Tafadhali Rais Mkapa endeleza Ukimya!

Mkapa anaweza kabia kutusaidia kuvuka hapa tulipo ili tusonge mbele. Ila ndio hivyo tena anatuona kama ni mbumbu fulani vile. What a mess!!
 
Mwanakijiji nadhani mtu wa kwanza kufungwa jiwe shingoni na kutupwa baharini atakuwa Mh. Petro Kayanza Pinda kwasababu alimtetea sana Mkapa pale mjengoni.
 
Mzee wa Kijiji, kama uko nje lini utarudi nyumbani uanzishe Chama tujiunge tuzunguke nchi nzima kukusanya wanachama na hatimaye ushike usukani wa nchi yetu? Kama uko hapa nyumbani jitokeze tukuunge mkono, Unastahili kabisa kuwa kiongozi wa nchi hii!

twaja.. vyapikwa viko jikoni.. mambo ni kama "COPA cabana"..
 
Mkapa ana tatizo moja kubwa: Kwake yeye "being humble is equal to humiliation". ndio maana tangu kujikuta kwenye hii aibu, either anashindwa kujibu tuhuma au akijaribu kujibu anatanguliza kiburi.

Mkapa ushauri wangu wa bure huu hapa: Simama mbele ya umma sema i am sorry for what i did to you my fellow Tanzanians. Naombeni msamaha, tasahau yaliyopita tugange yajayo....Mimi ni binadamu na wala sio malaika. Naahidi kutumia muda wangu uliobaki hapa duniani kutoa ushauri na kumsaidia Rais aliyepo madarakani kuongoza kwa busara ili asije kuingia kwenye mtego nilionaswa....

mzee hilo limemshinda Lowassa.. unadhani Mkapa ataweza? Niliwahi kuandika makala miaka ka' miwili iliyopita isemayo "viongozi wasiokosoea na taifa la wasiokasirika"! Hawawezi kuomba msamaha!
 
Mi naona President Mkapa anashambuliwa sana baada ya kutoka madarakani kwa sababu hakuwa na lugha laini maana wabongo tunapenda sana kubembelezwa.

Alishasema mazuri na mabaya yote anayapokea kwa hiyo anatambua kuna vitu vilienda vizuri na kuna vitu havikwenda sawasawa!

But jamaaa alijaribu kufanya kile alichoona anaweza na kuna kipindi mambo yalionekana, alidhibiti mfumuko wa bei na hata kauchumi kalianza kupaaa!

Hayo mambo ya ufisadi na uhalifu uliyoyataja kuna vyombo vinavyohusika ku deal nayo, issue viwajibike tuu kuutokomeza kabisa sasa huwezi kumlaumu yeye moja kwa moja
 
Ben ni kiburi, jeuri na too proud to bow down na kuomba msamaha, hivyo anadharau kelele zote zinazoelekezwa kwake kwa kisingizio kuwa ana 'just ignore them'. Kwa dharau zake, jeuri yeke, kiburi chake na pride yake, "Karma" itamshukia na kumwadhibu hapa hapa duniani siku yake ikifika.Huyu ni mwanahabari iliyegeuka kuwa mwanadiplomasia, katika kipindi chake chote cha miaka 10 ya utawala wake, hakuwahi kuzungumza na waandishi wa habari ana kwa ana kama ilivyoakifanya Nyerere, alipoulizwa kwa nini, alidai waandishi wetu are stupid!.Hakuwahi kufanya mahojiano yoyote ya man to man na redio au televisheni yoyote ya Tanzania, yeye ni CNN na BBC tuu. Nlibahatika kushuhudia mahojiano yake na Tim Sebastian, kwenye 'Hard Talk' kwa kweli alijidhalilisha jinsi alivyotaka kuleta ubabe ulioishia kwenye mahasira.Andiko la Shivji kuhusu Mkapa, limenigusa sana, na naamini pamoja na kiburi, na madharau yake, pia anaguswa moyoni na shutuma dhidi yake, na labda anatubu na kujuta kimoyo moyo ambapo Mungu amemsamehe, lakini sisi Watanzania bado hatujamsamee, ila akifuata ushauri wa Mwakijiji wa kunyamaza kimya kabisa, Watanzania tutatafsiri ni namna ya kuomba msamaha na tutamsamehe.
 
