Tafadhali wajuzi wa mambo haya mtufafanulie

Mrimi

JF-Expert Member
Jul 18, 2011
1,691
633
Kuna hoja nimeipost jukwaa la sheria lakini naona kijiwe kile ni kama hakina wateja wengi nimeamua kuiweka hapa sebuleni ili wenye ufahamu na mambo haya watusaidie.

Issue yenyewe wote tunaifahamu. Ni issue hii iliyowagawa watanzania ktk makundi mawili.

Kundi la kwanza linaona maandamano ambayo chadema imekuwa ikiyafanya kwamba ni haki yao kikatiba ili kuonesha hisia zao juu ya kile ambacho wanaamini hawatendewi haki yao kikatiba.

Kundi la pili linaona chadema kama chama kinachopenda fujo na kinachokaidi amri halali ya jeshi la polisi.

Jeshi la polisi linasema sharti chadema iombe kibali cha kufanya maandamano na kwamba, polisi wanaopt kutoa au kutokutoa hicho kibali kwa kuzingatia maswala ya kiusalama.

Kwa upande wa chadema wanasema kufanya maandamano ni haki yao kikatiba na kwamba maandamano hayaombewi kibali, isipokuwa wanatakiwa kutoa taarifa tu polisi. Na polisi wajibu wake ni kuhakikisha kwamba maandamano yanafanyika ktk hali ya amani na utulivu.

Kimsingi hiyo ndiyo hoja yangu. Sasa basi, Jukwaa la Katiba limetangaza kusudio lao la kufanya maandamano nchi nzima katika kupinga kile wanachosema kusomwa mara ya pili bungeni kwa muswada wakatiba mpya.

Kwa hiyo ningependa wajuzi wa mambo haya ya kisheria mtufafanulie ukweli kuhusu hili, kwamba ni nani yuko sahihi. Napenda sana tunapojadili tujadili hoja kwa uhalisia wake, endapo tutajadili kwa ushabiki wa siasa zetu, naamini tutabaki kuendelea kulumbana katika mawala ambayo kimsingi watalamu wetu walitakiwa kuwa wameishayatolea ufafanuzi.

Nawasilisha...
 
Back
Top Bottom