Tafadhali Kikwete tangaza hali ya Dharura kwa Jiji la Dar; TUONGOZE KWENYE DHARURA HII!

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,463
39,929
Baada ya kufanya mazungumzo na watu mbalimbali na hasa baada ya kuona kina na uzito wa tatizo la mafuriko na hasa kwa vile mvua bado zinatarajiwa kunyesha tena Alhamisi, Ijumaa na Jumamosi na kwa vile hali hii itakuwa tata zaidi kuna uwezekano mkubwa sana wa kuvunjika kwa amani na utulivu katika Jiji la Dar kuliko wakati mwingine wowote. Vitu vyote muhimu vya kusababisha uvunjivu viko tayari.

- Shida ya njaa
- Kutafuta nafasi ya kujinufaisha na matatizo ya wengine
- Kushindwa kwa vyombo vya usalama kufika maeneo mbalimbali kwa haraka
- kukosekana kwa uongozi madhubuti na makini.

Nilitarajia tangu jana - Rais angekuwa wa kwanza kulihutubia taifa na hususan watu wa Dar juu ya janga hili na mipango ya serikali kulishughulikia na kuhakikisha usalama na utulivu. Nilitarajia kuwa masaa baada ya 12 kupita na hali kuonekana Rais angeweza kuzungumza na kuonesha uongozi kwa taifa na wakazi wa Dar na mara moja kuinitiate Emergency Protocol chini ya Emergency POwers Act of 1986.

Bahati mbaya masaa 24 yanapita sasa na tunaelekea masaa 36. Umuhimu wa kutangaza Emergency Situation ni kuweza kulazimisha resources mbalimbali kuweza kuanza kutumika (public and private) kwa ajili ya kunusuru kwani baada ya muda tutaona kuwa tatizo linalofuatia ni vitendo vya uporaji, ubakaji na matumizi ya nguvu ili watu wasalimike (natarajia kuanza kuona mambo haya 48 hours baada ya kuanza kwa mafuriko). Najua mojawapo ya matatizo ambayo yatatokea ni kuweza kuharakisha huduma mbalimbali hususan za afya - kwani mazingira ya mlipuko wa homa ya matumbo (typhoid) na kipindupindu (cholera) na Ecoli yako tayari. Na kwa vile hakuna mahali pa kujisaidia kwenye maeneo mengi, hali hii itakuwa ni mbaya sana ikianza hasa kwa watoto.

Ninaamini, kama kuna wakati wowote ambapo Rais Kikwete anahitaji kuonesha uongozi na kuwa yuko ontop of things ni kwenye hili lakini hadi hivi sasa haijatolewa kauli ya Ikulu masaa zaidi ya 24 inanitazia. Tunaweza kuwa na issue ya George Bush na Michael Brown wa FEMA pale alipotembelea wahanga wa Katrina. Sitaki (binafsi najisemea) kusikia ati "Rais ametoa pongezi kwa juhudi za uokoaji" and all the regular B.S kama tulizosikia baada ya Mv. Bukoba na Mv. Spice. Tunataka tuwaone wamekunja mashati na hawalali kuhakakisha Watanzania hawadhuriki kwani tayari wameshawalet down kwenye suala la miundo mbinu ya maji machafu na ya mvua na pia kwenye kusimamia ujenzi sasa tunapovuna walichopanda wasikae pembeni.


Tafadhali Rais Kikwete tangaza hali ya dharura na onesha uongozi saa na wakati huu kwani yawezekana Urais wako utaamuliwa na mengi sana lakini hili laweza kuwa ndio "defining moment". Maana kama wanasema mvua kama hii haijawahi kunyesha kwa miaka zaidi ya 57 jijini Dar manake hata Nyerere hakuwahi kujaribiwa kama unavyojaribiwa wewe - will you rise up and be counted? I hope and pray that you WILL answer this CALL OF HISTORY.

