Tabia hii ya Wachina mh

MONTESQUIEU

JF-Expert Member
Nov 8, 2010
847
80
Napenda sana chakula cha wachina but tabia yao hii inanishinda

Nimekuwa nikienda kwenye hotel zao mara kadhaa kupata kitu roho inapenda but Karibu mara mbili sasa nimeshindwa kula chakula nilichoagiza katika hoteli za kichina kwa sababu,ya tabia ya Wachina ya kutoa kamasi na makohozi mbele yangu wakati nataka kula .
kwa kweli nimetafakali hadi nimeshindwa kupata jibu.
Kwa wanao wajua zaidi
Je hii ni tabia yao au hawapendi rangi ingine iingie mahotelin kwao?
 
Swagger tu hizo. Neksti taimu fanya teki awei ukalie hom kwako!
 
Kama unaweza kula vyakula vya Kichina, kamasi litaweza kukutia kichefuchefu? coz msosi tu mi natapika!!
 
Sina uhakika kama ni utamaduni wao au ni individual case maana nimeshakutana na waafrika, wazungu wenye tabia kama hiyo pia.
 
me wananiuzigi wakiwa wanakala huku wanavuta sigara at the same time. hii sasa nchini kwao ndo imekithiri. km kuna mwanajamii amewahi kukaa nchini mwao zaidi ya mwaka atakuwa anafahamu. its too bad!!!!!!!!!!!!
 
i think ni mgahawa tu ulioenda mbona mingi tu iko shwari!
 
Hili pia wanalifanya hata hapa
 
i think ni mgahawa tu ulioenda mbona mingi tu iko shwari!
Huwa napita pita nchi za Asia mara kwa mwara ....Wahindi na Wachina nimefanya nao kazi sana. Mchina kutema mate/kohozi mbele ya kadamnasi si jambo la ajabu. Hata ndani ya benki ataliweka.Na Mhindi kuchafua hewa sio jambo la aibu. Mtafanya kazi chumba kimoja lakini jamaa atakuwa anaachia ushuzi wenye harufa kali sana ya zile spices zao.... inakera
 
Ndivyo walivyo, wao wanaona ni kawaida tu sawa na kuvuta pumzi sasa mtafanyaje? Malezi hayo na utamaduni.
 
Kwenye kambi zao hasa kwenye project za kujenga barabara huwa wanachota vinyesi chooni kwa ndoo na kumwagilia bustani za kabechi na mboga nyingine. Hawaelewi wengine tunapokuwa na kinyaa kula kabechi hizo.
 
Huwa napita pita nchi za Asia mara kwa mwara ....Wahindi na Wachina nimefanya nao kazi sana. Mchina kutema mate/kohozi mbele ya kadamnasi si jambo la ajabu. Hata ndani ya benki ataliweka.Na Mhindi kuchafua hewa sio jambo la aibu. Mtafanya kazi chumba kimoja lakini jamaa atakuwa anaachia ushuzi wenye harufa kali sana ya zile spices zao.... inakera

Hii ya wahindi nayo kali kivyake..
 
uhindini huku tushazoea hali hii...akienda kunawa kwenye sink la maji...duh unaweza kutapika kabisa...lol wahindi
 
Sio magahawa yote ya kichina iko hivyo inategemea uko wapi. Kama upo huko Dar naweza kuhisi mgahawa unaouongelea. Lakini mara nyingi chakula unachokuta kimepambwa sana kwenye mahoteli shika shika huwa kubwa pia. Vinginevyo jaribu teppanyaki za kijapan, chef anakuwa yuko mbele yako mnakuwa mnashauriana naye. Mtu wa kinyaa unakuwa umepata ahueni kidogo.
 
usiende TENA na uwaambia kabisa kuwa hutaki kwenda kutokana na tabia yao hii,kama kwao ni kitu cha kawaida lkn sie kwetu ni kitu kisichokuwa cha ustaarabu.waambie hapa sio China hii ni Tanzania,
sheshee
 
Mkuu baada ya wao kupenga makamasi mbele yako, je uliwaeleza juu ya kukerwa kwako na hiyo tabia? Manake wewe kama mteja una haki ya kumweleza mhusika dukuduku lako ili aweze kuboresha huduma yake, kwa manufaa yako kiafya na ya kwake kiuchumi.
 
Kosa nililofanya nikutowaeleza, but kwa kuondoka bila kula ni ujumbe tosha
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom