Tafakari Gharama za Maisha za Watanzania

msemakweli10

JF-Expert Member
Oct 14, 2013
229
46
Wana JF na watanzania wote kwa ujumla heri ya mwaka mpya.

Inasikitisha sana sana pale ambapo nchi ya maziwa na asali kama Tanzania watu wake wanaendelea kutaabika na umaskini.

Watanzania tulikuwa tunasubiri kwa matumaini makubwa upatikanaji wa nishati inayotokana na gesi. Upatikanaji wa gesi ungekuwa ni mbadala wa uharibifu wa mazingira ambapo ukataji miti ovyo ungepungua.

Masikitiko yangu ni kwamba wakati tukielekea kwenye upatikanaji wa nishati hii ya gesi, bei ya gesi imepanda badala ya kushuka ili kuwawezesha wananchi kujipatia nishati hiyo.

Mtungi wa gesi kwa kg 50 ni 63000 badala ya 54000 kama hapo awali.

Je, kwa hali hii, tunaenda wapi? Wewe mwananchi, acha ushabiki usio na tija. Fikiri kabla hujaamua.

Source: Mwananchi Newz Paper
 
michakato ndio wabongo wanajidaia.

Hivi tunawezaje kuishi kwa matumizi yafuatayo kila mwezi?

1. Matumizi nyumbani; chakula, umeme, gesi, maji, soda/juisi za wageni
2. Ada za watoto zinazolingana na za chuo kikuu
3. Matibabu hospitalini
4. pesa ya walinzi kwamwezi,
5. Sherehe za kuaga na kukaribisha mwaka mpya
6. Zaka ya kanisani na misikitini Kupanda Mbegu/ Sadaka Shukurani ya Neno
7. Tozo za Flying (wazoa taka wa mikokoteni ambao huzitupa hapo hapo)
8. Madalali wa nyumba/viwanja
9. Pango la nyumba Fremu ya biashara/ofisi
10. Mazakayo wa mitandao ya simu [airtime vouchers]
11. Mafuta ya gari Walinda/waosha magari (oya sista/blaza, mdogo wako nipo hapaaa)
12. Tozo za kuegesha magari
13. Makato ya Mikopo
14. Tozo za internet cafe ili uweze ku-surf
15. Rambirambi ya mfiwa mtaani kwetu
16. Harusi ya ndugu yako wa ukoo na zawadi
17. Sendoff ya mtoto ya mdogo wake rafiki yako na
18. zawadi Kumuaga mfanyakazi mwenzetu na
19. zawadi Michango ya komunio ya 1 & 2 na kipaimara
20. Michango ya besdei party na zawadi
21. Ndugu wa kule kijijini
22. Mshahara wa Hausigeli na na hausiboi
23. Bodaboda, teksi na bajaj
24. Duka la dawa
25. Tuisheni ya mtoto
26. Kuchangia wahanga wa mabomu na mafuriko.
27. Kwenda kumuona mtoto aliyezaliwa,
28. Kununua CD/DVD ya Uzinduzi wa Kwaya yetu
29. Chakula cha mbwa
30. Machango wa Ujenzi wa Kupanua Kanisa
31. Kuchangia Uinjilisti
32. Outing ya kitimoto
33. Ujenzi wa Nyumba Mwabepande
34. Kuendeleza shamba mkuranga (linalotaka kutaifishwa kwa kutoendelezwa)
35. Na kwa wale wenzetu wanaokwenda umbali wa Viti Virefu, moja moto moja baridi
36. Maji ya Traffik
37. Chai ya Nesi na Daktari,
38. Kahawa ya Hakimu, Karani na PP
39. Vishoka waunganisha maji na umeme
40. Kidogodogo cha mjumbe na mtendaji wa mtaa Hivi hali inakuwaje?
41. Mia mbili ya watoto wa mtaani/ombaomba,
42. kitu kidogo cha wale wanaolazimisha kuosha kioo cha gari kwenye foleni.
43. umeme uliopanda bei,
44. gesi iliyopanda bei,
45. maji yaliyoadimika,
46. bado contingency expenses maana huu usafiri unaotembelea ball joint,bush,fen belt havijafa...bado service,
47. Chakula cha mchana kazini especially kama maofisi yetu mama ntilie wanakaribiana bei na restaurants
48. Mchango wa kitchen pati na sare,baby shower...
49. bado hujatoa watoto outing jumapili n.k
50. Akiba ya uzeeni ambayo mtu anatakiwa aijenge wakati bado hajastaafu n.k

Hapo mwajiri amekuongezea mshahara kwa 7% tu wakati inflation ni above 19%.

Ukifikiria kwa makini unajiuliza Watanzania wanawezaje kuishi kwa style hii???
 
BUNDLE
SUBSCRIPTION
FEE
VALIDITY
Daily Bundle (20MB)
SMS ' datasiku ' to 15444
500/=​
1 day​
1 Day bundle (300MB)
SMS ' dataplus ' to 15444
3,000/=​
1 day​
 
Wana JF na watanzania wote kwa ujumla heri ya mwaka mpya.

Inasikitisha sana sana pale ambapo nchi ya maziwa na asali kama Tanzania watu wake wanaendelea kutaabika na umaskini.

Watanzania tulikuwa tunasubiri kwa matumaini makubwa upatikanaji wa nishati inayotokana na gesi. Upatikanaji wa gesi ungekuwa ni mbadala wa uharibifu wa mazingira ambapo ukataji miti ovyo ungepungua.

Masikitiko yangu ni kwamba wakati tukielekea kwenye upatikanaji wa nishati hii ya gesi, bei ya gesi imepanda badala ya kushuka ili kuwawezesha wananchi kujipatia nishati hiyo.

Mtungi wa gesi kwa kg 50 ni 63000 badala ya 54000 kama hapo awali.

Je, kwa hali hii, tunaenda wapi? Wewe mwananchi, acha ushabiki usio na tija. Fikiri kabla hujaamua.

Source: Mwananchi Newz Paper
Tatizo la viongozi wetu wa kisiasa,hawatendi yale wanayonena.

Imagine Rais wetu JK wakati anaingia madarakani mwaka 2005,aliahidi maisha bora kwa kila mtanzania, sasa badala yake siyo tena maisha bora kwa kila mtanzania,bali yamekuwa maisha ya majanga ya majanga kwa kila mTz, except kwa viongozi wakubwa ndani ya chama tawala na serikali ya CCM na wanafamilia wao.

Hebu jaribu kuimagine,siku zote viongozi wetu wanapokuwa kwenye majukwaa ya kisiasa,wamekuwa wakituhakikishia waTz kuwa baada ya kugundulika gesi nyingi sana nchini,inayokadiriwa kufikia cubic feet trillion 46,badala ya neema hiyo kuonekana kwa bidhaa zinazotumia gesi hiyo hiyo kama gesi ya kupikia na matumizi ya nishati ya umeme kupungua kama ambavyo wamekuwa wakituahidi kuwa zitapungua,badala yake imekuwa vice versa, bei zake ndiyo zimepaa kwa mtungi wa gesi kufikia eifu 63 na bei ya umeme kupanda kwa asilmia zaidi ya 40.

Hivi viongozi wetu hawa,sisi waTz tukiwaita kuwa ni wasanii wakubwa,watasema sisi waTz,tumewakosea adabu?!!
 
Kaka naomba nikusahihishe kidogo hapo kwenye KG ya huo mtungi ni kilo 30 tu na wala sio 50kg
 
Wananchi wa tanzania asilimia kubwa hawana akili timamu ndio maana huu ujinga unaendelea
 
Hata kidogo. Kwanza kabisa wao wenyewe hawajitambui, ni waongo na kwa hili yatawatokea puani.
 
Kaka naomba nikusahihishe kidogo hapo kwenye KG ya huo mtungi ni kilo 30 tu na wala sio 50kg

Bado sijaelewa hapa kitu gani mnazungumzia wekeni sawa! Mnazungumzia Mtungi Empty bila gesi au? Maana navyojua mimi mtungi wenye gesi wa kilo 30(gesi 15kg+mtungi 15kg) ni zaidi ya 150,000/= ukienda kubadilisha mtungi na kununua gesi ni 55,000/=
 
kilo 15 kujaza gesi pekee ilikuwa elfu 22 kwa sasa imepanda mpaka elfu 26 na hii ni kwa dar hatujuwi huko mikoani itakuwaje, kama kuna vitu vimenishangaza ni kupanda kwa bei ya gesi maana wengi tunatarajia ishuke zaidi na zaidi badala yake inapanda! hii nchi sijuwi tunaelekea wapi.
 
Hakuna sababu ya kulialia hapo,ujinga wetu wa kukubali kuhongwa pilau,tshirt,kofia na chumvi ndio unaotufikasha hapo! wanaotuhonga wanatudharau sana na kutuona wapumbafu na ndio maana wanafanya watakavyo! AMKA, JITAMBUE NA 2015 FANYA MAAMUZI SAHIHI TUWAPUMZISHE HAWA WAKOLONI WEUSI WALIOLEMEWA NA MIZIGO ILI TAIFA LITOKE HAPA LILIPOKWAMA!
 
Tanzania ni zaidi uijuavyo,wakati wenzetu wanaupokea mwaka mpya kwa matumain makubwa,cc walala hoi tunaupokea kwa gharama za maisha kupanda mara dufu,wanao washabikia manyan'gau nyinyiemu mungu na awalaan wao na uzao wao.
 
Tanzania ni zaidi ya uijuavyo,wakati wenzetu wanaupokea mwaka mpya kwa matumain makubwa,cc walala hoi tunaupokea kwa gharama za maisha kupanda mara dufu,wanao washabikia manyan'gau nyinyiemu mungu na awalaan wao na uzao wao.
 
Back
Top Bottom