Taarifa za kutoroshwa Ulimboka ni kweli?

rosemarie

JF-Expert Member
Mar 22, 2011
6,887
3,412
Naomba kujua kama kuna ukweli wowote kwenye hili'

Haruni Sanchawa na Makongoro Oging' SIKU chache baada ya Mwenyekiti wa Jumuiya ya Madaktari Tanzania, Dk Steven Ulimboka (pichani), kurejea nchini akitokea Afrika Kusini kwa matibabu, sasa hajulikani alipo.

Taarifa kutoka kwa mmoja wa wanafamilia zinasema kuwa familia hiyo imekuwa ikihofia maisha ya ndugu yao mara tu baada ya kutua nchini kutoka Afrika Kusini alikokuwa akitibiwa kutokana na kutekwa na kuumizwa vibaya na hatimaye kutelekezwa katika Msitu wa Mabwepande na watu wasiojulikana, hivyo sasa wamemtorosha nyumbani kwake na kumpeleka wanakojua wao.

"Alikotoroshewa ni siri ya ndugu na jamaa zake, hawataki kabisa watu wajue," kilisema chanzo chetu cha habari.

Uchunguzi wa gazeti hili umebaini kuwa kutoroshwa kwa Dk Ulimboka kunatokana na hofu waliyokuwa nayo wanafamilia kwa madai kuwa maadui wa ndugu yao wanajua kile walichomfanyia na wanatambua kuwa maadam sasa ana akili timamu, anaweza kuwataja.
Uwazi lilifunga safari hadi Ubungo Kibangu ambako inahisiwa anaweza kupatikana Dk. Ulimboka lakini matokeo yake waandishi wetu walipofika na kuuliza wenyeji wa nyumba iliyotajwa walijibiwa kuwa hayupo na walipotaka kujua yupo wapi, watu hao walisema hawajui.

"Siyo rahisi kumuona Dk Ulimboka ndugu zangu, kila mtu hana imani na mtu anayetaka kuongea na daktari hata baadhi ya ndugu nafasi hiyo hawaipati," alisema mtu huyo ambaye hakutaka kujitambulisha jina.

Habari zaidi zilidai kuwa baada ya kurejea nchini, Dk Ulimboka alitua kwa Mchungaji Josephat Gwajima kwa ajili ya kuombewa na kumshukuru Mungu kwa madai kuwa alinusurika kifo.

Taarifa zinadai kuwa baada ya kutoka kanisani hapo alienda Bagamoyo ambapo chanzo hicho hakijui alifika huko kwa lengo gani. Waandishi wetu walikwenda kanisani lakini hakuna kiongozi aliyekuwa tayari kumzungumzia Dk Ulimboka kwa madai kuwa msemaji ni Gwajima mwenyewe.

BABA MZAZI
Wiki iliyopita baba mzazi wa Dk Ulimboka alinukuliwa na vyombo vya habari akisema kuwa hayuko tayari kuongea lolote kuhusu mwanaye na kwamba yote amemwachia Mungu.
 
lini ametoroshwa iwapo juzi tu alikuwa kanisani hapo ubungo na alitoa sadaka ya shukrani?!!..hii taarifa ya lini...
 
Safi sana. Mficheni huko awe anaandaa makala na DVDs aipatie dunia. Kila mwenye chombo cha habari mwenye mapenzi ha nchi hii arushe asiogope kufungiwa maana itakuwa imetoka from the horse's mouth.
 
Sasa maisha anayoishi Ulimboka du!! unajua ili Ulimboka awe huru anapaswa kulizungumzia hili tukio bila uoga wala kumung'unya maneno. Ili itakuwa ndio salama yake, ila kwasasa ataendelea kuishi kama kuku wa kisasa, kujificha kwingi.
 
lini ametoroshwa iwapo juzi tu alikuwa kanisani hapo ubungo na alitoa sadaka ya shukrani?!!..hii taarifa ya lini...
.

Hata hilo gazeti limesema alikuwa kanisani na kuombewa mkuu. Soma vizuri mwishoni mwa story
 
Mimi sioni tatizo kwa Dr. Ulimboka kufichama au kufichwa na wanafamilia. Tumwache apumzike kwanza. Yaliyomtokea sio madogo kiasi cha kutegemea kuwa alipotua tu angeanza hekaheka za mapambano dhidi ya watesi wake.
 
hizi taarifa hajadhibitishwa rasmi labda walio karibu na familia ya dr. ulimboka watujuze zaidi
 
Mkuu haya magazeti pendwa sio chanzo kizuri cha habari. Ndo maana yanaitwa magazeti ya udaku. mia
 
"......Mtu yeyote ambaye hatafanya kitu chochote, ataishi, hatimaye atakufa, bila kufanya kitu chochote....." hiyo nayo ya kuishi mafichoni si adhabu???? bora atoke hadharani, na aisaidie polisi katika uchunguzi wa nani walihusika, ili awe huru.
"SAIDIA POLISI IKUSAIDIE"
Tujenge imani na vyombo vyetu vya dola.
 
Back
Top Bottom