Tabora School: Kichwa cha Tanzania

Mabata madogodogo yanaogelea yanaogelea katika shamba zuri la bustani!Yanapenda kulia kwa kwa kwa kwa kwa!
 
Asa,we uliesoma tabora boys na mie niliesoma minaki tuna tofauti gani?
 
Kaka tofauti ipo kwani Minaki na TBSS ni sawa? Namkumbuka my boy (masele) pia Issa alipozima mapinduzi ya kumkataa hgl.
 
Ngumi tunaamuka saa saba usiku enzi za mbabe Tyson na premier league kwa mrema ilikua raha sana.
 
Tulipofika pale form V PCM 1995_tulikuwa na mwalim mmoja tu wa chemistry, alikuwa anasema hata iweje hatuwez kufaulu_na only askari anaitwa CHACHA alikuwa anatutia moyo kuwa hiyo ni shule ya viongozi na kwamba lazima tutakuwa viongozi, NAMSHUKURU M/MUNGU kuwa pamoja na hali/mazingira nayotoka, kweli leo mimi ni kiongozi, pia namshukuru M/mungu kwa riziki anayonipatia na familia yangu
 
Ngumi tunaamuka saa saba usiku enzi za mbabe Tyson na premier league kwa mrema ilikua raha sana.

Msimsahau mzee Magesa(mwalimu Magesa), Afende Majamboz-Usikimwagie kitumbua changu mchanga. Zoezi funga fungua, one two nani kakwambia wamesoma hao waambie waseme 'moja mbili, moja mbili.....) utaipenda Boz weee.
 
Kama kuna kitu siwezi kusahau ni ile siku tuliyovamiwa na milambo,kusema kweli siku ile ningeweza kupoteza maisha.Thanks god sikupa hata jeraha.Nasikia Mrisho kapelekwa wizarani,Nkumba,Masele wameukwaa uhead master katika shule zingine.Pamoja na kwamba ile ni special school,lakini ina upungufu mkubwa sana wa walimu ingawa vijana wanajitahidi sana kuibeba.

Siku ya uvamizi wa Milambo ilikuwa noma na ile mvua ilivyokuwa ikipiga nakwambia watu tulijifungia kwenye chamber zetu na kuzima umeme. Kuna baa pale nje kuelekea boma paliitwa kwa Sonda mara nyingi tulienda kuangalia taarifa ya habari na tamthilia kwenye TV. Vp mwl. Magese na Mwombeki bado wapo?
 
aah mwalimu madafu alikuwa anachapa sana viboko kudadeki.........hadi mitako imeota sugu,bt anyway iz cool,yule mzee maduka na mke wake pale wakitulangua sana maji ya kunywa,glass sh 10 kama sikosei,vp mnakumbuka pale nyuma ya mzee maduka??kulikuwa na duka lingine tullikuwa tunaenda kula mtindi baada ya kupiga makande yaliyopikwa kwa mawese??kulikuwa na dem mmoja pale akiuza mtindi,madent kibao wakimfukuzia yule binti,vp zile trip za kipalapala kucheza mpira.mwl masele naeeee,akikukuta town hujavaa uniform utakiona siku ya paredi..dahh shida tupu tabora boyz,pale student centre yule mzungu padre bado yupo,nimemsahau jina???? he iz the best pastor of all timez,kuna mllinzi mmoja pale akituuzia viazi vitamu vya kupika ikiingia usiku saa 1 baada ya dinner mnakumbuka,unakumbuka pale chini ya mwemmbe karibu na messi ya chakula?madem wa wosso kibao wakati boyz mnakula lunch,mkimaliza mnakaa chini ya mwembe hadi saa 12 jioni,vile vyoo vipi wazee??ukiingia lazima uache nguo nje...manake hiyo harufu,,,mi sisemi........tabora ...good tread