MMJ, heshima zako Mzee na nakuvulia kofia kwa article yako. Kila Jumatano miye hukimbilia kununua Mwanahalisi na Raia Mwema nikusome wewe la Lula wa Ndali. Hiyo statement ya Mkapa imejaa arrogance na dharau aliyokuwanayo huyu Mzee. Nadhani ni vya kuzaliwa pia! Nasikitika Mwalimu hakuliona hilo akabeba mbuzi kwenye gunia aliyekuja kumkana hata aliyembeba. Aibu!

Mzee wa Kijiji, kama uko nje lini utarudi nyumbani uanzishe Chama tujiunge tuzunguke nchi nzima kukusanya wanachama na hatimaye ushike usukani wa nchi yetu? Kama uko hapa nyumbani jitokeze tukuunge mkono, Unastahili kabisa kuwa kiongozi wa nchi hii!
Big NO.
Kwa nini? au kwa lipi?

Uongozi wa nchi si jambo dogo.MMK ni mzuri sana katika kuchambua masuala mbalimbali hasa yanayohusu mustakabali wa nchi yetu.MMK amefanya sehemu yake.MMK anastahili PONGEZI NA SHUKRANI,watanzania tuna deni kubwa kwa MMK,vilevile vizazi vijavyo vitamkumbuka kwa mchango wake mkubwa kwa taifa letu/lake kwa kutumia Kalamu yake,lakini HILI LA KUANZISHA CHAMA NA URAIS ,HAPANA.

MMK ni winga , ukimchezesha kama beki TUTAFUNGWA , mwache HAPOHAPO.
 
Ben ni kiburi, jeuri na too proud to bow down na kuomba msamaha, hivyo anadharau kelele zote zinazoelekezwa kwake kwa kisingizio kuwa ana 'just ignore them'. Kwa dharau zake, jeuri yeke, kiburi chake na pride yake, "Karma" itamshukia na kumwadhibu hapa hapa duniani siku yake ikifika.Huyu ni mwanahabari iliyegeuka kuwa mwanadiplomasia, katika kipindi chake chote cha miaka 10 ya utawala wake, hakuwahi kuzungumza na waandishi wa habari ana kwa ana kama ilivyoakifanya Nyerere, alipoulizwa kwa nini, alidai waandishi wetu are stupid!.Hakuwahi kufanya mahojiano yoyote ya man to man na redio au televisheni yoyote ya Tanzania, yeye ni CNN na BBC tuu. Nlibahatika kushuhudia mahojiano yake na Tim Sebastian, kwenye 'Hard Talk' kwa kweli alijidhalilisha jinsi alivyotaka kuleta ubabe ulioishia kwenye mahasira.Andiko la Shivji kuhusu Mkapa, limenigusa sana, na naamini pamoja na kiburi, na madharau yake, pia anaguswa moyoni na shutuma dhidi yake, na labda anatubu na kujuta kimoyo moyo ambapo Mungu amemsamehe, lakini sisi Watanzania bado hatujamsamee, ila akifuata ushauri wa Mwakijiji wa kunyamaza kimya kabisa, Watanzania tutatafsiri ni namna ya kuomba msamaha na tutamsamehe.
Mkulu
Umezungumza,heshima.
 
Simtetei Mkapa, wala siwezi kumtetea Mkapa kwa madudu yaliyofanyika katika kipindi chake!! Lakini ni vyema kusema kuwa Mkapa alikuwa shupavu, ni bahati mbaya tu kuwa alirithi nchi iliyokuwa imechoka isiyokusanya madeni, isiyokuwa na hadhi mbele ya mataifa mengine na iliyokuwa haina hata hifadhi ya fedha za kigeni. Alirithi nchi iliyokuwa imenajisiwa kwa uongozi mbayana kuchoka kabisa. Ilikuwa ni nchi ambayo haikusanyi kodi na iliyokuwa inashindwa kutawalika kiasi kwamba Baba wa taifa akalazimika kutoka kwenye kustaafu kwake na kurudi katika siasa za kuirudisha nchi katika mstari wa kutawalika!!! kwa kweli Mzee Mwinyi alikuwa ameshindwa kuitawala nchi hii ina kuigeuza kuwa kichwa cha Mwendawazimu, kiasi cha kufikirika kuwa mtu kama Augostine Mrema angeweza kutuongoza!!!

