Kama uko bongo anza kumpaka pilipili kali katika kidole anachonyonya, inasaidia sana na nimeona wengi wameacha baada ya kupakwa pilipili. Nimesema kama uko bongo maana majuu ukigundulika kama unafanya hivyo basi hiyo ni Child abuse na unaweza kupoteza mtoto/watoto kwa kufanya hivyo. Kila la heri.
Mi nimenyonya mpaka form one ila usiku tu
na akili ilikuwepo tu lakini baada ya hapo niliacha
si ugonjwa na sidhani kama ni tatizo
Habari wanajamvi,
Nina kijana wangu ana miaka 8 mpaka sasa ananyonya kidole sana mpaka akilala, nimejaribu kumkataza sana, hana dalili ya kuwacha, nikawa namchapa ninapomuona ananyonya! lakini bado tu hana dalili ya kuwacha. Ninawaombeni jamani mwenye kujuwa njia au dawa ya kukabiliana na hili tatizo atuelimishe, natumai wengi hapa atakuwa ametusaidia
Asante mama...ila kula kucha nimeshindwa kuacha...watoto wangu nao wameiga
hata binti yangu wa 2 years ananyonya sana kidole gumba, nimejaribu kumdiscourage nimeshindwa. lakini akiwa occupied na michezo hanyonyi ila akiwa analia ataendup kunyonya na pia akitaka kulala. naogopa kumpaka pilipili maana akiweka kidole machoni atateseka sana. nimeamua kumwacha tu, lakini inasemekana hiyo process inaharibu dental arragement mdomoni.
hata binti yangu wa 2 years ananyonya sana kidole gumba, nimejaribu kumdiscourage nimeshindwa. lakini akiwa occupied na michezo hanyonyi ila akiwa analia ataendup kunyonya na pia akitaka kulala. naogopa kumpaka pilipili maana akiweka kidole machoni atateseka sana. nimeamua kumwacha tu, lakini inasemekana hiyo process inaharibu dental arragement mdomoni.
unahangaika nini ndugu yangu......... muache tu akikua ataacha............
unachanganya mambo mawili hapo.............. kukua kimwili na kukua kiakili............... huo umri wa miaka minane ni umri wa mwili na kutokana na maelezo yako inaonekana umri wa akili yake uko nyuma kidogo ya miaka minane............... hapo ndipo wazazi wengi hukosa hekima........... sio lazima akili na mwili vikue pamoja........ kuna watoto amabo akili iko mbele ya umri a wengine umri uko mbele ya akili. huyu wako naona mwili ndio uko mbele ya akili kwa makuzi............... jaribu kutathmini na matendo mengine ayafanyayo kama michezo, uhusiano na watoto wengine, nyimbo aazoimba, tabia ake wakati wa chakula nk...... utagundua kuwa ana tabia ambaz watoto wengine wa miaka 8 walisha ziacha.......... ushauri wangu:
1. endelea kumsoma. inaonekana hata wewe hujamjua vizuri na kama utaendelea kumhukumu kabla hujamjua sawasawa utamuathiri kisaikolojia
2. wakati unapoendelea kumsoma usimchukulie hatua ambazo ni harsh kama hizo ulizoshauriwa za kutumia pilipili, au viboko kama ulivyosema umewahi kumchapa............ ulifanya makosa, acha. unaweza hata kumfanya akuogope, kukuchukia, au hata akajiona hapendeki... ni hatari kwa saikolojia yake
3. jitahidi kusisitiza shule na uhakikishe anapata elimu bora
4. jitahidi kuzumgumza naye mara kwa mara na hasa mambo mbalimbali ya maisha kwa mfano hadithi za kidini kuhusu watu maarufu katika dini yako kutoka katika biblia kama hutojali
5. nk.
kwa kifupi, mwanao ni mzima hana tatizp lolote ila ukiendelea kumshughulikia bila busara wewe ndiye utakayemletea matatizo hasa ya kisaikolojia........................
BAK sidhani kama pilipili inasaidia. mimi nimenyonya sana kidole nikaja kuacha mwenyewe nilipoenda sekondari (bording). nilipakwa sana pilipili, sikuacha. nakumbuka siku kaka yangu alinivizia nikiwa nimelala akanipaka pilipili, badala ya kuvyonya kidole nikakiweka jichoni, ilikuwa balaa. na sikuacha.
ataacha akikuwa, miaka 8 bado mdogo. akikua ataona aibu.
.........Kumbe tupo wengi tunaokula kucha, mie udogo wangu nilikuwa nanyonya kidole baadaye nilivyokuwa nikaacha kunyonya kidole nikahamia kwenye kucha. Huwezi amini hadi leo bado nakula kucha za vidole vya mkononi, natamani kuwa na kucha ndefu lakini siwezi kuvumilia kula kucha.
Sasa hivi nimeamua kukomesha hii tabia ya kula kucha, nimeamua kuweka kucha bandia na kupaka rangi ili nitakapotaka kula kucha nakutana na rangi.......lakini ninamiss kweli kweli kula kucha zangu......hivyo nimeacha kama vidole vitatu special kwa kula kucha.
........Ndio maana nataka kuacha kaka yangu, maana kucha ni sehemu ya urembo ya mwanamke. Halafu hizi kucha bandia wala sijisikii kabisa kuwa comfortable nikiziweka.........hata hivyo nimeshapiga hatua katika kuacha, siku hizi nanunua candies ili nikijisikia kula kucha basi nachukua candy nakula.Mhhhh! Pretty! warembo hawali kucha bwana!!!!...umekosa vya kula? Ziache kucha zipendeze
Asante mama...ila kula kucha nimeshindwa kuacha...watoto wangu nao wameiga
Sioni haja ya kuanzisha thread nyengine, hata hivyo naomba ruhusa kwa mwenye thread hii nitoe mchango wangu kwa kuweka nami nililonalo..
.
Kijana wangu 4yrs old nae alikua na tabia hiyo (ya kunyonya kidole), tulifanikiwa kumsaidia kuacha kwa kumkataza kwa maneno na wakati mwengine tulimfunga plasta.
Ila amekuja na tabia nyengine ya ajabu pia,,anachofanya sasa ni kwamba, anapokula chakula akiweka tonge moja linabaki kinywani kwa muda mrefu sana (anamung'unya) kwahiyo wakati wa kula lazima kuwe na mtu wa kumsisitiza atafune chakula na kumeza,,vyenginevyo itamchukuaa hata 2 hours kula chakula,,na mara kadhaa anapokua amelala usiku utakuta ana chakula kinywani.
Bado tunaendelea kumuelekeza lakini kama kuna njia nyengine ya kumsaidia naomba michango yenu