Tabata demolitions:Director sacked

BAK

JF-Expert Member
Feb 11, 2007
124,790
288,006
I am glad to know that there are still some leaders in Tanzania who can make the right decision and say "You are fired" I wish JK could do the same instead of waiting for the so called viongozi to resign.

Tabata demolitions: Director sacked

THISDAY REPORTER
Dar es Salaam

ILALA Municipal Director John Lubuva has reportedly been sacked for his role in the controversial demolitions of over 80 residential houses at Tabata Dampo in Dar es Salaam late last month.

Sources within the Dar es Salaam City Council have told THISDAY that Lubuva was relieved of his duties early this week in the wake of widespread condemnations of the demolitions that left hundreds of people without shelter and destroyed property worth millions of shillings.

The sources said the Temeke Municipal Director, Idd Nyundo, has been appointed to fill the vacancy left by Lubuva, while the Temeke position has been filled by an official identified only as Kongwa.

When asked by THISDAY to respond to the reports, Dar es Salaam city Director Bakari Kingobi, said he could not confirm or deny anything, but conceded that changes had been made in the Ilala Municipality administration.

''I am not the spokesman for IIala Municipality and thus for me to address such an issue will be illegitimate,'' Kingobi said.

It has also been verified that the Dar es Salaam regional commissioner's office has already been formally notified of the changes by the ministry responsible for local government and regional administration within the Prime Minister's Office

The RC, Abbas Kandoro, was an early visitor to the demolition scene and at the time expressed shock at the destruction caused without his knowledge.

He also pledged that those responsible would be severely disciplined.

While the Ilala municipal engineer and legal director were both suspended from duty soon after, a defiant Lubuva continued to ignore calls for his resignation.

The Tabata Dampo demolitions were roundly condemned by the public, particularly since a court case related to the dispute at hand was still pending.

A presidential- government probe team was subsequently formed to further investigate the incident amid strong allegations of bribery involving senior municipal officials.

The over 300 affected residents have in the meantime been living in makeshift shacks provided by the RC's office and other charitable institutions, awaiting compensation.

They have been allocated plots at Chanika on the outskirts of the city, but say they cannot move there even after getting compensation, until the government puts necessary infrastructure at the site.

According to one of the victims, Tauzany Bwana, fresh attempts by Ilala Municipality officials to relocate them to Vingunguti Secondary School temporarily have also been rejected.
 
yote sawa tu...wasingefukuzwa kwa kubomoa Tabata.......walitakiwa kufukuzwa kwa kuruhusu watu kujenga kiholela ndani ya jiji
 
Isije kuwa danganya toto nyingine. Mtu anafukuzwa kwa mbwembwe halafu baada ya siku kadhaa mnasikia ni mkuu wa wilaya fulani huko! Au anaenda mahakamani na kulipwa mamilioni kama wale maafande wa polisi waliotimuliwa na Mkapa miaka ile! Hatua ya kumtimua tu mtu kazini haitoshi, kwani bado inaacha maswali kadhaa: Kutimuliwa kwa huyo mkurugenzi kunawasaidiaje waathirika wa bomoabomoa hiyo? Kutimuliwa kwa huyo mkurugenzi kuna athari gani katika sheria na taratibu zinazoongoza mambo hayo ya mipangomiji katika halmashauri? Atimuliwe, sawa, kama adhabu kutoka kwa mwajiri wake, lakini pia ashtakiwe kwa adha aliyowasababishia wananchi. Na wahusika wote wafanyiwe hivyohivyo. Hatua zichukuliwe kuziba mianya yote waliyotumia kufanya uonevu huo. Na wananchi walioathirika na uzembe/uonevu huo wafidiwe ipasavyo. Hapo nitaridhika kuwa hatua zimechukuliwa.
 
Isije kuwa danganya toto nyingine. Mtu anafukuzwa kwa mbwembwe halafu baada ya siku kadhaa mnasikia ni mkuu wa wilaya fulani huko! Au anaenda mahakamani na kulipwa mamilioni kama wale maafande wa polisi waliotimuliwa na Mkapa miaka ile! Hatua ya kumtimua tu mtu kazini haitoshi, kwani bado inaacha maswali kadhaa: Kutimuliwa kwa huyo mkurugenzi kunawasaidiaje waathirika wa bomoabomoa hiyo? Kutimuliwa kwa huyo mkurugenzi kuna athari gani katika sheria na taratibu zinazoongoza mambo hayo ya mipangomiji katika halmashauri? Atimuliwe, sawa, kama adhabu kutoka kwa mwajiri wake, lakini pia ashtakiwe kwa adha aliyowasababishia wananchi. Na wahusika wote wafanyiwe hivyohivyo. Hatua zichukuliwe kuziba mianya yote waliyotumia kufanya uonevu huo. Na wananchi walioathirika na uzembe/uonevu huo wafidiwe ipasavyo. Hapo nitaridhika kuwa hatua zimechukuliwa.

Mimi najua kasimamishwa kazi ili uchunguzi uendelee .These are double standard yaani BOT wanaendelea kupeta na Tume zipo lakini wa Jiji anafanyiwa kweli ? Ama kweli kuna kazi za kuzima moto.Lakini huyu mjinga waliwahi kuvuta gari na kulifungia basi nilimtolea uvivu hadi akalitoa.Ana dharau sana .Mwache aoshwe .

Posted Date::3/20/2008
Serikali yamsimamisha kazi Mkurugenzi Manispaa ya Ilala
Na Muhibu Said

SERIKALI imemsimamisha kazi Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala, jijini Dar es Salaam, John Lubuva, kutokana na kashfa ya kuvunjwa kwa nyumba zaidi ya 99 za wakazi wa Tabata Dampo, kulikofanywa na baadhi ya watendaji wa manispaa hiyo, kinyume na taratibu.


Lubuva ambaye hivi karibuni alikaririwa na baadhi ya vyombo vya habari akigoma kujiuzulu, amesimamishwa kazi wiki hii kutokana na kashfa hiyo iliyosababisha wakazi hao waendelee kuishi katika mahema hadi sasa.


Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Stephen Wassira, alimwambia mwandishi wa gazeti hili kuwa Lubuva amesimamishwa kazi kutokana na ubomoaji wa nyumba hizo.


Alieleza kuwa uamuzi huo umefikiwa na serikali ili kupisha tume iliyoundwa na manispaa hiyo kuchunguza uvunjwaji wa nyumba hizo.


"Kuna makosa yaliyotendeka na kuna tume iliyoundwa kuchunguza, hivyo ni jambo la kawaida kwa kiongozi anayehusika kuwajibika ili kupisha uchunguzi wa tume. Ukikamilika ataambiwa uamuzi," alisema Wassira.


Alisema bado hajafahamu lini Lubuva alipewa barua ya kusimamishwa kazi, lakini akasisitiza kuwa mkurugenzi huyo wa siku nyingi amesimamishwa kazi katika manispaa hiyo.


"Sijui barua amepewa lini, lakini najua amesimamishwa kazi," alisema


Lubuva anakuwa kiongozi wa pili kusimamishwa kazi katika manispaa hiyo kutokana na uvunjwaji huo uliofanywa kiholela na watendaji wa manispaa hiyo.


Kiongozi wa kwanza kusimamishwa, ni Mhandisi wa Manispaa hiyo, Iddi Kisisa aliyesimamishwa kazi siku chache kwa tuhuma za kusimamia uvunjwaji wa nyumba hizo, ulioelezwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Abbas Kandoro hivi karibuni kuwa ulikiuka haki za binadamu.


Awali, Kandoro alishauri kufukuzwa kazi kwa viongozi wote wa manispaa hiyo watakaobainika kuhusika ama kuamuru au kubariki uvunjwaji wa nyumba hizo.


Akielezea sababu za hatua hiyo kali kwa watendaji hao, alisema imetokana na ama uzembe au kutowajibika kwao katika maamuzi yao, hivyo kusababisha uvunjaji wa haki za wakazi wa eneo hilo ambao nyumba zao zilivunjwa Februari 29, mwaka huu.


Alifahamisha kuwa kitendo cha uongozi wa manispaa hiyo, kuwavunjia nyumba wakazi hao, siyo cha kiungwana na kimekiuka misingi ya haki za binadamu, utawala bora, taratibu na sheria.


Alisema uchunguzi wa kina uliofanywa na ofisi yake umebaini kuwa eneo la Tabata Dampo lilikuwa na mgogoro wa muda mrefu na mtu anayejulikana kwa jina la Allied Cargo Freight, ambaye amedai kumilikishwa kihalali mwaka 2002.


Lakini walalamikiwa wakakata rufaa Mahakama Kuu ambako mwaka 2003 chini ya Jaji Masati mahakama hiyo, haikutoa haki kwa upande wowote bali iliamuru kesi hiyo irudishwe katika baraza la usuluhishi


Alisema ilipofika Februari 5, mwaka huu, Freight alifungua kesi katika Baraza la Ardhi Ilala, kuishtaki manispaa hiyo kwa kutoa vibali hivyo vya makazi, kesi ambayo hukumu yake ilitolewa Februari 18 kwa kutaka wakazi hao waondolewe eneo hilo kwa gharama za manispaa yenyewe.


Katika kutekeleza hukumu hiyo, Februari 27 mwaka huu manispaa hiyo, ilipeleka notisi kwa Afisa Mtendaji wa Tabata, kumtaka awatangazie wananchi hao kuondoka au kusubiri kubomolewa nyumba zao.
 
Wanafukuwa watu wadogo wadogo tu lakini hao walioko Wizara ya Sheria, TAKUKURU na kwingineko mnasubiri wajiuzuru wenyewe???????????? Ni busara gani hizi!! Najua wananchi wa Tabata na maeneo hayo walipata shida sana baada ya kubomolewa nyumba zao. Sasa watanzania wengine ambao wanazidi kutaabika bado na maisha ya kubahatisha kutokana na UFISADI wa SISIEMU wamekuwa INVISIBLE??????????????????

Jamani sheria i-apply kwa yeyote equally na si kwa sababu huyo yuko TAKUKURU au Manispaa Ilala. JK tafadhali acha kuangalia sura au viuno vya watu, wajibisha watu hapa, kila mtu kwa adhabu anayostahili. BE SERIOUS just for a minute.
 
.............hili jambo linachukuliwa kisiasa ...lile eneo ni la mtu na ana hati....watu wanavamia na wanajenga ..wanarpotiwa serikalini ,,hakuna hatua inayochukuliwa kuwaondoa.....eneo ni la viwanda!!!

kwa kuwa serikali iliyopo ni populist inapenda kufanya jambo kisiasa kufurahisha watu....lakini in reality wale waliobomolewa wanayo makosa ..kosa la watu wa manispaa ni procedural..waliyotumia kuvunja...lakini hilo halibatilishi hukumu..

wazee sheria ipo pande mbili...haki ya yule mwenye eneo pia lazima ilindwe...nina wasiwasi kuwa kuwa kitendo cha serikali kutisha watendaji wanapochukua hatua itawafanya waogope ku enforce law....lazima tufuke mahali tuondokane na ujenzi wa kiholela .....na uamuzi wa kupambana na ujenzi holela tusitegemee ufurahishe wananchi..ni uamuzi mzito...


ni aibu ukiingia kwa ndege kweye anga la dar es salaam ubaona jinsi nyumba zilivojengwa kama mkutano wa inzi......lazima zibomolewe zote....na maeneo kama jangwani,tandale,manzese...makampuni kama nssf wajenge maghorofa hao wakaazi wapewe kipaumbele kukopeshwa au kupewa bure..floor zinazobaki zikodishwe.....tutabakiwa na maeneo ya wazi..maeneo kama vingunguti tubomoe kwa njia ya PPP[public private partnership]....tujenge viwanda...na waendelezaji wa viwanda wajenge magorofa kuwaweka hawa wakazi pamoja na kuwalipa mapesa
.......

mnajua nji wa dar es salaam unapanuka horizontal unnecessarry....hii inaongeza gharama za kuwafikishia wananchi huduma....

namshauri muheshimiwa rais na waziri mkuu wasiogope kuchukua uamuzi mziti kusafisha jiji kwa kuogopa kukosa kura....tukienda nchi za watu tunaona wivu na kuona aibu bado tua mji holela!!!!!
 
Back
Top Bottom