Tabora iliyodidimia inahitaji kuinuliwa...

Once a convict

rage270308.JPG


Always a law breaker

07ragekam.jpg

tatizo wanyamwezi uswahili umezidi,kwa vile wanacheza naye draft huku akiwanunulia kahawa baasi akili zinawaruka na kumpa kura.
 
Tabora ni ngome ya CCM. Hata mfanyeje haitahamia CDM. Mmeona Igunga. Mtapoteza nguvu nyingi na pesa ambazo mngetumia kwingine. Ngome zingine za CCM ni Lindi, Mtwara, Unguja na Pwani.

Msipende kujua ni kwa nini iko hivyo. Inatokana na nchanganyiko wa vitu vingi na haviko systematic. Hata Marekani kuna Red States na Blue States.

CDM iwekeze zaidi kwenye maeneo yasiyo ngome za CCM. eg Mwanza, Shinyanga, Musoma, Mbeya, Arusha etc

Sidhani kama Tabora ni ngome ya CCM. Kuwa na 100% ya wabunge wa CCM hakuuanyi mkoa kuwa ngome ya chama hicho. Tungekuwa na chaguzi huru na haki maneno yako yangekuwa na ukweli. Wananchi wa Tabora wanatawaliwa na kitu kikuu kimoja. Ni wepesi wa kukata tamaa. Akipatikana mtu wa kuwatia moyo basi CCM haina chake pale.
 
Dah...maendeleo Tabora???? Unyuma wa Tabora kimaendeleo hautokani na mambo ya vyama, ni watu wenyewe, ni asili yao, tuseme hivi, kuwa nyuma ya kila jambo muhimu kwa ustawi wa jamii ni sehemu muhimu sana ya wana Tabora, utake usitake huo ndiyo ukweli.
Mwaka 2010 Shinyanga ilikuwa nyuma sana ukiringanisha na Tabora, lakini sasa hivi Shinyanga inabadilika kila mwezi, na ndani ya mwezi au miezi kadhaa lazima project ikamilike au uone improvements, iwe NGO's, individuals au public.
Lakini ukiingalia Tabora, pamoja na kurundikiwa vyuo na ofisi tofauti kuweka zonal offices pale, bado ina drop kila uchao.
 
Kwani Chadema wanajenga barabara?

Mbona hawajajenga Arusha town mpaka leo hakuna hata barabara moja japo ya nusu kilometa ya Lami? wao ni mabingwa wa malumbano tu
Kwani CCM imejenga barabara ngapi? Ukumbuke Serikali iliyopo madarakani ni ya watu wote wenye vyama na wasiokuwa na vyama. Kwa hiyo serikali inawajibu wa kujenga barabara nakuwahakishia wananchi uwepo wa huduma mbalimbali. Hivyo, ni kweli kwamba Chadema hawajajenga barabara kwa sababu hawajapewa fursa ya kufanya hivyo, lakini wananchi wajaribu kuwapa waone kama wataweza au la. Ninawaakikishia wananchi wakiwapatia Chadema uongozi wataweza sana.
 
tatizo wanyamwezi uswahili umezidi,kwa vile wanacheza naye draft huku akiwanunulia kahawa baasi akili zinawaruka na kumpa kura.

Hilo NI tatizo la Athari ZA waarabu, uswahiili tu uvivu majungu niyo kazi
 
Jamani barabara za mkoa wetu wa Tabora zinatisha. Mpaka sasa hakuna barabara hata moja yenye rami ambayo inaingia mkoa wa Tabora. Chama changu cha Chadema mko wapi? Waamsheni wananchi wa Tabora kwani ni waelewa. Siku zote wanyamwezi na wasukuma ukiwaelimisha wakaelewa watakuunga mkono. Chadema nendeni Tabora kwani waanzilishi wa vyama hakina Fundikira, Mapalala na Kasela Bantu wote walikuwa ni wenyeji wa Tabora.
Wana JF muwe huru kuchangia kwenye thread ili mkoa wa Tabora uweze kuinuliwa. Kwasababu wanasiasa wenye maamuzi nao wanatembelea mtandao wetu wa JF. Nahisi kuna kitu kitafanyika.

Nyie si ndo mmejifanya kuikumbatia ccm kwa kuwachagua ktk nyadhifa mbalimbali kama ubunge, diwani na hata rair, sasa hiyo vijana wa mjini wanasema imekula kwenu, 2015 nadhani hamtarudia makosa ya kujizalilisha
 
Mheshimiwa mbunge wa Simba na Rufita Club Aden Rage, kwa kuwa umeshindwa kulitetea jimbo lako sisi Chadema tunakuja hatukubali wananchi waendelee kutaabika na usafiri kisa eti barabara mbovu.
 
Kumbuka hata mbuyu ulianza kama mchicha tuuuuu

Tabora ni ngome ya CCM. Hata mfanyeje haitahamia CDM. Mmeona Igunga. Mtapoteza nguvu nyingi na pesa ambazo mngetumia kwingine. Ngome zingine za CCM ni Lindi, Mtwara, Unguja na Pwani.

Msipende kujua ni kwa nini iko hivyo. Inatokana na nchanganyiko wa vitu vingi na haviko systematic. Hata Marekani kuna Red States na Blue States.

CDM iwekeze zaidi kwenye maeneo yasiyo ngome za CCM. eg Mwanza, Shinyanga, Musoma, Mbeya, Arusha etc
 
Na ndio maana mimi Pangu Pakavu najiandaa kuwakomboa wana Tabora kupitia chama mbadala, CDM.

Ni majuzi tu nilitoa salam kwa Mh Rage, mbunge wa Simba Sports Club, nikasema akae chonjo kwa kuwa umaskini na udhaifu wa Tabora hauvumiliki kamwe. Tabora haikupaswa kuwa hivyo ila ni dhahiri kwamba ama wanatabora hawakupewa elimu sahihi ya mageuzi ama elimu hiyo imechelewa kuwafikia.

Hakuna miujiza katika maendeleo, ni lazima kelele na juhudi zifanywe ili kuleta maendeleo hayo, ukisoma taarifa ya mkoa huu ya miaka 50 ya uhuru unaweza kulia bure, ofisi ya mkuu wa mkoa inaishia kusema eti kumekuwa na maendeleo ya kilimo hususan tumbaku na kwamba eti uvunaji wa asali umekua. Hivi tokea mwaka 1963 hiyo tumbaku na asali zimewafaidisha vipi wakulima wa Tabora, Mh Nkumba ataniunga mkono katika hili. Hiyo asalu ni ipi kama pale senta ya Nyuki kule airport imeishia kuchukuliwa na Mbola Project ile ya vijiji vya millenia, sembuse barabara???

Mabadiliko tutayahubiri na tutawaelimisha wanyamwezi na wasukuma ili twende sambamba, wakati wa ujinga umepita.

Ni mimi
Pangu Pakavu.
.

Mkuu kinachoniacha hoi kwa wana Tabora ni kuhusu hii centre. Centre hii iliyokuwa ikijulikana kama Beekeeping Training Institute -Tabora Kilikuwa ni chuo pekee na maarufu kwa ufugaji wa nyuki kusini na mashariki ya Afrika. Cha kushangaza wanasiasa wakaamua kukiondoa Tabora na kukipeleka Olmotonyi Arusha kwa sababu wanazojua wao huku wana Tabora wanachekelea tu huku mkoa ukikosa chachu za uchumi na maendeleo.

Sababu zilizofanya chuo kuhamishiwa Tabora zilikuwa ni uwepo wa uzalishaji mkubwa wa asali hasa ukifuata historia ya Tabora kama kuanzishwa kwa "Tabora Beekeepers Co-operative Society" (TBCS) in 1962, with 100 beekeepers. TBCS, Kipalapala, in 1991,ilizalisha 86.4 tonnes of "organic" honey which exported to UK and Netherlands. However, in 1995, only 10.6 kg honey was collected: "How to teach beekeeping in Africa"; "How can we solve the prob-lem of low productivity of East African Beekeeping. Utaona kuwa uzalishaji wa asali ulishuka baada ya chuo kuondolewa Tabora.


