Taasisi gani z/ipewe jina la Kawawa na kwanini?

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,476
39,995
Kuna mjadala unaendelea wa kutafuta namna ya kumuenzi mzee Kawawa kwa kuliweka jina lake katika taasisi moja au zaidi ili kuakisi mchango wake katika historia ya ujenzi wa taifa letu. Hii inatokana na ukweli kwamba alitoa mchango mkubwa katika haki za wafanyakazi, sanaa, lugha na michezo na hata katika jeshi.

Alikuwa ni mwigizaji wa kwanza mzalendo
Muasisi wa shirikisho la wafanyakazi wa serikali
Mkuu wa nchi
Alitoa agizo la matumizi ya lugha ya Kiswahili katika shughuli za ofisi (agizo lake limerudiwa hivi karibuni)
Alishiriki katika uhamasishaji wa JWTZ wakati wa vita vya Kagera hadi kwenda mstari wa mbele kuwahamasisha wapiganaji
Alishiriki katika kandanda na hata kuwa mwamuzi

Ukiondoa barabara iliyopewa jina lake, ni taasisi gani nyingine ambazo zingeweza kupewa jina lake kwa heshima yake na mchango wake kwa taifa?
 
Mwanakijiji,
Kwa sababu elimu haina kikomo, ningependekeza tujenge Technical College nyingine tuipe jina The Rashid Kawawa Technical College of Tanzania.
 
Ikulu ipewe jina la Kawawa kwani alihimili sana mashuti na lawama zilizotokana na maamuzi mengi ya Ikulu.
si vibaya kuitwa jina lake kwa kuwa majengo mengi ya serikali yana majina mf. sukari hausi, Mawasiliano hausi (TCRA), Nkurumah hall, n.k.

natoa hoja
 
Nafikiri vitu karubu vyote vimeshapewa majina ya watu kasoro bandari na vitakavyojengwa baadae
 
Ringo acha utani.
Bandari iitwe kawawa, unajua maskhara yaliyopo pale? usijekupeleka jina lake kusiko shekhe.

Nimesema Ikulu maana wengi tutamkumbuka hata vizazi vijavyo watakuwa na shahuku ya kumjua shujaa huyu wa imani
 
Kwa kuwa alikuwa muigizaji wa kwanza mzalendo (sikujua hili, asante Mkjj), pengine chuo cha sanaa Bagamoyo kingeweza kupewa jina lake. hii ita-draw attention na kukiwezesha kupandishwa hadhi (natamani hata kingefikia kuwa chuo kikuu).
 
Ni kweli nadhani ingeundwa taasisi ya elimu au sanaa na ikapewa jina lake kumuenzi au hata taasisi za lugha kwani alikuwa akikipenda kiswahili na alikuwa anahimiza sana matumizi yake....
 
Mbona kashaenziwa kwa vitu vingi tu?kuna barabara ina jina lake,shule za msingi na sekondari kibao zina jina lake bado tu mnataka na mataasisi tena.Lakini pili hivi mtu anaenziwa kwa kupewa jina kwenye taaisisi au ni kwa kufuata matendio yake?Kila mtu akifa jina lake linapewa taasisi lol..Hivi hatuna staili nyingine ya kuwaenzi hawa ndugu zetu?hebu tuanze kuthink outside ze box..Lol.
 
Katika mambo aliyofanya mwishoni kabla hajaachia madaraka yake ilikuwa ni kuhamasisha wananchi wawe na "mshikamano," na nadhani ni yeye aliyeeneza masamiati huo kwa haraka. Kwa vile ofisi ya msajiri wa vyama vya siasa inatakiwa kuhudumia vyama vyote kwa usawa, na hivyo kudumisha mshikamano miongoni mwa wanatanzania wote bila kujali vyama vyao, basi ninashauri kuwa Ofisi ya Msajiri wa Vyama vya siasa iitwe "Ofisi ya Vyama Vya Siasa ya Kawawa (Kawawa Political Parties Office)" au simply "Ofisi ya Kawawa" (Kawawa Office)" na ijengewe jengo la kudumu (kama halipo) na lenye vifaa vya kisasa litakaoitwa "Kawawa House." Kufanya hivyo watanzania wote tutapewa mwanya wa kutosha wa kutunza legacy ya Mzee Kawawa bila kujali itikadi zetu.
 
Mzee Mwanakijiji nadhani tutakuwa wanafiki tukianza kusema tutafute namna ya kumuenzi Kawawa wakati wote tunaijua na ipo wazi, ila tunajutahidi kuikwepa kadiri tuwezavyo. Si kwa kuipa jina lake shule fulani, barabara au hata kijiji. Tunaweza kumuenzi kawawa kwa kuwa waadilifu kama yeye, kwa kutokuwa wezi, waongo, na walaghai. Tukimuenzi Kawawa kwa njia hiyo tutakuwa na manufaa makubwa sana.
 
kwa kuwa tuna sokoine univesity, Mkwawa Univesity, basi Dodoma univesity iitwe Kawawa Univesity, vile vile naunga mkono KIA-Kawawa Internatioal Airport
 
Kwa kuwa kawawa alikua pia ni mwanzilishi wa JKT basi ni vyema makao makuu ya jkt yakaitwa R. M. Kawawa au hata mgulani jkt paitwe kawawa, pia Machinga complex kwa kuwa zipo barabara ya kawawa ziitwe kawawa complex.

Pia jamani kuna huyu makamu wa Raisi aliefariki akimalizia kazi zake barabara ya kilwa, kwa heshima yake kwa nini barabara hiyo isiitwe Dr. Omar Ali Juma Road?ni ushauri tuu
 
Back
Top Bottom