Tafadhali Kikwete tangaza hali ya Dharura kwa Jiji la Dar; TUONGOZE KWENYE DHARURA HII!

Usalama ulimeguka vipande vipande. kwa wale tuliokuwepo jana Dar tuwe wakweli hakuna mkubwa/kiongozi ambaye angeweza kufanya lolote au kuzunguka huku na kule. Hata ambulance na magari ya zima moto yote yalishindwa kumudu mtikisiko wa hali ya jana na kusimama mahali pamoja kwa masaa manne. kwa hiyo hata viongozi wasingeweza kwani na wao walizuia ama maofisini au majumbani kwani polisi wasingeweza kusimamia usalama wao ( usalama wa viongozi) na wa wananchi kwa pamoja.
 
kila tukio la maafa linakwenda na wadandiaji ili waweze kupata misaada ya chakula, magodoro na vitu vingine. Namba itazidi kuongezeka
 
Ama kweli watu wavivu sana! hali ya hatari watangaze vipi? Mwenye macho haambiwi tazama,! ukiangalia maeneo ambayo yameathirika sana ni maeneno ya mabondeni amnapo siku zote serikali ilikuwa ikiwapigia kelele watu hao wanaodhaniwa kuwa wamevamia waondoke! lakini ni wabishi na mara moja hukimbilia mahakamani kuweka court order kuwa wameruhusiwa kukaa mpaka shuri litakaposikilizwa, aidha, wakati mwengine huamua kuwatoa mbio tena huku wameshika mapanga watu wanaojaribu kwenda kuwato kwa nguvu! Mamlaka ya hali ya hewa walsihatangaza tokea mwenzi wa tisa "September" kuwa mvua za vuli mwaka huu zitakuwa kubwa sana hivo watu wahamae! hawasikii! halafu mumlaumu RAis hivi kweli jamani ??? hebu muacheni huyu mtoto wa watu kwanza ! mmezidi kumsakama ! MKOMENI KWANZA MTOTO WA MWANAUME NA MWANAMKE MWENZENU ! kutwa midomoni! yeye mnataka afanye nini? kama post nyingine hapo juu kulitokea mafuriko kilosa je mlifanya nini ??? mbona hatukusikia state of emergency kutangazwa? na juzi juzi meli ilizama ! acheni UVIVU ! twendeni tukajenge taifa! JK mnamuonea sana! mvua zikiwa kubwa kama hivi hata nchi ZILIZOENDELEA huwa kuna mabalaa kama haya! msidanganywe labda muwe mnaishi kwenye nchi ambazo hazijawahi kufikiwa na mvua kubwa kama hizi ! HIZI NI QUDRA ZA MWENYE EZ MUNGU! na tuungane kuwaombea weneztu na kisha tukae chini kutafuta jia mbadala ya nini cha kuwafanyia watu wa mabondeni! Mungu ibariki TAnzania na vizazi vyake.
 
Ya Kilosa hayakaribiani kabisa na haya tunayoyashuhudia; believe me.
Mh! Nakumbuka wewe ni mmoja wa waliofanyakazi nzuri sana kufuatia mafuriko yale. Unayalinganisha na haya kwa lipi? Vifo? Vingine ni vya watoto wanaozaliwa na kutupwa na mama zao kila siku hapa mjini. Vingine ni vya walevi wa kupindukia. Mungu amesaidia kidogo mvua hizi zinanyesha alfajiri, tayari kunakuwa kumekucha. Nimepita pale Kigogo asubuhi hii. Palikuwa shwari kidogo. Mtu akifa kwa mvua zilizonyesha baadae inalaumiwa serikali kweli?
 
Ni kweli MMM, JANA imeripotiwa watu zaidi ya mia sita(600) wapo shule ya mchikichini na wanaitaji misaada ya kibinadamu.
Kwa Dar kukishanekana dalili ya misaada au hata mlo mmoja tu wa bure wanakwenda waliomo na wasiokuwemo
 
Ameongeza Rais Kikwete: “Napenda pia kupitia kwako kutoa pole zangu nyingi kwa wote walioumia ama kupoteza mali zao katika mafuriko haya. Wajulishe kuwa moyo wangu uko nao wakati huu wa mazingira magumu. “Chini ya usimamizi wako, ningependa kuona uongozi wa Mkoa kwa kushirikiana na taasisi na vyombo vyenye ujuzi na uzoefu wa kupambana na majanga na dharura za namna hii, kuhakikisha kuwa tunaendelea kuokoa watu ambao badowamezingirwa na mafuriko, tunawapa matibabu wale walioumia katika mafurikohayo, na tunawahifadhi na kuwapa huduma za kibinadamu wote waliopoteza nyumba na makazi yao katika mafurikio hayo.”