Beekeeping Training Institute – Tabora (BTI): The Beekeeping Training Institute started in 1969 for certificate course and 1970 diploma course in Olmotonyi. In 1978 the both the certificate and Diploma courses in Beekeeping was shifted to Tabora Beekeeping Institute until 1994. In 1995 the courses was transferred back to Olmotonyi. In 2006 the beekeeping courses was combined with forestry courses. This system lasted in 2008 when the two courses were separated again. Tabora Beekeeping Institute is to start again by offering Beekeeping course in 2010/2011.

Ukiangalia jinsi ambavyo mkoa unarudi nyuma ni dhihiri kuwa sera za kuondoa chuo kukirudisha Arusha kimeua ukusanyaji wa Asali Tabora, kwani unafanywa na watu bila kuwa na ujuzi na matokeo yake wanaua nyuki ili kuchukua asali which means msimu ujao. mambo haya yote yanatakiwa wanatabora wafahamishwe, maana kuanza kudai haki zao.

Hivi unapochagua mbunge kama Rage, anapata wapi muda wa kufuatilia haya yote zaidi ya kuwawekea wanaTabora kale ka redio ka Voice of Tabora tu?
 
Huo ni Mkoa uliosahauliwa toka awamu ya kwanza, kwa mara ya kwanza tunaona Kikwete akiwekeza kwa mabarabara huko. Baada ya dhiki faraja. Huyo ndio JMK.
Kuna wakati huwa najiuliza hivi great thinkers ni nani? Nilidhani ile post yako ya ongoing projects ingeufunga huu uzi lakini wapi! Watu wamefumba macho na kujielekeza kwa Rage wakati uzi ni kuhusu barabara na unewapa majawabu. JF kuna mabingwa wa ubishi na wala siyo thinkers! Mkoa mmoja una miradi toka Manyoni hadi mpakani mwa kigoma zaidi ya km 250! Kuna ujenzi wa barabara toka Tabora mjini kwenda Nzega zaidi ya km 100 ili kuunganisha barabara ya Dsm-moro-dodoma-singida-shinyanga-mwanza! Bado tunasema hakuna kinachofanyika huko Tabora?
 
Sehemu yoyote
ukishaona wanamcha
gua
mwarabu, muhindi,
msomali, jua eneo hilo
kuna wa2 wabovu
mnachagua all shaabab
na bado mtachagua
hadi wachina!!!.
 
Eehh Mungu uliyeumba mbingu na nchi, ukaumba wanadamu, ukaumba vitu pia vinavyoonekana na visivyoonekana, tupe moyo wa subira katika kutambua uwepo wa Wazalendo wanaokesha kufikiri ni vipi wanaikomboa Tabora. Wape moyo mkuu akina Pangu Pakavu ili waje na mipango yao kama wanavyoahidi humu kwamba wako dedicated kuwaokoa Wanyamwezi. Na zaidi mungu, wape ujasiri katika kuuangusha umaamuma wa fikra za uchawi, umwinyi na majungu ambayo waumini wako wa Tabora wanasimangwa kuwa nao.

Elimu ile ya uraia ambayo Chadema inaiendeleza mwanzo mwisho nayo mungu itupie jicho lako la rehema kwamba iufunike mkoa huu ili ile kwelu yako, amani na ilimu yako ihubiriwe kwa wote bila kujalu rangi, kabila wala itikadi za Wanatabora.

