Huyu ni mzee mmoja kati ya wagonjwa wangapi wanaofikiria hivyo?. Ikiwa leo wapo Watanzania ambao wanafikiria kwa fikra zao mtu kama Lowassa ambaye miaka mitano tu iliyopita alikuwa adui mkubwa wa jamii na anayestahili kifungo cha Segelea, leo anahimizwa na kusifiwa il arudi madarakani unafikiri sisi wazima kweli?.Mkandara, kwenye taarifa ya bahari ITV 8pm yuko mzee mmoja (zaidi ya miaka 60) amevunjika mguu na alipoenda MOI hakupata matibabu kwa sababu ya mgomo. Lakini yule mzee alisema bila kumumunya maneno "madaktari wagome hadi wapate haki yao". Unaweza kuona ni jinsi gani wananchi wameamua kugharamia mabadiliko - life on the line kwa huyu mzee lakini aona bora iwe hivyo.
Na leo hii wabunge wa ccm hawako kwenye mood ya kujadili huu mgomo badala yake wamekazania kujadili JF! inasikitisha.
Kifupi mkuu wangu nimegundua jambo muhimu sana ambalo zamani nilijiaminisha kwamba vijana wasomi wa leo wanaweza kuleta mabadiliko kumbe nilikuwa najidanganya kama wadanganyika wengine. Inasikitika sana kuona Taifa langu linakoelekea lakini yanibidi kukubali matokeo kwa sababu UMOJA hautapatikana kutokana na sisi wenyewe kuupoteza UTU.