IMETOLEWA NA:
KURUGENZI YA MAWASILIANO YA RAIS IKULU
DESEMBA 21, 2011
DAR ES SALAAM

Ikiwa hii paragraph haijeditiwa na aliyeiweka hapa, basi hii ndio picha halisi ya ikulu yetu. Utafikiri imeandikwa na kindergarten kid fulani hivi huko kijijini. How can they be serious ?

wewe ndiye umefika mwisho wa kufikiri badala ya kuangalia ujumbe na kama umefika kwetu barabara wakati huu wa maafa unaangalia, nukta, koma na parandesi kwenye taarifa hiyo. Je, ungepewa jukumu la kwenda kuokoa watu sehemu ambayo hamuelewani lugha na unatakiwa kujua au kuelewa mahitaji yao na namna ya kuwasaidia.......sijui ungerudi.
 
Usalama ulimeguka vipande vipande. kwa wale tuliokuwepo jana Dar tuwe wakweli hakuna mkubwa/kiongozi ambaye angeweza kufanya lolote au kuzunguka huku na kule. Hata ambulance na magari ya zima moto yote yalishindwa kumudu mtikisiko wa hali ya jana na kusimama mahali pamoja kwa masaa manne. kwa hiyo hata viongozi wasingeweza kwani na wao walizuia ama maofisini au majumbani kwani polisi wasingeweza kusimamia usalama wao ( usalama wa viongozi) na wa wananchi kwa pamoja.

Ndiyo maana inatakiwa vikosi vya uokoaji viwe na helikopta na mitumbwi inayoweza tumika ktk hali kama ya jana,kinyume serikali yako inanunua magari ya washawasha na ya kurushia wananchi mimabomu ya machozi wktk wanadai haki zao.
 
Kwa Dar kukishanekana dalili ya misaada au hata mlo mmoja tu wa bure wanakwenda waliomo na wasiokuwemo

umenena ndugu, kwenye msafara wa mamba na kenge wamo ndio hali halisi. hali ya wanaohitaji inaweza kukuzwa na wadandiaji wa maafa kwani misaada inapotoka wanapata pia ambao sio sehemu ya walioathirika
 
Ama kweli watu wavivu sana! hali ya hatari watangaze vipi? Mwenye macho haambiwi tazama,! ukiangalia maeneo ambayo yameathirika sana ni maeneno ya mabondeni amnapo siku zote serikali ilikuwa ikiwapigia kelele watu hao wanaodhaniwa kuwa wamevamia waondoke! lakini ni wabishi na mara moja hukimbilia mahakamani kuweka court order kuwa wameruhusiwa kukaa mpaka shuri litakaposikilizwa, aidha, wakati mwengine huamua kuwatoa mbio tena huku wameshika mapanga watu wanaojaribu kwenda kuwato kwa nguvu! Mamlaka ya hali ya hewa walsihatangaza tokea mwenzi wa tisa "September" kuwa mvua za vuli mwaka huu zitakuwa kubwa sana hivo watu wahamae! hawasikii! halafu mumlaumu RAis hivi kweli jamani ??? hebu muacheni huyu mtoto wa watu kwanza ! mmezidi kumsakama ! MKOMENI KWANZA MTOTO WA MWANAUME NA MWANAMKE MWENZENU ! kutwa midomoni! yeye mnataka afanye nini? kama post nyingine hapo juu kulitokea mafuriko kilosa je mlifanya nini ??? mbona hatukusikia state of emergency kutangazwa? na juzi juzi meli ilizama ! acheni UVIVU ! twendeni tukajenge taifa! JK mnamuonea sana! mvua zikiwa kubwa kama hivi hata nchi ZILIZOENDELEA huwa kuna mabalaa kama haya! msidanganywe labda muwe mnaishi kwenye nchi ambazo hazijawahi kufikiwa na mvua kubwa kama hizi ! HIZI NI QUDRA ZA MWENYE EZ MUNGU! na tuungane kuwaombea weneztu na kisha tukae chini kutafuta jia mbadala ya nini cha kuwafanyia watu wa mabondeni! Mungu ibariki TAnzania na vizazi vyake.
Wewe unaishi wapi na madaraja yaliyokatika watu watafikaje seheme za kazi kujenga nchi kama serikali yaako na mafisadi wako hamjengi madaraja ya dharura
 
Hivi watu kujenga mabondeni wameacha kuwa Watanzania au wamepoteza utu wao? Au katiba yetu inasema "Kila mtu aliyejenga mlimani na nyumba ya kisasa anastahili haki ya kutambuliwa na kuthaminiwa utu wake"? Au wale waliojenga nyumba za kiasasa na wanaishi mahali pakavu ndio wanaamini wao ni binadamu zaidi na wana haki zaidi ya kutetea uhai wao? grrrrrrrrrrrrrrrrrr
 
Huyo ndiyo JK rais wa matukio

Ni makosa kudhani Rais ataongelea kila kitu utakuwa hujui itifaki na mgawanyo wa madaraka na mamlaka. Mkoa una kiongozi na itifaki iko wazi mkuu wa nchi itamtumia salaam za pole mkuu wa mkoa na wananchi wake. Hii haina maana Rais kamaliza kazi kwa salaam mbona tumesikia vikao vilikuwa vinaendelea Ikulu jana nzima na leo.
 
