Taarifa ya Nchimbi kwa wanahabari

Steven Robert Masatu

JF-Expert Member
Aug 7, 2009
2,458
1,821
Hiyo attachement ya NCHIMBI kwa vyombo vya habari.

Hii haivurugi uchunguzi wa kamati aliyoteua?

attachment.php
 

Attachments

  • waziri.JPG
    waziri.JPG
    85.2 KB · Views: 6,803
Uchunguzi wa kamati hauna maana tena kwasababu kesi imeshafikishwa mahakamani. Kwahiyo kulizungumzia swala hilo kwa namna yoyote ikiwa ni pamoja na kamati kutoa majibu yake na kuyatangaza hadharan kabla ya hukumu ya mahakama kutolewa itakuwa ni kuingilia uhuru wa mahakama.

Serikali ni kama imeshalizika jambo hilo tayari. Inaniuma sana!
 
huyu jamaa atakuwa mgonjwa huyu..hivi anajua kweli hadhi ya uwaziri au.?
 
Nchimbi kama mnashirikiana na waandishi wa habari wangekutimua Jangwani jana. Hii ni kuonyesha eti unafanya kazi. Ungefanya jambo la msingi na tukakuona shujaa kama ungetangaza kuachia ngazi
 
Atakachoweza kujivunia katika uwaziri wake huyu jamaa ni wakati ule alipokua waziri wa michezo na utamaduni alipowapatanisha Muheshimiwa SUGU na RUGE katika ule ugonvi wao! And that is all! Apart from that ile juzi ningemuona wa maana kama angeachia ngazi mbele ya waandishi wa habari.
 
Mjadala umefungwa kwa mbinu hii ya kuwaziba mdomo watanzania throu Court
 
Nani alimtuma amlipue Daudi Mwangosi? I wish tume will come out with very positive result!
 
"Wakati mkondo wa sheria umeanza kufuatwa nawaomba wadau wote kutoa nafasi kwa utaratibu huo wa kisheria kufanya kazi"
Suala lipo mahakamani sasa ni marufuku kulijadili!:tape:
 
Kwahiyo amemuacha RPC Kamuhanga ili ashirikiane na waandishi. Kweli hapa TZ kila tusi linawezekana.
 
Safi Nchimbi waeleze hawa wasio na hiyana hawajui zuri hata kushukuru kwa hatua iliyofikiwa hongera sana kazi nzuri big upppppppppppp
 
Jamaa inasemekana anauota urais 2015 ndo maana anatafuta simpathy kwa waandishi ili awatumie kipindi hicho
 
Aisee, hili swala la marehemu Mwangosi na ubabe wa polisi litanifanya nipigwe ban...... Maana tangu jambo hili litokee sa nyingine nimekuwa napata hasira sana humu jf na kutamani sana kutukana......... nimevumilia naona uvumilivu karibu utanishinda, nitasema liwalo na liwe nimwage mitusi humu..... Mungu azidi kunipa uvumilivu.
 
Back
Top Bottom