Ukiongoza tutakuunga mkono! Tuambie tufanye nini tusaidie, tuambie tusifanye nini ili kufanya kazi iwe rahisi; tuambie kama watu wanaweza kujitolea kuja kusaidia na waje kufanya nini? WE NEED A LEADER!

mmm



HILI NDILO TAMKO LA IKULU:


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amemtumia salamu za rambirambi Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mheshimiwa Said Meck Sadiq kuomboleza vifo vya watu 13 ambao wamepoteza maisha katika mafuriko makubwa yaliyotokana na mvua ambazo zimekuwa zinanyesha tokea juzi, Jumanne, Desemba 20, 2011. Aidha, Rais Kikwete amempa pole Mkuu huyo wa Mkoa kutokana na uharibifu mkubwa wa nyumba, makazi na mali nyingine za wananchi uliosababishwa na mvua hizo ambazo pia zimesababisha uharibifu wa miundombinu. Rais Kikwete pia ameuelekeza uongozi wa Mkoa wa Dar es Salaam kwa kusaidiana na taasisi na vyombo vyenye uzoefu wa maafa kushirikiana katika kuendelea kuokoa maisha ya watu, kusaidia waliozingirwa na mafuriko na kuwahifadhi na kuwasaidia wale wote waliopoteza nyumba na makazi kutokana na mafuriko hayo.


Katika salamu zake, Rais Kikwete amemwambia Mheshimiwa Sadiq: "Nimepokea kwa masikitiko habari za vifo vya wenzetu 13 ilivyotokana na mafuriko yaliyosababishwa na mvua kubwa ambayo sote tumeishuhudia katika Mkoa wa Dar es Salaam tokea jana. Amesema: "Nakutumia wewe rambirambi zangu kutokana na vifo hivyo, na kupitia kwako kwa familia, ndugu na jamaa waliopoteza wapendwa wao katika balaa hili la mafuriko. Wajulishe kuwa msiba wao ni msiba wangu, naelewa machungu yao na niko nao katika hali ya sasa ya maombolezo. Mungu aziweke pema peponi roho za marehemu wote."
Ameongeza Rais Kikwete: "Napenda pia kupitia kwako kutoa pole zangu nyingi kwa wote walioumia ama kupoteza mali zao katika mafuriko haya. Wajulishe kuwa moyo wangu uko nao wakati huu wa mazingira magumu. "Chini ya usimamizi wako, ningependa kuona uongozi wa Mkoa kwa kushirikiana na taasisi na vyombo vyenye ujuzi na uzoefu wa kupambana na majanga na dharura za namna hii, kuhakikisha kuwa tunaendelea kuokoa watu ambao badowamezingirwa na mafuriko, tunawapa matibabu wale walioumia katika mafurikohayo, na tunawahifadhi na kuwapa huduma za kibinadamu wote waliopoteza nyumba na makazi yao katika mafurikio hayo."


IMETOLEWA NA:
KURUGENZI YA MAWASILIANO YA RAIS IKULU
DESEMBA 21, 2011
DAR ES SALAAM


My Take:
Sidhani kama Ikulu wameelewa hata kidogo uzito wa mafuriko haya na jinsi ambavyo ifikapo Jumamosi yatakuwa na madhara makubwa kwa watu, mali, na uchumi wa Dar-es-Salaam (kama siyo nchi). Hili si Tatizo la Mkoa kama taarifa ya Ikulu invyoonesha; ni tatizo linalohitaji uongozi wa kitaifa. Kwani vifo vitakuwa vingi kuliko watu wanavyofikiria. Tusije kusikia tu "tulidhania"...
 
Jiulize wabunge na mameya wa Dar wako wapi?

Ths country is just fxxx up

Airport dar nayo imefurika maji

hawa wengine wote haijalishi; people need to look at their President. Kama kazi anaona ngumu au anaona ni tatizo la "watu wa mabondeni" basi akae kimya tu wananchi wamesurvive without his leadership and I bet they will survive anyway.
 
hawa wengine wote haijalishi; people need to look at their President. Kama kazi anaona ngumu au anaona ni tatizo la "watu wa mabondeni" basi akae kimya tu wananchi wamesurvive without his leadership and I bet they will survive anyway.
which President are you talking about?
 
Sasa hii imametoea dar . Tujiulize
ni matukio mangapi ya aina hiyo yametoea kigoma, kagera morogoro, dodoma .bila kupta attention sahihi. Kama dar inakuwa hivi vipi ikitigi singida si watu wanaweza kufa kwa kiu ya maji wakati wa kiangazi.

Tujiulize maswali magumu beyond dar na beyond mafuriko ya maji. Mimi naona Hii inaoyesha kuna watu itigi singida wanaweza kufa sabau ya kiu ya maji wakati wa kiangazi.

Na ile tume ya maafa si kazi yake huwa inaaza baada ya maafa kutokea........

Hodi Hodi Kipindu pindu dar. kwaheri mgao wa umeme mtera lol
 
hawa wengine wote haijalishi; people need to look at their President. Kama kazi anaona ngumu au anaona ni tatizo la "watu wa mabondeni" basi akae kimya tu wananchi wamesurvive without his leadership and I bet they will survive anyway.

Yes,we survived once. We can do it all over again with or without him
 
Akli na Ufahamu wa viongozi wetu .... vilishachuliwa na mafuriko siku nyingi zilizopita ... Its just externally reflecting what is inside ... No wonder!!

Lakini kweli hata sisi wanachi ... hatuna cha kujilaumu hapa? ... I mean We don't have a shame to share!!
 
Akli na Ufahamu wa viongozi wetu .... vilishachuliwa na mafuriko siku nyingi zilizopita ... Its just externally reflecting what is inside ... No wonder!!

Lakini kweli hata sisi wanachi ... hatuna cha kujilaumu hapa? ... I mean We don't have a shame to share!!
Somebody!!! diwanis, religious leaders, community activists...... mobilize people, tools, troops or whatever.
The aftermath will be disastrous too... people are peeing in those waters!!
 
hivi BARAZA LA USALAMA LA TAIFA liko wapi?

ripoti ya Mbagala na Gongo la mboto ziko wapi?

kwa nini thread ya BARAZA LA USALAMA ilihamishwa ?

JF inamlinda nani?
 
nchi nyingine vyombo vyote vya habari vingekuwa vinaongelea maafa haya oa kutoa updates,hii ingehamasisha uokoaji,wale wanaokaa mabondeni kuchukua taahadhari nk. Ajabu vyombo vyetu vya habari wanapiga muziki ni aibu.uzalendo utatoka wapi kwa mtanzania wa kawaida?
 
nchi nyingine vyombo vyote vya habari vingekuwa vinaongelea maafa haya oa kutoa updates,hii ingehamasisha uokoaji,wale wanaokaa mabondeni kuchukua taahadhari nk. Ajabu vyombo vyetu vya habari wanapiga muziki ni aibu.uzalendo utatoka wapi kwa mtanzania wa kawaida?

At least Channel 5 na 10 wamejaribu pamoja na matatizo ya matangazo na kuchelewa kuanza kuyarusha.
 
nchi nyingine vyombo vyote vya habari vingekuwa vinaongelea maafa haya oa kutoa updates,hii ingehamasisha uokoaji,wale wanaokaa mabondeni kuchukua taahadhari nk. Ajabu vyombo vyetu vya habari wanapiga muziki ni aibu.uzalendo utatoka wapi kwa mtanzania wa kawaida?

Yeah, mie nimefungua Clouds nasikia wameisifia kwa kutoa habari nasikia R&B za 1990s wakati watu wako katika mafuriko.
 
kwanza Baba mwenye nyumba mwenyewe yupo? Isije ikawa tunamuuliza kumbe yupo nyumba ya jirani.
 
Mwenzenu huwa najiuliza mara nyingi - hivi walipokuwa wanataka kuwa viongozi walikuwa wanafikiria wanatakiwa kuongoza nini magari? au kwa wingi wa saluti wanazopigiwa?
 
30 Reactions
Reply
Back
Top Bottom