TAFAKARI: NEEMA YA MACHUNGU ya IRENE ISAKA KUTOKA NSSF

PICHA YA NINI WAKATI HAKUNA MFANYAKAZI ANAE PATA MSHara wa halali aneweza lipa hio pesa interest peke yake ni million 223 jumlisha na mkopo wa m 68 ni m 291 kwa bed room 2 .
unaweza jenga yako kwa m 40 bila mikwaruzo

mi naomba msaada,hivi kwa nini hao NSSF wanataka tukakope bank wakati hela zetu wanazo wao?kwa nini tukalipe riba kule wakati wao hawatupi interest?mi msaada jamani, hapa hesabu inakataa
 
Kwa milion 100 utajenga nyumba nzuri ya three rooms tena na kiwanja uwe umenunua say 10 million katika maeneo ya kawaida hata Kigamboni ambako tena sq 700 hadi 900 unaweza kupata kwa milion 15. Ati afordable houses, are they? Tanzania haina nafasi ya kuwapa wananchi wake maisha bora kwa kila mtanzania bali maisha ya uchungu kwa kila mtanzani. Sad, very sad.
 
Hapo nimekutikana na matatizo mawili
1. HISABATI
2. UNG'ENG'E
Hizo units zinamaana ni idadi ya nyumba na hiyo bei ni kila au?
 
Kwa hiyo unaishia kulipa pesa mara 3 zaidi ya uliyokopa!!

Itabidi ulipe tu kwani Irene anazihitaji hela zako ili akapige dili kubwa zaidi na wakubwa wake waliomweka hapo alipo


2d15Irene-Isaka.jpg



Hivi Mama huyo huwa ni Mmachame au? anapenda sana ngawila za watu walizodunduliza kwa mateso makubwa wakiwa kazini,

Hivi sasa nasikia wanamradi tata wa nyumba hizo wanazouza sehemu fulani na si mbali sana sikilizieni litabuma vizuri tu kwani wanajua WaTZ ni wajinga hawajui lolote na wavivu wa kufikiri
 
Nasikia jana bungeni Irene kakukumbukeni na kuwatumia sms....
"Tafadhali nipigieni"



Muswada wa mafao ya Wastaafu; [audio] Taarifa za habari TBC, Radio One
05/11/2013

Taarifa za habari kwa njia ya sauti za TBC na Radio One Stereo zimepachikwa kwenye pleya hapo chini baada ya habari ifuatayo ya Gloria Tesha via HabariLeo -

SERIKALI imewasilisha bungeni Muswada wa Sheria ya Mfuko wa GEPF wa Mafao ya Wastaafu ya Mwaka 2013 . Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Maendeleo ya Jamii imetaka uondolewe mkanganyiko wa kanuni ya kukokotoa pensheni na kiinua mgongo, kwa kuwa na vigezo vinavyofanana ili mifuko yote itoe mafao sawa.

Aidha, imeshauri Msimamizi na Mdhibiti wa Hifadhi za Jamii (SSRA) kutengeneza utaratibu maalumu katika mifuko yote ya
Hifadhi za Jamii na kubuni mfumo mpya na rahisi wa kutumia simu za mkononi, kuwafikia Watanzania wengi kujiunga na mifuko hiyo.

Kamati kupitia kwa Mwenyekiti wake, Jenista Mhagama ilitoa ushauri huo baada ya muswada kuwasilishwa bungeni na Naibu Waziri wa Fedha, Saada Salum.

"Fomula ya kukokotoa pensheni na kiinua mgongo kama inavyopendekezwa katika Muswada inatumia kigezo cha kigawo cha 1/580 wakati mifuko mingine inatumia 1/540, kadhalika kigezo kingine ni wastani wa mishahara wakati kuna mifuko inatumia mshahara wa mwisho," alisema Mhagama, ambaye ni Mbunge wa Peramiho (CCM).

Alisema eneo hilo linaleta mkanganyiko mkubwa na linatakiwa kufanyiwa kazi haraka kuainisha mafao hayo kwa mifuko yote.

"Ni maoni ya Kamati kuwa na umuhimu mkubwa sasa wa kuwa na vigezo vinavyolingana ili mifuko itoe mafao sawa bila kuathiri mifuko yote husika tofauti na ilivyo sasa," alisema.

Pia Kambi rasmi ya Upinzani Bungeni a imependekeza kuwepo kwa vigezo sawa vya ukokotoaji wa pensheni na kiinua mgongo na kupendekeza kuwa nguvu ya ziada inahitajika kuwafikia Watanzania asilimia 80 wenye shughuli binafsi.

"Unapozungumzia sekta isiyo rasmi, tunagusa takribani Watanzania asilimia 80 wenye shughuli za kujiingizia kipato kama wavuvi, wakulima wadogo wadogo, madereva wa daladala, waendesha pikipiki, fundi waashi, fundi vyerehani, wamachinga na Watanzania wengine wajasiriamali, hawa wote wanapaswa kuangaliwa," alisema Cecilia Pareso, Mbunge wa Viti Maalum (Chadema).

Akichangia muswada huo, Mbunge wa Kigoma Kusini, David Kafulila (NCCR-Mageuzi) na Mbunge wa Kigoma Mjini, Peter Selukamba (CCM) ambao kwa nyakati tofauti pia walitaka kuwepo na vigezo sawa kwa mifuko yote ya hifadhi ya jamii ili itoe mafao sawa.

Serukamba alisema suala la kuwepo kwa vivutio vya kushawishi wanachama wengi kujiunga na mfuko fulani vinaweza kubaki lakini upo umuhimu wa lazima kuweka vigezo sawa vya mafao. Aliipongeza Serikali kwa Muswada huo akisema ni muhimu kwa maendeleo ya Watanzania.

Awali, Naibu Waziri wa Fedha, Saada Mkuya kwa niaba ya Waziri mwenye dhamana Dk William Mgimwa, akitoa maelezo ya Muswada huo alisema unakusudia kufuta Sheria iliyopo hivi sasa ya Mfuko wa Akiba ya Wafanyakazi Serikalini sura ya 51 iliyotungwa mwaka 1942.

Alisema lengo la kutunga upya sheria hiyo ni kutekeleza matakwa ya Sera ya Taifa ya Hifadhi ya Jamii ya Mwaka 2008 pamoja na Sheria ya Marekebisho ya Sheria Mbalimbali za Mifuko ya Hifadhi ya Jamii ya mwaka 2012 iliyofanya marekebisho katika sheria za Mifuko yote ya hifadhi ya jamii nchini.
 
Back
Top Bottom