Jambo likitokea Dar mnalikuza sana. Barabara zetu zinachinja wangapi kila wiki? Janga la asili kama hili halitatuliki mara moja kiasi hicho. After all, mvua hadi dakika hii tunayojibizana humu zinaendelea kunyesha.

Sorry,hold on WildCard!

Tunakubali ni janga la asili,hatuwezi kuzuia mvua kunyesha,Ishu ni je tunakabiliana vipi na tatizo hasa uokoaji,je taasisi tulizozipa kazi hii zinafanya nini? Kusaidia waathirika hilo ni jambo lingine ambalo pia mimi silipingi,ni jambo zuri, na ndilo tunatakiwa kufanya next.Mvua zinaendelea kunyesha,uokoaji unaridhisha? Mkuu,kama haikufanyika kilosa,sio sababu ya kutokufanyika dar.

Bado tunabaki pale pale huu utawala ni wa wababaishaji!
 
Hivi watu kujenga mabondeni wameacha kuwa Watanzania au wamepoteza utu wao? Au katiba yetu inasema "Kila mtu aliyejenga mlimani na nyumba ya kisasa anastahili haki ya kutambuliwa na kuthaminiwa utu wake"? Au wale waliojenga nyumba za kiasasa na wanaishi mahali pakavu ndio wanaamini wao ni binadamu zaidi na wana haki zaidi ya kutetea uhai wao? grrrrrrrrrrrrrrrrrr

ili uwe binadamu kamili ni pamoja na kutambua hatari inayoweza kukukabili kwa matendo yako kabla ya kuilaumu serikali pekee. kama huwezi kutambua kuwa kujenga mabondeni ni hatari kwa maisha yako na unakufa kwa kosa hili eti tu serikali haikukuzuia kujenga bondeni ni kasoro kubwa kwenye fikra pana ya ubinadamu. Ni heri kuilaumu serikali kwa kutokukupa kiwanja nje ya bonde lakini usiikomoe serikali kwa kwenda kujenga bondeni.
 
Wewe unaishi wapi na madaraja yaliyokatika watu watafikaje seheme za kazi kujenga nchi kama serikali yaako na mafisadi wako hamjengi madaraja ya dharura

Hata dunia ya kwanza marekani na japan pamoja uwezo wao wa kiuchumi tumeshuhudia wakizidiwa na vimbunga, sunami na matetemeko ya ardhi sembuse ndio iwe nchi ya dunia ya tatu Tanzania.
 
Ameongeza Rais Kikwete: "Napenda pia kupitia kwako kutoa pole zangu nyingi kwa wote walioumia ama kupoteza mali zao katika mafuriko haya. Wajulishe kuwa moyo wangu uko nao wakati huu wa mazingira magumu. "Chini ya usimamizi wako, ningependa kuona uongozi wa Mkoa kwa kushirikiana na taasisi na vyombo vyenye ujuzi na uzoefu wa kupambana na majanga na dharura za namna hii, kuhakikisha kuwa tunaendelea kuokoa watu ambao badowamezingirwa na mafuriko, tunawapa matibabu wale walioumia katika mafurikohayo, na tunawahifadhi na kuwapa huduma za kibinadamu wote waliopoteza nyumba na makazi yao katika mafurikio hayo."

IMETOLEWA NA:
KURUGENZI YA MAWASILIANO YA RAIS IKULU
DESEMBA 21, 2011
DAR ES SALAAM

Narudia kusema kuwa kama MMJ hajaedit hili tamko, then tuna safari ndefuuuu. Tunategemea Ikulu ina iwe na watu makini zaidi ya hii kindergarten stail. Hapo kwekundi ni ishara tosha ya ulegelege .
 
Sorry,hold on WildCard!

Tunakubali ni janga la asili,hatuwezi kuzuia mvua kunyesha,Ishu ni je tunakabiliana vipi na tatizo hasa uokoaji,je taasisi tulizozipa kazi hii zinafanya nini? Kusaidia waathirika hilo ni jambo lingine ambalo pia mimi silipingi,ni jambo zuri, na ndilo tunatakiwa kufanya next.Mvua zinaendelea kunyesha,uokoaji unaridhisha? Mkuu,kama haikufanyika kilosa,sio sababu ya kutokufanyika dar.

Bado tunabaki pale pale huu utawala ni wa wababaishaji!

Enzi za Mkapa tulishuhudia reli ziking'oka na madaraja yakikatika kwa mvua za El nino, watu morogoro walikosa makazi haijapata kutokea hadi leo basi hakuna utawala ambao hauwezi kuwa wa kibabaishaji
 
Back
Top Bottom