Watawala wa sasa wameturudisha alikoitoa nchi hii na mapungufu yao ya sasa tunayapeleka kwa Mzee Mkapa. Mbona Watanzania tu wepesi wa kusahau?????

Nawaambia tukidodosa aliyofanya Mzee Mwinyi wakati wa kipindi chake, tutagundua kuwa Mkapa alikuwa nafuu sana ila bahati mbaya watanzania tu wepesi wa kusahau.

Ikulu ya Mwinyi si kuwa kulianzishwa kampuni binafsi kama ANBEM bali kulikuwepo na biashara hata za dhahabu na watu walikuwa wanajua hata bei ya rais wetu!!!! Je wana JF nani anaweza kujitokeza na kusema anajua bei ya Mkapa???? hakika hakuna ila tumesahau nani alifuta Azimio la Arusha na kuanzisha Azimio la Zanzibar!! Jamani tusiwe wepesi wa kusahau wapi tulipo jikwaa na kuwa tunakumbuka tulipo angukia!!!

Kwa "mema" aliyoyafanya alikuwa akitimiza wajibu wake haswa kama Rais wa nchi yetu wala hatuna sababu ya kukumbuka wala kumshukuru!

Twaangalia 'mabaya' kwa sababu alitusaliti tuliompa kura zetu na zaidi alimsaliti Mwalimu Nyerere ambaye alimuamini mia kwa mia! Alichokifanya dhidi ya Mwalimu si kitendo cha kiungwana hata kidogo. Akataifisha NBC pamoja na Mwalimu kumsihi asifanye kosa hilo. Akawa na ufedhuli na kiburi. Kama kweli angelithamini kazi kubwa Mwalimu aliyomfanyika hata kuupata urais basi angalau angelijaribu kurudisha Azimio la Arusha kama zawadi kwa Mwalimu. Lakini alichokifanya ni danganya toto maana wakati anaingia madarakani, kwa kuwa Mwalimu alikuwa bado yu hai Mkapa akatangaza mali zake na kuahidi kwamba atapambana kikamilifu na rushwa. Wakati anatoka madarakani wala hakuthubutu kututangazia mali zake kwa kuwa alijua amekiuka misingi ya uongozi/utawala bora - amefanya biashara akiwa Ikulu na kujinufaisha kwa kutumia cheo chake. Ushupavu wake hautusaidii lolote hivi sasa maana nchi inasambaratika kutokana na makosa aliyoyafanya MAKUSUDI kwa kiburi na jeuri aliyokuwanayo!
 
Simtetei Mkapa, wala siwezi kumtetea Mkapa kwa madudu yaliyofanyika katika kipindi chake!! Lakini ni vyema kusema kuwa Mkapa alikuwa shupavu, ni bahati mbaya tu kuwa alirithi nchi iliyokuwa imechoka isiyokusanya madeni, isiyokuwa na hadhi mbele ya mataifa mengine na iliyokuwa haina hata hifadhi ya fedha za kigeni. Alirithi nchi iliyokuwa imenajisiwa kwa uongozi mbayana kuchoka kabisa. Ilikuwa ni nchi ambayo haikusanyi kodi na iliyokuwa inashindwa kutawalika kiasi kwamba Baba wa taifa akalazimika kutoka kwenye kustaafu kwake na kurudi katika siasa za kuirudisha nchi katika mstari wa kutawalika!!! kwa kweli Mzee Mwinyi alikuwa ameshindwa kuitawala nchi hii ina kuigeuza kuwa kichwa cha Mwendawazimu, kiasi cha kufikirika kuwa mtu kama Augostine Mrema angeweza kutuongoza!!!

