Taarifa za mikopo midogo midogo ya kibiashara!

Naomba wadau wa jukwaa hili tusaidiane kuweka taarifa muhimu za kibenki ili ziwasaidie wadau wanaohitaji mikopo midogo midogo na ile ya kati kwa ajili kuendesha biashara. Natamani tungekuwa na business directory ila sijui kama ipo ....(wenye taarifa watatusaidia).

Nimeweza kukusanya hizi taarifa na naomba wadau muongeze kile mnachokijua,

1. CRDB Bank Ltd...Mikopo midogo midogo (may be 1-20 mil), interest rate (with insurance) ni 20%, na lazima mtu awe na hati ya kiwanja au nyumba

2. FINCA .....Nimepata taarifa kuwa mtu akikopa 15mil anatakiwa kurudisha 1.7mil kwa mwezi ambayo inatupa interest ya 33.3%

3. NBM.....Kuna mtu kachukua loan ya 30mil ambayo atailipa kwa miaka 4; interest + other charges imefikia 12mil (40%)
........Nimepata taarifa za NMB kwamba small loans (100K-5mil) interest rates in 24% (2% per month)

4. TIB (Tanzania investment Bank)...Wanatoa mikopo ya kati na mikubwa...Nasikia wanaanzia USD 150K

5. SACCOS...SACCOS ambayo mie ni mwanachama inatoza 13% ila wanatoa pesa ndogo ndogo (1-10mil) na lazima ukae kwenye queue kwa karibu miezi 6!

7. NBC...Wanatoa mikopo kwa riba ya 20-24% ila iko based on overdraft. Unatakiwa kuwa na hati ya nyumba au dhamana nyingine. Kwa ujumla nimependa package yao ingawa riba bado iko juu sana!!

8. Exim wanatoa mikopo ya biashara kwa riba ya 19%. Unaweza kuchukua zote au kwa overdraft!!

9. Barclays bank wanatoa mikopo ya kati na mikubwa tu (>50mil). Interest yao ni 25%.

10. Stanbic wanatoa mikopo ya biashara pia...interest rates zao ni 21% na matakwa mengine ni kama kwa banks nyingine (hati ya nyumba, leseni ya biashara, audited accounts etc)!! Hawa nao wanatoa overdraft facilities!

11. Kenya Commercial Bank (KBC)....wana mikopo ya biashara kuwanzia 10mil na interest rates zao ni 19%. Masharti mengine ni kama banks nyingine na wanakubali overdraft..Ila sikuweza kupata details za interest rates per month kwenye overdraft!

12. Equity Bank....Inasemekana watakuwa na masharti nafuu ila bado hawajaanza kufanya biashara rasmi. Tutazidi kuwafuatilia!


Mwenye taarifa zaidi atuwekee hapa ili tuweza ku-update hii page ili iwasadie wale wanaohitaji mikopo ili wajikwamue!

Babu DC!!

Updates

Important information (TIB)





Equity Bank

Wote naona interest zao ni about 20%
 
Imeongelewa mikopo toka benki na taasis za fedha, mikopo toka kampuni za simu ipo, lakini itawafilisi watu na serikali inatazama. Riba ni tishio, kwa mfano mikopo ya timiza ni 14.5% kwa siku 21! Kwa mwaka nawaachia wachumi waendelee.
 
Je hii ya lazima uwe na dhamana wakati ndo unaanza ipoje TUNAPENDA SANA KUKOPA TATIZO MASHARTI YAKE MAGUMU KATIKA BANK NYINGI TZ
 
Benki Bora ya kukopa ni NMB tu ila kuupata utatembea miezi mitatu, watakuzungusha ili uwabip na rushwa, ukichukua 10,000,000/= jua 1mil au laki sita 600
 
Sasa wengine hizo shule za asilimia hatujui nambie nikikopa laki sita au millioan moja narejesha ngapi fedha !
 
Tanzania Womens Bank riba zao ni nafuu Sana ni 12.5%, na mikopo yao ipo ya miezi sita 200,00/= hadi 400,000/= na mwaka mmoja hadi miwili 500,000/= hadi milioni 3.
 
Habari,jaman Mimi Nina Kiwanja Kipo Iringa Mjini-ISAKALILO Hakina Hati(nlijaribu Kufuatilia Hati Wakanizungusha Sana Pia Nikashindwa),naomba Kwa Yeyote Au Anaejua Wapi Nitapata Mkopo Wa Milioni 1 Security Ni Hicho Kiwanja Na Ntailipa Ndani Ya Miezi 6 Nahitaji Nifanye Kilimo Eneo La Mgololo..Shamba Nimeshakodi Na Kukulima Hvyo Bado Mbegu Na Madawa Tu.Naombeni Sana Kwa Yeyote Anisaidie Ili Nijikwamue Kimaisha
0769868915
 
Samahanini kwa anayefaham hili kwa kina anifahamishe Je ni kweli Bayport wanakopesha simu za smartphone na ofisi zao ziko wapi
 
Samahanini wana jf mimi nina vifaa vya salon ya kike nina kila kitu sasa nachohitaji ni bank gani inayoweza kunipatia mkopo wa laki 5 tu nataka nikodishe flem nifungue salon problem yangu ni kodi vifaa ninavyo na wateja ninao ni mzoefu wa kazi ya salon
 
Imeongelewa mikopo toka benki na taasis za fedha, mikopo toka kampuni za simu ipo, lakini itawafilisi watu na serikali inatazama. Riba ni tishio, kwa mfano mikopo ya timiza ni 14.5% kwa siku 21! Kwa mwaka nawaachia wachumi waendelee.

m power ya voda mikopo yao ni nafuu sana ukiliganisha na airtel maana voda wao ni 9% ndo riba na unarejesha ndani ya mwezi mmoja
 
Back
Top Bottom