Tafakarini kwa makini hili....

Mwanamageuko

JF-Expert Member
Oct 31, 2010
8,602
5,569
“Kwa sisi kugomea hotuba ya Rais, tunajua ujumbe wetu umefika kwa wahusika wakiwamo bwana mkubwa mwenyewe (Rais Kikwete), viongozi wa mashirika na taasisi mbalimbali na mabalozi, kuonesha kuwa kuna tatizo la msingi ambalo Chadema inataka lishughulikiwe.

“Tunajua kuna watu wameudhika, na tunajua kuwa hatukumfurahisha Rais, lakini ujumbe wetu umefika.

Kuna baadhi ya watu wamepotosha kuwa tunampinga Rais. Haikuwa nia yetu kutaka avuliwe urais au aondolewe ofisini, tulitaka aone kuwa kuna tatizo ambalo linatakiwa kushughulikiwa na yeye ndiye mhusika.”

Mbowe alisema hoja ya kwanza ya Chadema ni kuona umuhimu wa kuwa na Katiba mpya
itakayoliwezesha Taifa kujenga misingi imara ya demokrasia na kuifanya nchi kuwa na amani, itakayokalika na kila mtu bila kujali kabila, dini au chama chake cha siasa.

“Tunataka Katiba ambayo itamfanya kila Mtanzania aishi kwa amani na upendo, mfano mzuri ni Zanzibar, walikuwa na tatizo kama hilo lakini sasa wamelishughulikia, kwa kuwa na Katiba nzuri na wamekubaliana kuendesha mambo yao … si unaona kila mtu anafurahia
hili na wote wanaishi kwa amani kabisa?” alihoji.

Nimenukuu Nimewasilisha
 
Back
Top Bottom