Taarifa ya Msiba...!

PJ tunaomba more info wapi kwa FT? ibada ya mazishi itakuwa kanisa gani some of us are living in Arusha and we would like to attend. thanks
iNFO ZITAKUWA AVAILABLE.
Kwa ufupi ni kwamba marehemu atasafirishwa kuelekea Njombe Iringa!
Kwa huku Arusha wanaishi USA, na ni wazi kutakuwa na taratibu za kuuaga mwili wa marehemu kati ya Jumamosi na JUMAPILI!.
HIYO ndiyo itakuwa nafasi ya pekee kwa tulio Arusha kuagana na shemeji yetu.
Tuko pamoja.
 
Our deepest condolences to Freetown. May God rest her soul in peace.
 
Mungu wangu!nimeshtuka karibia kutoa machozi.moyo umeniuma aisee,mara ya mwisho kuonana na Freetown alinionyesha picha za familia yake wakiwa na furaha sana.nimeumia sana,na namuomba Mungu ampe FT moyo wa subra na ailaze pema roho ya marehemu .Amen
Ooooh!
Too bad!...na inasikitisha!
Basi wewe una kumbukumbu mpya zaidi ya huyu mana, na yapasa umwombee ili akapumzike mahala pa salama!
 
Dah!! Nimepata mshtuko sana, Najua Freetown yuko katika wakati mgumu sasa hivi hasa pale unapompoteza mtu wako wa karibu uliyekuwa unaishi naye ni vigumu sana lakini la zaidi ni kumshukuru Mungu na kumwomba ampumzishe mahala pema shemeji yetu nakumbuka wakati tumekuja Arusha ndipo nilifahamihana na Freetown nampa pole sana kwa msiba uliomkuta tunamwombea sana hasa katika kipindi hiki kigumu anachopitia.

BWANA ALITOA BWANA AMETWAA JINA LA BWANA LIHIMIDIWE.

TF.
 
FT Mungu akupe nguvu katika kulikabili hili wewe na binti zako wapenzi. Sisi kama binadamu hatuna namna ya kupunguza machungu yaliyomo mioyoni mwenu lakini yeye atupae pumzi atawaongoza. Mkabidhi yeye.

Pole sana
 
wakuu,

nimetaarifiwa sasa hivi kwamba mke wa member mwenzetu freetown ameaga dunia mchana huu saa7.30 kwenye hospitali ya kcmc-moshi.

freetown ni member 'legend' hapa majukwaani, na kwa wale waliofika arusha mwaka jana (27/12/2010) tulipoenda safari ya tarangire wanapata hisia zaidi juu ya kuondokewa na mkewe kwa huyu member mwenzetu, maana tulikuwa pamoja nae bega kwa bega, na alisafiri na wanae, mabinti wawili.

mipango ya mazishi bado haijawekwa wazi, na zaidi inasubiri kuwasili kwa freetown mwenyewe toka ughaibuni anakomtumikia mkoloni, na kwa taarifa nilizopewa ni kwamba anatarajiwa kuondoka huko leo usiku, na atawasili kesho alasiri, mungu akipenda.

tutajuzana zaidi kinachoendelea, kwa sasa tunachoweza kusema ni kwamba mungu ailaze pema roho ya marehemu mke wa freetown.
amen.

update 1:
freetown ameondoka usiku wa saa 7.30 mahala anapoishi kuelekea doha-qatar,ambako likuwa aondoke saa 10.00usiku waleo(11/2/2011), lakini bahati mbaya flight aliyoondoka
nayo anakoishi imechelewa kwa masaa mawili, hivyo hakuweza kuunganisha connection ya qatar-airways usiku wa leo, na hivyo atalazimika kulala hapo qatar na leo usiku ndipo atasafiri kwa shirika hilohilo na atafika dar-jnia kesho(ijumaa) saa 7.mchana, na atakuwepo uwanjani hadi saa 12.00jioni, ambapo ndio atapanda precision air kuja kia.

update 2:
mulioko dar mna nafasi kubwa ya kuonana na ft hapo jnia kesho, maana atakuwepo hapo kwa more than 4 hrs kabla ya kuja arusha, hivyo kwa watakaopenda kumtafuta tutawapa contact yake mumpate kirahisi.

update 3:
marehemu mrs ft atasafirishwa siku kati ya jmosi au j'pili kutoka arusha kuelekea njombe iringa, ambako ndiko domicile place ya couple hii...


rip,pole sna mkuu
 
Poleni sana na pole FT sana,the bible says SHUKURUNI KWA KILA JAMBO, jipe moyo Mungu atakuwa pamoja nawe
 
Pole sana FT, mwenyezi mungu akupe nguvu, ujasiri na subira katika wakati huu wa majonzi ya kuondokewa na mwenzio.
Mrs FT, RIP.
 
RIP Mrs Freetown

Pole nyingi kwako Freetown Mungu akupe uvumilivu katika kipindi hiki kigumu.
 
oooh inaumiza sana.
mungu amlaze mahali pema peponi,na pia amjalie ndugu yetu utulivu na ujasiri katika kipindi hiko kigumu.
 
Pole sana FT tunajua upo kwenye wakati mgumu sana kwa kuondokewa na mwenzi wako, Tupo pamoja na we kwenye maombi.
Ulimpenda sana lakini mwenyezi Mungu amempenda zaidi, apumzike kwa amani. Amen
 
Back
Top Bottom