Mwishowe wewe mungu, tupe kufahamu kwamba maendeleo ya watu wa Tabora yako mikononi mwao lakini pia ukiwakinga na janga la mbunge wa Simba Sports Club ambayo enzi zile za Milambo Sports Club, naam enzi zile za akina Mikidadi Jumanne a.k.a 'bubu' ilikuwapo na hapakuwa na mbunge wa Simba, kwa kuwa hata simba ilishika adabu. Tupe wewe kuwakumbuka akina Mayayi wale kurwa na doto wa pale Mihayo Secondary School walivyoparangana katika soka hadi ulipowaonyesha mlango wa ughaibuni wakatukimbia. Tuwezeshe kuwakumbuka vijana wetu waliokuwa wakilima nyanya pale kiloleni upande wa kushoto kama unatokea kule kanyenyela kwa akina mungu pole kanyenyela wa orion na wale wa chemchem kwa watusi na cheyo B karibu na kota za jeshi airport walipokuwa wakiuondosha umaskini kwa kujiajili bila mafanikio.

Wape moyo wa subira watu wako wa malolo na izimbili na kilimo dhaifu cha mahindi bila mbolea ilhali mbunge wao yuko bize kukamata jezi feki za simba kwa kuwa alichaguliwa ubunge ili kuwatumikia simba s.c. Na hatimaye uwakumbuke na walala hoi wa isevya na ipuli kule mnadani ambako kila jumamosi wanakula mbuzi wa wizi bila halmashauri yetu butu kukusanya mapato ili kutekeleza mipango ya maendeleo wakibakia kukimbizana na wakulima maaikini wa muhogo na wafuga kuku kulipia MDR hata kabla ya kujua kama watauza kuku wao ama muhogo wao.

Sote tunakuomba na kukusihi uwakumbuke na kule tambukareli na mihogoni ambapo wakulima wa mchicha hawajui wakauze wapi kwa kuwa mbunge wao kachagua kufungua Rufita Club ili dada zetu wakajiuze humo na vijana kwa wazee walewe pombe. Na hata wale vijana wavuvi wa Igombe nao mungu tunakuomba uwaepushe na ushuru mkubwa wa dagaa ambao wao wanawaita samaki ili wauze hao samaki wasiohata na jina waziendeshe familia zao. Wape nguvu na waonyeshe mwanga wale akina baba wanaoshinda pale Kachoma kila kilabu cha mataputapu na wanzuki waamke kwa kuwa sasa uchafu huo umepanda bei. Na mwisho nakusihi waamshe na kuwaonea huruma wakazi wa kule Itonjanda wachimbe visima bila kujua watapata wapi fedha za kugharamia kazi hiyo

Wa bilal taufik.

Ni mimi
Pangu Pakavu,
Nakuomba na Kukusihi.
 
Ndugu zangu,

Leo nimetembea kwa miguu kutoka mahali nilipofikia maeneo ya Ali Hassan Mwinyi Stadium hadi Chuo Cha Ualimu kunakofanyika mafunzo ya wanahabari. Umbali wa kilomita mbili hivi. Nimetembea nikiongea na wenyeji ambao wengi wanatembea kwa miguu. Kuna niliyojifunza njiani. Tabora si mji wa daladala, hazizidi nne mji mzima.

Baiskeli na pikipiki ndio daladala za Tabora Mjini. Na moja kubwa linalochangia Tabora kubaki nyuma ni miundo mbinu mibovu ikiwamo barabara na ukosefu wa usafiri wa uhakika wa treni umechangia kurudisha nyuma maendeleo ya Tabora.

Na lingine ni attitude ya umwinyi ya baadhi ya watu wa Tabora Mjini. Jana nimezunguka sana kutafuta vocha ya simu, naambiwa kuna wenyeji ambao hawataki kufanya biashara ya vocha ambayo faida yake yaweza kuwa shilingi elfu nne kwa vocha za laki moja! Tabora inahitaji muingiliano zaidi na watu wa mengine. Miundo mbinu itawezesha hilo.


Naam, Tabora iliyodidimia inahitaji kuinuliwa, na wenye jukumu la kwanza la kuifanya kazi hiyo ni Wana-Tabora wenyewe.
Maggid Mjengwa,
Tabora, Januari, 26, 2012
Mjengwa Blog::Habari,Picha,Matangazo
Tembelea pia; Tabora & Singida Press Clubs
 
Ni kweli Tabora yaitaji spesho atensheni.

ILA UKWELI UNABAKI PALE PALE .........
1.ccm imekuwa ikielekeza maendeleo kwenye maeneo/majimbo/mikoa yenye mchanganyiko wa siasa.
2.Ikiwa Tabora wanataka kukumbukwa ni lazima waamke kisiasa (sio lazma wawachague wabunge wa upinzani) kwa kupunguza idadi ya kura wanazoimwagia CCM

my take:KAMA UNAPATA MAZIWA BURE YANINI UJISUMBUE KUFUGA NG'OMBE i.e kama ccm inapata maelfu ya kura bure tabora yanini iwaonge/iwalainishe wanainchi maendeleo??
 
Hongera ndugu mwenyekiti kwa kutupa habari!!Ingawa ndugu mwenyekiti kila siku nasema pamoja na uandishi wako mahiri!lakini uuna kasoro kubwa sana!mi ni mfuasi wa mada zako nying kuanzia blog yako na hata kwenye magazeti!!Binafsi nilishawahi kukuambia ndugu mwenyekiti una umimi na kuijfanya kujua sana katika habari zako na maoni yako!

Ni nadra sana wewe kuchangia mijadala ya watu!iwe jamvini au kwingineko!!!ulichosema kuhusu Tabora ni sahihi!mi nikiwa mmoja wa watu tuliosoma Tabora Boys!Ila naona ni fursa nyingine kukumbusha jaribu kufanya mawazo yako yaangalie uhalisia sio tu kwa sababu ushapata publicity basi we ndo mjuaji wa kila kitu! Hivi ulivyoanzisha makala za Mamwindi na Dr Kreluu katika Raia Mwema hukujua kwamba ungeweza kuandika kitabu!!

Acha kujua kaka angu!!Unajitahid kuandika ila unapotoshwa na ujuaji wako ambao kuhishi kwako Sweden kwa muongo 1 nao nadhani huwa unachangia katika ujuaji wako!!!Utanisamehe kama nimekukwaza maana mimi kwako ni kichuguu kwa vyote umri na UJUAJI WA MAMBO ILA NATHUBUTU KUSEMA NINACHOFIKIRI!!!

KINAWEZA KUKUJENGA ZAIDI
 
Nimekulia Tabora, narudi Tabora, na ni ukweli usiopingika tabora inadidimia. Kwa kiasi kikubwa tabora ilikuwa inategemea uzalishaji wa mbao na kilimo - kuanguka kwa vitu hivyo kumeishusha tabora sana. Ili, iweze kuendelea kwa mazingira ya sasa, tabora inapaswa kujikita katika uzalishaji mbao na kilimo - haswa kupitia vyama vya ushirika
 
Mkoa wowote bila kuwa Mbunge wa upinzani hata mmoja kila kukicha badala kusonga mbele utakuwa ukirudi nyuma kimaendeleo! Mfano, mikoa ya kanda ya kati na mikoa ya kusini kwani CCM siku zote wanaamini maskini ndo mtaji wao. Na bado Tabora itazidi kudidimia.
 
Mkuu majid tatizo la Tabora ni umwinyi mwingi mno walionao wenyeji....ukichunguza hapo mjini utagundua bishara kubwa zote zinafanywa na Wachaga, Wa-Syria na Wahindi; wenyeji wanakaa kutwa vijiweni wakinywa kahawa na kucheza draft...hali yahuo mji kwa kweli inasikitisha sana. Hata zikifanyika juhudi gani bila kubadili-attitude na mind set ya wenyeji haitasaidia.

Sijui ni nini kitauokoa huo mji.
 
Sijakuelewa, una chuki na Maggid au.................
Hope amesema anachoona yeye na si aseme unachotaka wewe.
 
Back
Top Bottom