Watawala wa sasa wameturudisha alikoitoa nchi hii na mapungufu yao ya sasa tunayapeleka kwa Mzee Mkapa. Mbona Watanzania tu wepesi wa kusahau?????

Nawaambia tukidodosa aliyofanya Mzee Mwinyi wakati wa kipindi chake, tutagundua kuwa Mkapa alikuwa nafuu sana ila bahati mbaya watanzania tu wepesi wa kusahau.

Ikulu ya Mwinyi si kuwa kulianzishwa kampuni binafsi kama ANBEM bali kulikuwepo na biashara hata za dhahabu na watu walikuwa wanajua hata bei ya rais wetu!!!! Je wana JF nani anaweza kujitokeza na kusema anajua bei ya Mkapa???? hakika hakuna ila tumesahau nani alifuta Azimio la Arusha na kuanzisha Azimio la Zanzibar!! Jamani tusiwe wepesi wa kusahau wapi tulipo jikwaa na kuwa tunakumbuka tulipo angukia!!!
Hayo ya ufisadi wakatu wa Mzee Ruhusa hayakuwa na impact za muda mrefu na alivyoondoka aliiacha nchi is still virgin, Lakini kaja Mkapa na mikataba ya kifisadi na muda mrefu kama madini ni mikataba ya miaka hamsini, IPTL miaka ishirini n.k. Na hata atakayekuja siyo rahisi kubadilisha hii mikataba
 
Mwinyi hakuacha nchi virgin mkuu, mbegu yake ndio imeanza kuvunwa sasa, umesahau ishu km loliondo na zinginezo???? Kumbuka biashara alizokuwa anafanya na waarabu, kumbuka mkewe alivyokuwa anafanya biashara mpaka za kutuletea bia mbovu!! Mkapa aliporithi urais, ni km aliendeleza na kuimarisha mauchafu yao... sasa baada ya kuwazidia sasa goma limeanza kutapika ktk enzi hizi za Muungwana!!
 
Mkapa ananyamaza, kimya maana anajua kunawatu wanaosema kwa niaba yake. Ila najua kuna siku tu hiyo kinga ikitoka, lazima tu atasema.
 
Ben ni kiburi, jeuri na too proud to bow down na kuomba msamaha, hivyo anadharau kelele zote zinazoelekezwa kwake kwa kisingizio kuwa ana 'just ignore them'. Kwa dharau zake, jeuri yeke, kiburi chake na pride yake, "Karma" itamshukia na kumwadhibu hapa hapa duniani siku yake ikifika.Huyu ni mwanahabari iliyegeuka kuwa mwanadiplomasia, katika kipindi chake chote cha miaka 10 ya utawala wake, hakuwahi kuzungumza na waandishi wa habari ana kwa ana kama ilivyoakifanya Nyerere, alipoulizwa kwa nini, alidai waandishi wetu are stupid!.Hakuwahi kufanya mahojiano yoyote ya man to man na redio au televisheni yoyote ya Tanzania, yeye ni CNN na BBC tuu. Nlibahatika kushuhudia mahojiano yake na Tim Sebastian, kwenye 'Hard Talk' kwa kweli alijidhalilisha jinsi alivyotaka kuleta ubabe ulioishia kwenye mahasira.Andiko la Shivji kuhusu Mkapa, limenigusa sana, na naamini pamoja na kiburi, na madharau yake, pia anaguswa moyoni na shutuma dhidi yake, na labda anatubu na kujuta kimoyo moyo ambapo Mungu amemsamehe, lakini sisi Watanzania bado hatujamsamee, ila akifuata ushauri wa Mwakijiji wa kunyamaza kimya kabisa, Watanzania tutatafsiri ni namna ya kuomba msamaha na tutamsamehe.
Kwa waafrika ni aibu baba hata kama ana makosa kiasi gani, kuacha nyumba yake isambaratike. Anatakiwa asimame na kutuoa mwelekeo maana ni kweli anajutia aliyoyafanya ingawa ni kwa sirisiri. Ingekuwa na msaada mkubwa kwake kama angeweza kupata fursa ya kutuchukulia watanzania kama ni watu tulio karibu naye kwa kutuface na kuondoa hili jambo linalogoma kutoka mbele yake. dawa ya tatizo sio kukaa kimya, ni kulikabili.
 
