HIVI KWANINI WABUNGE WETU WANALALAMIKA JUU YA BAJETI BADALA YA KUTIMIZA WAJIBU WAO?! WANAMLALAMIKIA NANI?
Kimsingi bajeti inapopelekwa Bungeni na serikali inakwenda kwa ajili ya mjadala na marekebisho palipo na mapungufu NA SI KUPITISHWA KAMA WAJIBU TU, tunategemea mjadala wenye lengo la kuboresha bajeti iliyowasilishwa bungeni kwa faida ya wananchi.
Sasa haya malalamiko ya baadhi ya wabunge barabarani, mara "niko tayari kufukuzwa"!! Nani anamfukuza nani?! Nani anayetishia uhuru, haki na wajibu wa kikatiba wa wabunge wetu mpaka wanalalamika barabarani?!!
Nashauri wabunge timizeni wajibu wenu, jadilini na kuishauri serikali ndani ya bunge juu ya maboresho ya bajeti iliyoletwa kwenu! Kulalamika barabarani kunaonyesha ama baadhi hawajui wajibu na haki zao kikatiba, au kuna watu wanatafuta umaarufu binafsi. Hivi kila mmoja akilalamika na nyie tuliowapa dhamana ya kuisimamia na kuishauri serikali maana yake nini? Nyie mlalamike na wananchi walalamike kuna sababu gani ya nyie kupewa dhamana hii kubwa mliopewa!!
With due respect TIMIZENI WAJIBU WENU BUNGENI NA SI BARABARANI KULALAMIKA KUTWA KUCHWA!