Tabia Zetu na Usafi: Najisi ni nini?

Steve Dii

JF-Expert Member
Jun 25, 2007
6,402
1,254
Hivi pale mtu anaposema kuwa 'hiyo imeingiwa na najisi' anakuwa anamaanisha nini haswa? Naomba maelezo tafadhali. Akhsanteni.

steved-albums-a-picture169-thisday-urinating-15-10-08.jpg

"An interesting take on this seemingly-difficult subject to understand is shown in this recent picture of one fellow comfortably and nonchalantly urinating in the same seashore waters being simultaneuosly used by numerous other people for various activities at the magogoni Ferry area in Dar es Salaam" (16-10-2008)

Picture courtesy of: Haki-hakingowi.blogspot.com. Description Courtesy of: ThisDay.co.tz
 
Najisi asili yake ni neno la Kiarabu na nitakapotoa tafsiri au maana zake si vema kuingiza udini. Maana ya kwanza na itumikayo sana ni uchafu ila huo uchafu nao una aina nyingi labda Kiingereza kitasaidia kutoa mwangaza: dirty, filth, impure, profane, contamination. Pia ipo najisi kitendo - (verb) k.m. kumnajisi mwanamke (defile or rape a woman).

Najisi kwa Uislamu (ritual uncleanliness) zipo aina nyingi vile vile lakini kwa muhtasari tu zinagawika kama najisi ndogo na najisi kubwa. Najisi kubwa ni ile ambayo Muumini akiwa naye au akiipata ni budi aoge udhu wake ukamilike, kama vile akifanya kitendo cha ngono, kutokwa na manii au kuchezea sehemu za siri za opposite sex, n.k. Lakini najisi ndogo (kwenda haja kubwa au ndogo, n.k.) udhu unaweza kupatikana kwa kutawadha tu, yaani kujiosha viganja vya mikono, mikono yenyewe, pua, uso na miguu. Baada ya kutakasika (kuzitoa hizo najisi) ndio Muumini anaruhusiwa kuswali, kushika Msahafu (Qur'an) na kufanya ibada zingine.

Swali lako naona limeambatana na picha ya Ferry huku mtu anakojoa baharini na mwingine anapaa samaki. Hiyo ni najisi anatia baharini lakini mimi sitatoa ufafanuzi iwapo hao samaki ni "halali", wasafi kuliwa au ni najisi pia! Nawaachia wenzangu wajuzi zaidi wachangie hii mada.
 
KJnne46, akhsante sana kwa maelezo, ni ya kina kwa kweli. By the way, jina lako bado laniwia vigumu kulitaja, je ulipotelea wapi ndugu?!
 
yani mtu anaekojoa hovyo mimi ananipandisha mashetani kabisa .. yani huyo kwenye picha natamani nimtoe hapo nimchape bakora ... kwani baharini hakuna nyoka bora hata angemnyofoa hiyo gadget yake.

najsi ni uchafu kama huyo anavyofanya na maelezo ya Kjnne46 yanatosheleza.. nasikia maji yakisogea kidogo unaona mpaka haja kubwa hapo ferry .. yani kinyaa
 
KJnne46, akhsante sana kwa maelezo, ni ya kina kwa kweli. By the way, jina lako bado laniwia vigumu kulitaja, je ulipotelea wapi ndugu?!

Jina langu sio siri, lipo ktk huo mfupisho wa "jnne" yaani jumanne.

Nipo bado lakini nasita kuchangia mada nyingi kwa sababu baadhi ya washiriki wanajawa na jazba na hawaijadili mada, na mara nyingi wanamponda binafsi mtoaji mada au mchangiaji. Kibaya zaidi hata wale ambao tungewategemea watusaidie kimawazo/kiutaalamu (k.m. wasomi wa Chuo kikuu) tunawakashifu mmoja mmoja na hata kumwita mtu "HUYO SI MWISLAMU TU!" Sasa dini na mchango wake yanahusiana nini ikiwa ana facts ama points za kuingia akilini.

Samahani kwa kwenda nje kidogo ya mada yetu ya najisi.
 
Back
Top Bottom