Elections 2010 Tafakari picha hii na linganisha na mdahalo wa leo

ndugu nakupongeza sana kwa ujuzi wako kwa maana umeweza ku summarize mkutano wa JK na media wa masaa
matatu kwa kutumia picha moja. hongera sana.
 
hawa media sasa hivi ni mawakala wa vyama sometimes wanatumiwa bila kujua. Ndio njaa tuwasamehe tu bure na tuwaelimishe
 
What's up with hii kwamba TV zote zimeonesha hii kampeni event ya kilaza Kikwete na wakati walichunia za Slaa (na Lipumba)?
 
What's up with hii kwamba TV zote zimeonesha hii kampeni event ya kilaza Kikwete na wakati walichunia za Slaa (na Lipumba)?
hizi television zetu zina unafiki mwingi sana. Unapomeza media na kuiendesha kama unavyotaka, umeshaliteka taifa. Mdahalo wa Slaa walisema wangeurudia na hata wakatangaza, then wakatuwekea mieleka. Shame on you media. The history will blame you. But not for all, maana wamechagua wale walio wa kwao.

Kuna jamaa aliweka post kabla ya mdahalo kwamba umechakachuliwa na jamaa kaandaliwa maswali na ndivyo ulivyokuwa.
 
hivi tofauti ya wale watumwa walokuwa wanawabeba mamwinyi kwenye vitanda vyao na hawa waandishi wa siku hizi nini?????

jamaa mmoja msambaa mwenzangu huko lushoto alienda sokoni akakanyagwa mguuni bahati mbaya na mzungu, mzungu kamwambia "sorry" msela badala ya ku'mind alivyorudi maskani akaanza kushangilia eti kakanyagwa na mzungu, kwake ni bahati na sifa kubwa kukanyagwa na mzungu. SASA NDO HAWA WAANDISHI WETU.
 
Mkuu hongera sana. picha hii ilichorwa na Gpdfrey Mwampemwa maarufu GADO aliyeko nairobi kenya. Aliichora just a year baada ya kikwete kusworn in.
ndicho kilichotokea leo kwamba all the media ime-bow mbele yake.
WHAT A SHAME
 
Hahaha.. Yaani wamechagua Media house zao, wakachagua na waandishi wao kudadeki ili kueneza propaganda zao, na bado mkwere asivyobebeka akaanza kutupa story zake na washkaji wake wa kizungu wanavokuja kujenga muhimbili na mambo km hayo' je hela yetu inayoliwa na wajanja vipi? mbona unawasapoti watu walio kwenye kesi za ufisadi kwenye kampeni? na yale matundu ya vyoo kule bagamoyo? Maisha bora ni vijana kuuza grocery?? Mkwere embu tuambie vizuri au unazeeka mkuu!!

9c picture aisee!!
 
Mkuu hongera sana. picha hii ilichorwa na Gpdfrey Mwampemwa maarufu GADO aliyeko nairobi kenya. Aliichora just a year baada ya kikwete kusworn in.
ndicho kilichotokea leo kwamba all the media ime-bow mbele yake.
WHAT A SHAME

Nakumbuka magazeti yetu mengi yalipiga sana kelele kuwa jamaa kawadhalilisha.....but they proved it today!!
Ile shoo ya leo ni aibu kwa taaluma ya habari hapa nchini, watu wanapoamua kutumikia "njaa" badala ya taaluma na jamii...Sikumbuki kuona mkutano wowote kwenye TV ambapo staili yake imefanana na ile ya leo..Ndio maana naelewa ni kwa nini hawakutoa mwaliko kwa watu wa magazeti maana sidhani kama kubenea,Kibanda au Jenerali wangekubali kutanguliza njaa kiasi kile.
 
ni vema kama TV zimeonyesha zimeonyesha uozo wake wakidhani wanamsaidia
 
Wanahabari hao hao waliojilipua na JK nimewasikia mara nyingi wakikemea wananchi wachache wenye njaa wanaouza haki yao ya uraia kwa tshirt na kanga. Leo wameniacha nieduwaa, nimekata tamaa, sitakaa niamini tena watakachokisema (wote wale waliouliza maswali kwa JK)
 
Safi sana msanii. Huyu Kikwete angefaa kuhojiwa na watu kama akina Vicent Makole,ushaona wapi m2 anaulizwa kuhusu 'sura' ya nchi halafu anaelezea Mkonga wa taifa? Hivi ni kipi Kikwete achoona c chema hapa tz. Kila pungufu kwake ni 'ni kweli hilo suala lipo' bt amelitatua vipi,anatoa story. Hivi watanzania wote na akina mama wajawazito walio vijijini wataenda kutibiwa Mhimbili?
 
Mkuu nimeamini kuwa wengi wetu tunafikra sawa....I hope tuko na age ambazo zinalandana...meaning that wakati wa mageuzi ukifika tutakuwa wote.

I was surprised our journalists could not address/ask Kikwete the real astonishing issues of the nation...it was badly....

anyway hao ndo wazee wetu wa baadaye wakati tutashika hatamu....

Hiyo picha ime-prophecy the real picture of media professionals are doing in the country

Hureeee mkuu
 
Kwa waliobahatika kuona katuni ya jana kwenye gazeti la mwananchi watakubaliana nami kwamba ilitabiri yatakayotokea kwenye mdahalo huo. Huwa najiuliza Masoud kipanya wa enzi za Mkapa aliishia wapi? au alishaahidiwa kupewa ukuu wa wilaya? Nini kilimtokea jana mpaka akachora ile katuni?
 
Back
Top Bottom