Taarifa ya Lissu kwa vyombo vya habari kuhusu Spika wa Bunge

Yaani hata kama alielekezwa kuwa atatakiwa kulinda maslahi ya magamba, ameshindwa kutumia akili maana analinda hata pasipostahili!
 
CCM kama wanataka kurudisha umma kuwa upande wao huyu mama naye ni gamba. Kitu cha kujiuliza ni kwa nini Samuel Sitta ambaye ni CCM alipata heshima kubwa sana kutoka kwa wananchi kwa jinsi alivyolifanya bunge kuwa la kidemokrasia, haki na uwazi bila ya kuangalia chama?.

The more huyu mama anavyozidi kuwanyanyasa wapinzani bungeni the more popular wapinzani wanavyokuwa on public na the more CCM inavyozidi kuchukiwa na wananchi kwa kuendesha nchi kibabe.

Uwezo wa huyu mama ni mdogo sana katika kuendesha bunge la vyama vingi la karne ya 21 yenye watu wanaojua kuchambua pumba na mchele. Wabunge wa CCM kama wanafikiria huyu mama hawasaidii bali anawadidimiza wote kuonekana useless. Nina amini kuna wabunge makini sana wa CCM ila wanafunikwa na magamba ya huyu mama, anayedhani bado tupo enzi za mfumo wa chama kimoja.
 
Lissu kama mwanasheria anashangaza sana. Sasa mara aseme yeye yuko mahakamani kwa kesi inayohusu hao waliouiliwa Nyamongo halafu alaume Spika hakutenda haki kuzuwia yasiongelewe. Hivi ananini huyu? Ili mradi alalamike tu?

SI asuse kama anaona hatendewi haki? Asuse na kwenda mahakamani pia (Spika sikasema yuko nje kwa dhamana? Au alidanganya hapo Spika). Lissu susa kwenda mahakamani halafu muulize Mbowe zile siku mbili alilaa kitandani? Sakafuni au juu ya desk? Alipokaidi kwenda mahakamani?

:wof: shii
 
Kutokana na Spika wa bunge kuliendesha bunge kwa upendeleo Mnadhimu Mkuu wa Kambi ya Upinzani Bungeni Mh. Tundu Lissu amesema anaandaa malalamiko rasmi atakayoyafikisha mbele ya Kamati ya Kanuni za Kudumu za Bunge.
" Ili kuepuka hili, inabidi tumpeleke Mheshimiwa Spika kwenye Kamati ya Kanuni za Kudumu za Bunge ili uamuzi wake ukajadiliwe na kutolewa maamuzi ya haki. Kazi ya kuandaa malalamiko hayo itakamilika baada ya muda mfupi kwani vielelezo vyote muhimu tayari vimekwishapatikana.”
--------------------------------------------------------------
Tundu A.M. Lissu (MB.)MNADHIMU MKUU, KAMBI RASMI YA UPINZANI
 
Alipoombwa mwongozo wake kutokana na ukweli kwamba hakuna kesi hata moja ambayo imefunguliwa au inayoendelea katika mahakama yoyote ya Tanzania inayohusu mauaji ya wananchi wa Nyamongo au yanayowahusu polisi wanaohusika na mauaji hayo, Spika Anna Makinda alidai kwamba wauliza maswali wenyewe walikuwa wanakabiliwa na mashtaka ya jinai katika Mahakama ya Wilaya ya Tarime yanayotokana na matukio ya mauaji ya wananchi watano yaliyofanywa na polisi katika eneo la Mgodi wa North Mara tarehe 16 Mei mwaka huu na kwa hiyo hawakupaswa kuuliza maswali yao.

Huyu ni SPIKA wa wote au ni wa CCM?
- Kwa maneno yake na maamuzi yake cha kwanza kabisa AOMBE Msamaha kwa kuongea CRAP.

Huyu si ndio pia alisema MAFISADI hawajui na maana yake kwake ni wale wanaochukua wake za watu! Mijitu mingine Bwana, kwa kuongea pumba. Hata ukiipa majukumu ya aina gani. Watu wanahujuwa, na mafisadi wanaitafuna nchi na yeye analeta ushoga wa kipumbavu.

Anayosema Mh. Lisu ni sawa lakini atofautishe uanaharakati na ubunge, kwa taarifa hii amewapa nafasi ya kujipanga wajibu mapigo. Laiti kama angeyatoa bungeni na kuwashangaza ingelipa.
 
Kwa raha zake Makinda ata mkimtoa keshaweka historia ya kuwa mwanamke wa kwanza kuwa speaker!
Kwake yeye mission accomplished so tutabaki tunaumiza kichwa
 
Huyu kikwonge ameishia kukumbatia chama..nilijua mambo kama haya yatatokea.
 
Lissu kama mwanasheria anashangaza sana. Sasa mara aseme yeye yuko mahakamani kwa kesi inayohusu hao waliouiliwa Nyamongo halafu alaume Spika hakutenda haki kuzuwia yasiongelewe. Hivi ananini huyu? Ili mradi alalamike tu?

SI asuse kama anaona hatendewi haki? Asuse na kwenda mahakamani pia (Spika sikasema yuko nje kwa dhamana? Au alidanganya hapo Spika). Lissu susa kwenda mahakamani halafu muulize Mbowe zile siku mbili alilaa kitandani? Sakafuni au juu ya desk? Alipokaidi kwenda mahakamani?
Nimeamini kweli wewe ni Faza Fox.
 
Fox !bila shaka unaugonjwa wa kutoelewa hata ukieleweshwa!vipi shule ya kata imekuharibu!jaribu kuchangia kitu unachoelewa kama hujui kitu kaa kimya kuliko kuleta upupu humu
 
Lissu kama mwanasheria anashangaza sana. Sasa mara aseme yeye yuko mahakamani kwa kesi inayohusu hao waliouiliwa Nyamongo halafu alaume Spika hakutenda haki kuzuwia yasiongelewe. Hivi ananini huyu? Ili mradi alalamike tu?

SI asuse kama anaona hatendewi haki? Asuse na kwenda mahakamani pia (Spika sikasema yuko nje kwa dhamana? Au alidanganya hapo Spika). Lissu susa kwenda mahakamani halafu muulize Mbowe zile siku mbili alilaa kitandani? Sakafuni au juu ya desk? Alipokaidi kwenda mahakamani?

Makinda mzuri akiwakandamiza chama cha upinzani, "akiwaponda" wa Kariakoo unakoishi wewe ni mbaya asiyejua vibaya! Double standards!
 
si ndiye spika huyu huyu aliyemruhusu waziri mkuu azungumzie issue ya ARUSHA huku akijua swala zima hilo liko mahakamani
ambapo waziri mkuu akasimama na kuzungumza uongo mtupu inakuwaje leo akatae issue isizungumzwe wakati mazingira ni yale
yale.
 
barua haina hata paragraph jamani??? aisee.......aniwei, spika Makinda ni reflection ya uongozi wa CCM kwani huyo ndiye waliyemuona cream, she is the best speaker CCM can provide at the moment, tutafanyaje sasa wakati Mama Makinda uwezo wake ndio huoKwa CCM yeye ni cream of the crop!! aisee.....
Duh! Mkuu, yaani wewe ubongo wako hauelewi mpaka kuwe na paragraphy? Hahahahaaa. Angalia content bwana. Acha uzuzu!
 
mimi ninashangaa sana kuona wabunge wa ccm wanaangalia tu na kuwaachia wapinzani peke yake kupigania masuala ya kitaifa na maendeleo ya waTanzania. Inafika mahali ninashindwa kuelewa, hivi hao jamaa wameenda bungeni kulinda maovu au kutetea wananchi? Yaani katika wabunge wa ccm hakuna hata mmoja anayemwogopa Mungu? mbona misikiti na makanisa yanajaa sana? Hawa watu wana mawe vichwani mwao badala ya ubongo? Vitu ambavyo hata mtoto wa mwenye umri chini ya miaka mitano anaviona wao hawavioni! Inasikitisha sana!!
 
She is old fashined, kama aliwekwa na akina Rostam Aziz naye ni gamba hivyo CCM iondokane naye, so incompetent!, Shame on her!
 
Lissu kama mwanasheria anashangaza sana. Sasa mara aseme yeye yuko mahakamani kwa kesi inayohusu hao waliouiliwa Nyamongo halafu alaume Spika hakutenda haki kuzuwia yasiongelewe. Hivi ananini huyu? Ili mradi alalamike tu?

SI asuse kama anaona hatendewi haki? Asuse na kwenda mahakamani pia (Spika sikasema yuko nje kwa dhamana? Au alidanganya hapo Spika). Lissu susa kwenda mahakamani halafu muulize Mbowe zile siku mbili alilaa kitandani? Sakafuni au juu ya desk? Alipokaidi kwenda mahakamani?

Na wewe hoja zako zinafanana sana na mwana-Magamba mwenzako Spika Makinda, hebu rudia hoja hii hapa ya Lissu na jinsi Magamba mwenzako Makinda alivyojibu:

Hoja ya Lissu: Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni imeelezea kusikitishwa na namna ambavyo Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano amekuwa akishughulikia mijadala ya masuala muhimu kwa umma na ambayo yanaelekea kuibua uozo katika utendaji wa Serikali na watendaji wake wakuu. Hii inafuatia uamuzi wa Spika kukataa maswali aliyoulizwa Waziri Mkuu Mizengo Pinda kuhusu mauaji ya wananchi wengi wa vijiji vinavyozunguka Mgodi wa Dhahabu wa North Mara katika eneo la Nyamongo wilayani Tarime yaliyofanywa na Jeshi la Polisi, Kanda Maalum ya Polisi ya Tarime na Rorya kwa vipindi tofauti tangu mwaka 2008.

Jibu la Anna Makinda: Hata hivyo, katika hatua ya kushangaza, Spika wa Bunge alikataza maswali hayo kujibiwa kwa hoja kwamba yalikuwa yanahusu mambo ambayo tayari yako mahakamani na kwa hiyo kuyajadili Bungeni itakuwa sawa na kuingilia uhuru na mamlaka ya Mahakama kinyume na kanuni 64(1)(c) ya Kanuni za Kudumu za Bunge, 2007.

Hoja ya Lissu: Alipoombwa mwongozo wake kutokana na ukweli kwamba hakuna kesi hata moja ambayo imefunguliwa au inayoendelea katika mahakama yoyote ya Tanzania inayohusu mauaji ya wananchi wa Nyamongo au yanayowahusu polisi wanaohusika na mauaji hayo!
Jibu la Spika Makinda: Spika Anna Makinda alidai kwamba wauliza maswali wenyewe walikuwa wanakabiliwa na mashtaka ya jinai katika Mahakama ya Wilaya ya Tarime yanayotokana na matukio ya mauaji ya wananchi watano yaliyofanywa na polisi katika eneo la Mgodi wa North Mara tarehe 16 Mei mwaka huu na kwa hiyo hawakupaswa kuuliza maswali yao.

Hoja ya Lissu:Akizungumzia uamuzi huo wa Spika Makinda, Mbunge Lissu - ambaye pia ni Mnadhimu Mkuu wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni - alimtuhumu Spika Makinda kwa kumkingia kifua Waziri Mkuu na kukiuka Kanuni za Kudumu za Bunge. “Mimi sijashtakiwa mahakamani kwa kosa lolote linalohusu mauaji ya wananchi wa Nyamongo, Tarime na wala kesi yangu katika Mahakama ya Wilaya ya Tarime haiuhusu matukio ya Nyamongo”, Lissu alisema. Aliongeza kwamba: “Wakati mauaji ya wananchi wa Nyamongo yalifanywa na Jeshi la Polisi tarehe 16 Mei, mimi na wenzangu wengine saba tumeshtakiwa kwa madai ya kuingia kijinai katika eneo la kuhifadhia maiti katika Hospitali ya Wilaya ya Tarime; kwa kufanya mkusanyo haramu katika eneo hilo; na kwa kuwazuia mganga wa Hospitali hiyo na askari polisi kufanya uchunguzi wa miili ya marehemu Emmanuel Magige, Chacha Ngoka, Chawali Bhoke na Mwikwabe Marwa waliouawa na Jeshi la Polisi. Makosa yote matatu yanadaiwa kutokea mnamo majira ya saa nne usiku wa tarehe 23 Mei 2011Kuhusiana na Mbunge Matiko, Lissu alidai kwamba Mbunge huyo wa Viti Maalum hakabiliwi na mashtaka yoyote mahakamani kwa jambo au kosa lolote lile. “Inaelekea Spika wa Bunge alitoa uamuzi wake huo bila hata kuuliza au kupewa taarifa sahihi kuhusu masuala ya mauaji ya Tarime na kesi iliyofunguliwa dhidi yangu na wenzangu.

All right, FF, wewe kwa akili yako unafikiri Mheshimiwa Lissu ameshtakiwa "kwa mauaji?" Na kama angeshtakiwa kwa mauaji, Je, masuala yaliyotokea mwaka 2008 yanamhusishaje Lissu au kila jambo la Nyamongo linamhusu Lissu?
 
Anayosema Mh. Lisu ni sawa lakini atofautishe uanaharakati na ubunge, kwa taarifa hii amewapa nafasi ya kujipanga wajibu mapigo. Laiti kama angeyatoa bungeni na kuwashangaza ingelipa.

Magamba wa kujipanga na kujibu hoja kama hizo ni nani?

Angalia hoja zao!

Lissu kama mwanasheria anashangaza sana. Sasa mara aseme yeye yuko mahakamani kwa kesi inayohusu hao waliouiliwa Nyamongo halafu alaume Spika hakutenda haki kuzuwia yasiongelewe. Hivi ananini huyu? Ili mradi alalamike tu?

SI asuse kama anaona hatendewi haki? Asuse na kwenda mahakamani pia (Spika sikasema yuko nje kwa dhamana? Au alidanganya hapo Spika). Lissu susa kwenda mahakamani halafu muulize Mbowe zile siku mbili alilaa kitandani? Sakafuni au juu ya desk? Alipokaidi kwenda mahakamani?

Hata Bungeni mambo ni hayohayo!
 
Kuongoza bunge si kazi rahisi. Na tokea mwanzo uchaguzi wa Anna Makinda kuwa spika ulikuwa na walakini ila ilijulikana wazi kwamba amewekwa kwa maslahi yao binafsi na iwe rahisi kumpelekapeleka watakavyo. Ila sasa CHADEMA watamfundisha adabu inabidi wamuwashie moto mpaka akione hicho kiti kichungu kwa hoja asizoweza zijibu.
 
Back
Top Bottom