Taarifa ya msiba:baba mdogo wa rafiki yetu x-pin afariki dunia

Pole sana X-pin kwa msiba uliokupata. Huyu mzee mbona mnaficha jina lake ? Juzi alipofariki mzee Bruno Mpangala , taarifa iliandikwa na watu wakajumuika kwenda nyumbani kwake msibani huko Kinyelezi; sasa huyu mzee mbona mnaficha jina lake hamtaki watu waende kwenye msiba wake sharti kwa kutuma PM?
 
Pole sana Kiongozi. Mungu awatie Nguvu woote, Wote njia yetu ni moja na kila mtu ana siku yake, Tunaposikitika kwa mwenzetu na sisi tunatafakari njia zetu.
 
Hommie Pole sana! Kama kawaida tupo pamoja kiutekelezaji zaidi

Naomba wapwa na mabinamu ambao they can make it to Tabata please kama kawaida yetu tumpe support.

Mungu ametoa na Mungu ametwaa Jina lake lihimidiwe

Amen
 
Fundi Mchundo mwenzake, nafikisha pole zangu nyingi sana kwako kwa kuondokewa na baba mlezi. Kwa maisha ya Tanzania, wengi sana tuliingizwa Dar na Shangazi, Wajomba, Kaka, Dada, baba na mama wadogo nk nk. Upande wangu mtu aliyenileta Dar nilishampoteza siku nyingi na ninakuwa mmoja ya watu ambao wanaelewa hasa hali uliyopo.

Mungu ampe mapumziko mema milele na nyie wafiwa awape nguvu katika kipindi hiki kigumu. Bwana katoa, bwana kachukua, jina lake litimizwe, Amen.
 
Poleni wote, X-pin, familia yako, wana JF ndugu, jamaa na marafiki wote wa marehemu!

DN
 
Msiba unakugusa kwa kiasi kilekile ambacho marehemu aligusa maisha yako...
Pole Xpin...pole wafiwa wote.
Tuko pamoja.
 
pole sana mkuu kwa msiba huu mzito mungu akupe nguvu ktk kipindi hiki kigumu
 
Pole sana X-pin na mwenyezi mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi, amen.
 
Kaka xpin
polen sana na familia kwa jumla ;ni huzuni kubwa kufiwa na mtu aliekujali aliekutunza
anaejuaa thaman yako ukiacha mod...mungu akupe moyo wa uvumilivu nr tuko pamoja
tuzidi kumwombea..bwana ametoa bwana ametwaa..
Mungu amrehemu
tuko pamoja kaka
 
Watanzania msiache kuwapa pole pia familia ya mc chi chi aliefariki leo mchana
mungu amlaze pema peponi
 
sorry for the loss big brother!!!

RIP baba Iribbini
 
jamani kwa sasa ndio tunaelekea makaburini kwa ajili ya kumpumzisha mzee wetu.....

tunazika kinondoni hapo

kuna foleni kubwa sana kutokea tabata

MUBARIKIWE SANA WAKUU
 
Back
Top Bottom