Dah braza umenikumbusha mambo matamu matamu aisee lile duka nyuma ya duka la mwl maduka palikuwa panaitwa WHY NOT KIOSK,nimekunywa maziwa sana pale 2000-2006,Yule mzungu padre alikuwa anaitwa Father William Crombie tumekula sana zawadi zake za mashindano ya KURAP pale student centre,aiseeh Tabora School na mkoa wa TABORA kwa ujumla vimenijenga kibishi,kielimu na kunifunza jinsi ya kuishi na watu wa jamii tofautitofauti. Tujivunie Shule yetu na tufikirie jinsi ya kupita mara mojamoja kuisaidia shule yetu na shule nyingine za kata vijijini kwetu zitoe products nzuri kwa ujenzi wa taifa letu.
 
Asa,we uliesoma tabora boys na mie niliesoma minaki tuna tofauti gani?
Idadi ya walimu na quality ya walimu inaweza kuwa sawa lakini kuna tofauti nyingi sana,kama ubora wa wanafunzi, jitihada ya kujifunza, umoja wa wanafunzi, Historia ya shule na location ya shule n.k TABORA SCHOOL IPO JUU SANA KULIKO MINAKI.
 
Idadi ya walimu na quality ya walimu inaweza kuwa sawa lakini kuna tofauti nyingi sana,(kama ubora wa wanafunzi), UBORA WA WNAFUNZI WA TABORA BOYS NI MKUBWA SANA MFANO TABORA BOYS PCM MWISHO AAB, WAKATI MINAKI PCM WANACHUKUA MPAKA WALIOPATA CCD NI DHAHIRI KWAMBA TABORABOYS NI KICHWAA CHA TZ
 
Jamani ile shule kila siku inazidi kuporomoka kielimu...angalia mwaka 1990 hadi 2000 duu elimu ilihuka sana sana hadi ikabadilishwa na kuwa ya kawaida....hakuna walimu kabisa vijana wanajitahidi kufufuka na kukariri past papers na kukomaa na vitabu.....ila hakuna walimu tabora kukame sana walimu wa UD wakipangwa huwa awaendi kabisa.....ime lostisha sanakizazi hicho unakuta kijana amekuja mkali toka wilayani huko.....akitoka na 4....high school balaa kabisa....wamepiga sana zero na four....vijana future zao zimeharibiwa sana TBSS....wengi wakaingia jeshini kuziba gape....sasa wako kama 200 ma captain waliopita miaka 90 hadi 2000.nawakilisha....

Punguza dhihaka,TBSS haijawahi kuondolewa kwenye group la Vipaji Maalum hiyo miaka unayoisema na wala hijawahi kuondolewa kwa miaka ya 2000-2012, Me nimepita pale miaka sita kila mwaka O-LEVEL na A-LEVEL lazima waingie Top Ten kwenye Physics,Chemistry,Biology,Basic Math na Additional MAth,Advanced Math me ni mmojawao O-LEVEL 2003,A-LEVEL 2006,Wewe au ndugu yako kama alikuja kutoka spoon feeding school lazima apige four au zero na huwa awazidi 2.Kama unabisha pitia website ya Necta 2004-2012 utaiona position ya Tabora Boys Secondary School.kama unazungumzia Tabora Girls sawa,lakini na wenyewe hawafikia kuondolewa kwenye kundi la special school
 
Kama kuna kitu siwezi kusahau ni ile siku tuliyovamiwa na milambo,kusema kweli siku ile ningeweza kupoteza maisha.Thanks god sikupa hata jeraha.Nasikia Mrisho kapelekwa wizarani,Nkumba,Masele wameukwaa uhead master katika shule zingine.Pamoja na kwamba ile ni special school,lakini ina upungufu mkubwa sana wa walimu ingawa vijana wanajitahidi sana kuibeba.

Umeandika uongo mwingi!

Mrisho na Masela wote walistaafu wakiwa walimu pale Tabora Boys.

Tena Masele baada ya kustaafu alikua anashinda Ng'ambo kwenye vijiwe vya kahawa na wazee wenzake.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom