tabora na kigoma

Emecka

Member
Jul 17, 2012
75
27
habari za asubuhi mabibi na mabwana katika jamvi hili.
jaman naombeni ushauri. nimepata kazi katika miji tajwa hapo juu. tabora na kigoma. mimi binafsi sijawahi kuishi wala kupita katika mji wa kigoma. isipokuwa tabora nilishawahi kupita tu tena nikiwa kwenye basi/ treni. je kati ya tabora na kigoma wapi ni pazuri?
 
Tabora ni mji mkubwa kuliko Kigoma, kuna miundo mbinu mizuri hasa mjini. Kigoma ni kimji kidogo hakina miundo mbinu mizuri. Tabora hakuna biashara kama Kigoma, hakuna mzunguko mkubwa pesa. Kama unataka kufanya kazi na kufanya biashara kigoma ni sehemu nzuri lakini kama unataka kufanya kazi tu na kula mshahara wako TBR ni best choice.
 
Nenda Tabora,kwani ni karibu na mikoa ya jirani.Namaanisha ukitaka kwenda Shinyanga, Mwanza au singida.Hata Dar ni safari ya siku moja.Kigoma tatizo umbali,ukiingia umeingia.Ukiwa na safari ya Dar ni siku mbili.Mwanza siku nzima.Kama ndio unasafiri kwa basi ndio utaipata fresh,tope kipindi cha mvua,na hupelekea kulala njiani kama sio kuchelewa kufika safari yako.Kiangazi ni vumbi kwa kwenda balaa.Vilevile kutekwa njiani na majambazi ni kitu cha kawaida.

Sent from my BlackBerry 9780 using JamiiForums
 
Mimi niko kigoma kwauliyosema hapa n kweli kbs
 
Watu wa kgm wakifika Tbr wanaona kiwanja, tafakali mwenyewe hapo. Watu wengi wa kgm wanakimbilia Tbr lkn wa Tbr hawakimbilii Kgm. Hapo pia tafakali.
 
Ninajua sehemu zote, kazi gani uliyopata? Nitakushauri vizuri nikijua. Kote kuna advantages na disadvantages
 
Baadhi ya Vivutio vya Kigoma: Lake Tanganyika Hotel

attachment.php

Lake Tanganyika Hotel kwa mbali
attachment.php

Swimming pool Lake Tanganyika Hotel

attachment.php

Lake Tanganyika Hotel.
 
mchagua jembe si mkulima! Nimekaa KGM nimekaa TBR; Nimepita JKT, nimeweza kuishi kote kote; nenda tu utayaona mwenyewe!
 
Mkuu mikoa yote hiyo miwili hovyo tu, we andaa akili yako kabisa kuwa unaenda mwisho wa dunia, huko hakuna afadhali maendeleo bado ni duni.
Ushauri wote utaopewa hapa ni kama tu unapewa moyo. Ni kama tu mtu akuulize moto wa gesi na moto wa mkaa upi utaniunguza sana...bhanaa eeh mioto yote itakuacha hali si hali..
 
Back
Top Bottom