EMT
Platinum Member
- Jan 13, 2010
- 14,483
- 15,308
Kwa mujibu wa sensa iliyofanywa mwezi Oktoba na Wizara ya Maliasili na Utalii, kwa sasa Selous-Mikumi ina tembo wapatao 13,084 na Ruaha–Rungwa tembo wapatao 20,090. Takwimu hizi zinaonesha kupungua kwa idadi ya tembo na hasa Selous-Mikumi ikilinganishwa na Sensa za awali.
Mwaka 1976 Selous–Mikumi ilikuwa na tembo 109,419. Idadi hii ilipungua kufikia 22,208 mwaka 1991 kutokana na wimbi la ujangili uliokuwepo katika kipindi cha mwaka 1984 -1989.
Hata hivyo, idadi hiyo iliongezeka na kufikia 70,406 mwaka 2006 baada ya Operesheni Uhai iliyofanyika mwaka 1989 na 1990 na juhudi za kimataifa za uhifadhi ikiwemo kusitisha biashara ya meno ya tembo. Aidha, idadi ya tembo nchini ilipungua hadi kufikia jumla ya tembo 38,975 mwaka 2009 na kuendelea kupungua hadi kufikia tembo 13,084 hivi sasa.
Hali kama hiyo inaonekana pia Ruaha-Rungwa ambapo sensa ya mwaka 1990 ilionesha kuwa na tembo 11,712 kutokana na wimbi la ujangili. Idadi hii iliongezeka na kufikia 35,461 mwaka 2006. Hata hivyo, idadi hiyo imepungua na kubakia tembo 20,090 hivi sasa.
Kwa matokeo haya inaonyesha kuwa idadi ya tembo Selous-Mikumi imepungua kwa asilimia 66 ikilinganishwa na idadi ya mwaka 2009 ambapo kulikuwa na jumla ya tembo 38,975. na huko Ruaha–Rungwa tembo wamepungua kwa asilimia 36.5 ikilinganishwa na idadi ya mwaka 2009 ambapo kulikuwa na jumla ya tembo wapatao 31,625.
Kupungua huku kunathibitishwa na idadi ya mizoga ya tembo iliyohesabiwa wakati wa zoezi la sensa. Jumla ya mizoga 6,516 na 3,496 ilihesabiwa katika mifumo ikolojia ya Selous-Mikumi na Ruaha–Rungwa. Katika zoezi hilo Wizara ilitumia vigezo vya uwiano wa mizoga na tembo hai waliohesabiwa (carcass ratio) kubaini vyanzo vya vifo hivyo. Katika hali ya kawaida, uwiano wa asilimia 7 – 8 unaashiria vifo vya asili kama vile ugonjwa na uzee.
Zaidi ya asilimia hiyo inaashiria vifo visivyo vya asili. Sensa iliyofanyika mwaka huu imeonesha uwiano wa asilimia 30 huko Selous-Mikumi na asilimia 14.6 kwa Ruaha–Rungwa. Kwa mujibu wa matokeo hayo, idadi kubwa ya vifo vya tembo vimetokana na vifo visivyo vya asili.
Chanzo: Kutoka Wizara husika.