Mi naona President Mkapa anashambuliwa sana baada ya kutoka madarakani kwa sababu hakuwa na lugha laini maana wabongo tunapenda sana kubembelezwa.

Alishasema mazuri na mabaya yote anayapokea kwa hiyo anatambua kuna vitu vilienda vizuri na kuna vitu havikwenda sawasawa!

But jamaaa alijaribu kufanya kile alichoona anaweza na kuna kipindi mambo yalionekana, alidhibiti mfumuko wa bei na hata kauchumi kalianza kupaaa!

Hayo mambo ya ufisadi na uhalifu uliyoyataja kuna vyombo vinavyohusika ku deal nayo, issue viwajibike tuu kuutokomeza kabisa sasa huwezi kumlaumu yeye moja kwa moja
Ben anastahili kubeba mabaya yote yaliyotendeka katika kipindi chake !! hatuwezi kumtetea kwa hili, lakini mfumo na matatizo yaliyotokea wakati wa kipindi cha mzee ruksa ni lazima yabebwe na mzee mwinyi mwenyewe. Mimi naona tatizo kubwa linalomkabili Mkapa ni kushindwa kujitetea na kusema ukweli wote. Mwinyi na Azimio la Zanzibar ndilo lilikuwa tatizo kubwa maana ruksa ilitolewa kwa kila kitu. Mkapa alinyanyua nchi hii bwana.
 
Kati ya Mwinyi, Mkapa na huyu wa sasa nani anaonekana kuwa angalau kuna kitu amewafanyia WaTZ??
Hakuna lolote la kujivunia kwa Mwinyi!! hata mfumo wa vyama vingi hakuutaka maana serikali yake iliendesha kampeni kubwa kuupinga, Thanks to Mwl. Nyerere ambaye alitetea hata akalazimisha 15% ya Watanzania waliotaka mfumo huo wameshinda.

Mkapa alidhibiti mfumko wa bei, aliifanya serikali ionekane inafanya kazi, alikusanya kodi na hata kujenga sura ya Nchi kimataifa! Alijenga barabara nyingi, alijenga Uwanja wa Taifa nk

Huyu wa sasa mpaka sasa hajafanya chochote zaidi ya kuzunguka dunia kama Vasco dagama. Ngoja tumsubiri tuone
 
Mzee wa Kijiji, kama uko nje lini utarudi nyumbani uanzishe Chama tujiunge tuzunguke nchi nzima kukusanya wanachama na hatimaye ushike usukani wa nchi yetu? Kama uko hapa nyumbani jitokeze tukuunge mkono, Unastahili kabisa kuwa kiongozi wa nchi hii!
Kauli za kilevi mtaacha lini?
 
Kati ya Mwinyi, Mkapa na huyu wa sasa nani anaonekana kuwa angalau kuna kitu amewafanyia WaTZ??
Hakuna lolote la kujivunia kwa Mwinyi!! hata mfumo wa vyama vingi hakuutaka maana serikali yake iliendesha kampeni kubwa kuupinga, Thanks to Mwl. Nyerere ambaye alitetea hata akalazimisha 15% ya Watanzania waliotaka mfumo huo wameshinda.

Mkapa alidhibiti mfumko wa bei, aliifanya serikali ionekane inafanya kazi, alikusanya kodi na hata kujenga sura ya Nchi kimataifa! Alijenga barabara nyingi, alijenga Uwanja wa Taifa nk

Huyu wa sasa mpaka sasa hajafanya chochote zaidi ya kuzunguka dunia kama Vasco dagama. Ngoja tumsubiri tuone

Hili nalo neno!
 
"Let he who is without sin, cast the first stone" whatever "bad" the President Mkapa did during his administration is trumped by the policies that he engineered for the betterment of watanzania.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom