Taarifa za Rostam kuunga mkono CDM Arumeru zakupikwa; Slaa akanusha vikali

Status
Not open for further replies.
Kwa kweli kwa uongo mnaongoza. Nimongea na Rostam muda mfupi uliopita akiwa Pariis Ufaransa, Waikati huo huo Chadema mnasema yuko Arumeru anawasaidia !! Hata propaganda lazima iwe inafanana na ukweli siyo uongo mtupu.
Mweka hazina wa CCM anasema yupo Ujerumani na Rostam mwenyewe alikiri alikuwa Arumeru wewe unabisha nini?
 
Mimi nafikiri hapa kuna mchezo unachezwa na Rostam Azizi kupitia hilo gazeti la Dira. Wenye habari kamili kuhusu gazeti la dira watupe mweleko wake iko huru, inaegemea wapinzani au ni vuvuzela la mafisadi, kundi fulani katika makundi ya ccm nk. Naona wanataka kumsafisha Rostam Aziz.
Ila kama ni kweli CDM wawe makini ni kwamba ni kwamba CDM wamemshinda Rostam na sasa anatumia filosofia ya " If you cant beat them, join them"
Hili ni gazeti la Sitta na walimuhoji na kumnukuu Rostam hivyo si habari ya uongo maana angekanusha
 
lakini inawezekana kweli mbona hata chadema hawajakanusha.!
 
lakini inawezekana kweli mbona hata chadema hawajakanusha.!
Chadema hawana sababu ya kukanusha maana muhimu ni maneno ya Rostam. Kwamba ni fisadi akiongea point tumpinge hapana
 
jamani huyu ni mfanyabiashara mwanasiasa ''business man politician"..rostam aziz hahitaji msamaha wa mtu yeyoye ili aweze kuishi nchi hii.ataendelea kuwepo na ataendelea kuwekeza nchi hii..hela ya ccm hadi leo tunavoongea inazalishwa na huyu msomi,na mbali ya hapo chama cha raila odinga (odm) ndani ya kenya kina mtumia kwa kazi hiyo hiyo..huyu sio tajiri mjinga,huyu ni tajiri anaejua anafanya nini!!
dowan(ya rostam & his co.) wanaidai tanesco Tsh. bilion 111/= +riba!, tafakari!
 
Kwa kile kinachoonekana kuwa Rostam Aziz ameanza kuhofia Chadema kushinda 2015, ameiunga mkono moja kwa moja katika uchaguzi Arumeru. Rostam alitembelea kambi sita za chadema katika kata mbalimbali. Huwezi kuyaamini maneno haya ya Rostam. Nanukuu:

"...ninachoomba kwa wananchi wa hili ni kuhakikisha wanamchagua mbunge mwenye uwezo wa kuzungumzia hoja za matatizo yao bungeni na sio kushawishi kuchagua chama kama ilivyo mazoea ya watanzania"

"Wagombea wote ni wazuri lakini ninawasihi wananchi wa Arumeru wachoke kudanganywa wajitahidi kuchagua tumaini la maisha yao, waondokana na kasumba ya kugawiwa vitu bure kwa ajili ya kuchagua chama fulani, ndio maana ikaitwa demokrasia.

Akizungumza na mwandishi wa gazeti hili kuhusu ujio wa Rostam, Dr Slaa alisema kitendo cha Rostam kutoa baraka kwa Nassari ni kutokana na kuzichoka siasa uchwara za CCM na kuzikubali siasa safi za Chadema.

Source.Dira ya Mtanzania.

My take, Rostam inaonekana anaiunga mkono chadema na nadhani anahofia itashinda 2015 hivyo ameanza kuwaunga mkono washindi tangia mwanzo

Mtoa mada unajikanganya.
Hapo uzalendo uko wapi ndani ya Rostam, na hiyo ndo naita unafiki.
Leo anaitwa fisadi kwa vile yuko CCM lakini fisadi huyohuyo akiwashabikia CDM basi ni uzalendo, what a cheap way to think!!
 
quote_icon.png
By sailor1
Kwa kweli kwa uongo mnaongoza. Nimongea na Rostam muda mfupi uliopita akiwa Pariis Ufaransa, Waikati huo huo Chadema mnasema yuko Arumeru anawasaidia !! Hata propaganda lazima iwe inafanana na ukweli siyo uongo mtupu.

Mweka hazina wa CCM anasema yupo Ujerumani na Rostam mwenyewe alikiri alikuwa Arumeru wewe unabisha nini?

Rostam hawezi kutembelea Arumeru kwa sasa mtu ana viwanja Dubai, jioni yupo Hongkong, Igunga hajawahi kaa zaidi ya wiki hata km ni Kampeni, leteni thread za uhakika au Mods azipeleke Jokes
 
Chadema hawana sababu ya kukanusha maana muhimu ni maneno ya Rostam. Kwamba ni fisadi akiongea point tumpinge hapana

kwa hiyo rostam anapingwa akiwa ccm akiwa chadema anakubalika... Kwa hiyo tuamini mafisadi wabaya wakiwa ccm wakiiunga mkono chadema wasafi...kweli baniani mbaya kiatu chake dawa.
 
kwa hiyo rostam anapingwa akiwa ccm akiwa chadema anakubalika... Kwa hiyo tuamini mafisadi wabaya wakiwa ccm wakiiunga mkono chadema wasafi...kweli baniani mbaya kiatu chake dawa.
Rostam ana haki ya kuongea. Sasa tuyachambue maneno aliingea badala ya kumwangalia aliyeongea. Je, maneno yake mabaya au mazuri? Ni fisadi sawa, lakini bado ana haki ya kutoa mawazo yake. Ni kama Lowassa anavyosema ukweli kuwa serikali inaogopa kuchukua maamuzi magumu au vijana wasio na ajira ni bomu. Hayo ni mambo ya kweli hatuwezi kumkosoa tu kwa vile ni fisadi.
 
Mtoa mada unajikanganya.
Hapo uzalendo uko wapi ndani ya Rostam, na hiyo ndo naita unafiki.
Leo anaitwa fisadi kwa vile yuko CCM lakini fisadi huyohuyo akiwashabikia CDM basi ni uzalendo, what a cheap way to think!!
Kwenye siasa huwezi kuepuka. Kwani akina Mrema, wasira, kaburu, lamwai nk CCM walikuwa wanawaitaje walivyokuwa wanachachafya huku upinzani? Leo wanawaitaje? Hata leo Rostam akiungama na kuipinga ccm corrupt hii kwanini tusimpokee? Kama Mungu anasamehe sisi ni nani?
 
Sasa tutaanza kuona thread za kumtukuza Rostam huku muda si mrefu!Haya watanganyika endeleeni na siasa zenu bana wengine watazamaji tu sisi!!
 
Rostam ana haki ya kuongea. Sasa tuyachambue maneno aliingea badala ya kumwangalia aliyeongea. Je, maneno yake mabaya au mazuri? Ni fisadi sawa, lakini bado ana haki ya kutoa mawazo yake. Ni kama Lowassa anavyosema ukweli kuwa serikali inaogopa kuchukua maamuzi magumu au vijana wasio na ajira ni bomu. Hayo ni mambo ya kweli hatuwezi kumkosoa tu kwa vile ni fisadi.

mkuu unachoongea ni kweli lakini lazima tujiulize kwa nini sasa na sio hapo awali.?je pamoja na kukiunga mkona ccm na kukidhamini kwa wakati wote unaweza kuamini kuwa anachokiongea ndio anachomaanisha lazima utathimini kwanza je amekiri madhambi yake ili aaminike...siamini kama dr. Slaa anaweza kuingia mkenge kirahisi namna hiyo kwa kumwamini rostam kwa maneno yake mepesi kiasi hicho....labda tungepata udhibitisho je rostamu ni kweli ilikisapoti chadema arumeru ndio tuendele kujadili.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom