wabunge huona sifa kutajwa tajwa bungeni kwa kuonywa na Kiti cha Spika au na wabunge wenzake.

Wengine huona sifa kuondolewa bungeni au kutakiwa kuondoa kauli za kudhalilisha dhidi ya wenzao. Bahati mbaya, chini ya siasa za vyama vingi, wabunge wa aina hiyo wakibanwa na kanuni, hutafuta huruma kwa kuhamishia suala hilo kwenye ushabiki wa vyama.Kwa mfano, unakuta mbunge wa chama tawala anatoa lugha isiyo ya staha dhidi ya upande mwingine na wenzake hawako tayari kumkosoa. Vivyo hivyo wa upinzani, anapofanya hivyo, anabaki akikingiwa kifua na wabunge wa kambi yake.

Jamii pia huziba macho na masikio juu ya utovu wa mbunge husika, na kuchukulia suala hilo kwa mtazamo wa siasa za vyama.Wakati macho na masikio ya Watanzania yakielekezwa bungeni mjini Dodoma, chonde Kiti cha Spika kiwe macho na wabunge wanaochafua chombo hicho kwa kusaka sifa na umaarufu kwa utovu wa nidhamu.

Kiti cha Spika kihakikishe kanuni na taratibu za Bunge zinaheshimiwa na kila mmoja bila kujali chama anachotoka wala nafasi yake. Spika adhibiti mihemko inayoambatana na lugha zisizo za staha ndani ya Bunge kwa kuhakikisha wanaokwenda kinyume wanaadhibiwa kwa mujibu wa kanuni.

Ingawa wabunge watakuwa wamepewa semina elekezi, Kiti cha Spika kisichoke kuendelea kuwafunda wote wapya na wa zamani juu ya heshima, nidhamu, uadilifu katika kuwasilisha ujumbe bungeni kuepuka kuligeuza gulio. Kiwafunde watambue kwamba wao ni viongozi wa nchi ambao hawakufika mahali hapo kwa bahati mbaya, bali wameaminiwa na umma wa Watanzania. Spika asiogope kutumia rungu lake kwa yeyote atakayekwenda kinyume na kanuni.

Rungu hilo litue kwa yeyote bila kujali chama, umri, jinsi na wadhifa wake . Kiti cha Spika kihakikishe Mkutano huu wa Pili wa Bunge la 11, hauwi mwendelezo wa jukwaa la uchaguzi . Nafahamu wazi kwamba, Spika atakapoamua kushusha rungu lake kwa mujibu wa kanuni na taratibu, wapo watakaoona kana kwamba wanaonewa. Lakini Kiti, chini ya Spika Job Ndugai, kisiangalie uso wa yeyote. Atakayepanda vurugu na lugha zisizo na staha bungeni, naye avune adhabu stahiki.

Yale mazoea ya kusema wabunge (hasa wapya) bado wanajifunza kwanza, yasipewe nafasi tena kwani ndicho chanzo cha matatizo. Kanuni za Bunge zizingatiwe tangu siku ya kwanza. Zikitumika vizuri, wabunge wataka sifa, umaarufu na wanaojifanya wapambanaji kwa kufanya vitendo visivyo na staha, hawatapata nafasi kuvionesha. Nasisitiza, umma wa Watanzania unataka maendeleo ndiyo maana ukawatuma bungeni. Wanataka kusikia hoja zenye maslahi kwao.

Kwa upande wa wabunge wasomi, onesheni uwezo wenu kwa kutoa hoja na kuuliza maswali yenye ‘akili’. Hata wabunge wasio na kisomo, wajisomee kuepuka kupoteza muda wa vikao kwa maswali mepesi mepesi. Kwa ujumla, umaarufu wa wabunge unapaswa utokane na hoja wanazotoa na si kwa kuwa vinara wa vurugu na vitendo vya ajabu bungeni.
 
Sijui unaposema 'utovu wa nidhamu' una maana gani! Kwani kuna wabunge wanaoweza kuwa na hoja nzuri na yenye tija kwa taifa ila ikaminywa na kutotakiwa kabisa hiyo hoja kisa tu imetoka kwa upande flani! sasa hapo aliyesababisha 'utovu wa nidhamu' ni nani?
 
Leo watanzania wamejionea ni wabunge Wa upande gani wanaoleta vurugu Bungeni. Tunamshukuru kwa hii kurusha live inatuonesha uhalisia wa vurugu Bungeni.

Queen Esther

Mheshimiwa Zitto ameonesha kabisa kwa dhati NIA Yake ya UBINAFSI ili asifiwe na mitandao ya kijamii kuwa yeye ndiye kaongoza au kaleta hoja ya kutengua kanuni nk.

Zitto ni MNAFIKI na tabia hiyo anayo muda mrefu. Leo kila mtu ameona wanaopoteza muda na kuleta vurugu Bungeni ni kina nani. Zitto hako katabia ndio kalikufanya ukafukuzwa CHADEMA. Bado unaendelea na hako katabia. Jitahidi ukue sasa uwe mwanaume.

Hoja zipo lakini zinazimwa na spika hivyo lazima zilazimishwe kupitia 'vurugu' kuliko kukubali kila kitu ' ndiyoooooooo'!
 
Yani leo Lissu na Zitto nimewashusha vyakutosha sana , kumbe wanatafuta umaarufu tu bungeni wala hawana kitu kichwan mwao mafunza tu
 
Wabunge wengi hawaelewi maana ya kazi zao, wanafikiri kukosoana tu ndio kazi ya mbunge , lakini hata wananchi wenyewe hawajui wanamchagua mbunge kwa kazi gani,kwa hiyo hakuna wa kumlaumu.Wacha wauze sura,mpaka wananchi watakapo pata mwamko na uelewa kwanini wanamchagua mbunge.
 
Kweli kabisa...
leo nimemuona serukamba na mama nagu wanajibu maswali kama mawaziri ....
Hakika spika kapwaya saaana wala hakuna utaratibu mzuri bunge linaenda kienyeji
 
Ku
Leo watanzania wamejionea ni wabunge Wa upande gani wanaoleta vurugu Bungeni. Tunamshukuru kwa hii kurusha live inatuonesha uhalisia wa vurugu Bungeni.

Queen Esther
Queen,,unashukuru kwa kipindi cha bunge kurushwa live tena??si ndo wewe uliyekuwa unasupport uamuzi wa TBC kutokurusha matangazo ya live??,,
 
Soma post yangu ya mwisho kwenye agenda ya Bunge kurushwa live niliandika "MTOTO AKILILIA WEMBE MPEEE!!!"

Bunge la Ijumaa Mhe. Kafulila alilamba garasha kwa hoja ya chupi na shanga. Hiyo ilikuwa live na hao wananchi wamesikia na hawana hamu. Wanasema kumbe ndio maana mlitaka kuwa live ili watoto wasikie matusi. Watoto wanauliza Bunge wanagawa shanga ndio maana wamevuliwa????? Imagine changamoto ya majibu kutoka kwa mzazi.

Leo Mhe. Lissu kaingia chaka, nae kaingizwa king kila mtu kaona live bila chenga!! Mhe. Zitto nae alitaka kumfunika Mhe. Jenista Mhagama. Hakujua huyu ni mama wa shoka. Aibu Yake Mhe. Zitto. Sifa sio nzuri!!!

Kuna wabunge Wa upinzani walikuwa wanaomba miongozo wamepewa nafasi waongee wakafuta kauli. Leo tamthilia ya upinzani na mauzauza ya kupoteza muda yalikuwa wazi wazi. Na bado!!!!

Mwisho tu naomba ule mpango wenu Wa mwaka mmoja muurushe humu tuujadili!!

OK,,hivyo tuseme ulikuwa unataka kuwaponya ukawa ili wasipatwe na unachokiita aibu??je ,,hiyo ndiyo ilikuwa nia yako tangu mwanzo ulipounga mkono swala la bunge kutokurushwa live???,,
 
Leo watanzania wamejionea ni wabunge Wa upande gani wanaoleta vurugu Bungeni. Tunamshukuru kwa hii kurusha live inatuonesha uhalisia wa vurugu Bungeni.

Queen Esther
Iache iendelee live. Wananchi siyo wewe tu.
 
Mkuu hoja wasitoe wapi kwa hii kasi ya Magufuli? zimebaki za kumulika na tochi tu....otherwise unaweza ukakufuru jamaa aendelee tu hadi Mungu atakapomchukua, tusifanye uchaguzi wa Rais tena
 
Mheshimiwa Zitto ameonesha kabisa kwa dhati NIA Yake ya UBINAFSI ili asifiwe na mitandao ya kijamii kuwa yeye ndiye kaongoza au kaleta hoja ya kutengua kanuni nk.

Zitto ni MNAFIKI na tabia hiyo anayo muda mrefu. Leo kila mtu ameona wanaopoteza muda na kuleta vurugu Bungeni ni kina nani. Zitto hako katabia ndio kalikufanya ukafukuzwa CHADEMA. Bado unaendelea na hako katabia. Jitahidi ukue sasa uwe mwanaume.

Queen Esther
Unataka Zitto akuoe! Chuki gani hizi! Au ulimtaka akachomoa? Punguza chuki,zitakuua we mwanamke.
 
Haya mkulima wa kiteto naona umeandika vema jana ulilala Lusaka au riverrine bila shaka hahaah
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom