Taarifa ya kifo cha wazazi wangu

PMNBuko

JF-Expert Member
Dec 27, 2010
967
154
Ndugu wa JF, Salaam,

Nasikitika kuwafahamisha kuwa wazazi wangu usiku wa kuamkia tarehe 2 May 2011 walivamiwa na majambazi wasiojulikana WAKAWAUA WAZAZI wangu wote kwa kuwachoma visu huko Muganza, Rulenge, Ngara.

Nimasikitiko makubwa sana.
 
Pole sana mkuu, Ni tukio la kusikitisha sana, tuko pamoja, Mungu akutie Nguvu
RIP Wazazi.
 
Innalillah wainailaih rajiuun, POLE SANA KWA JANGA ZITO LA MSIBA
 
Pole sana mkuu!
Mungu awatie nguvu, tupo pamoja na nakutakia maandalizi katika kuwapeleka na kuwalaza kwenye nyumba zao za milele.
Bwana alitoa na Bwana alitwaa jina lake lihimidiwe.
Amen!
 
Inasikitisha sana. jamani ukatili huu mpaka lini?
Mungu akupe roho ya uvumilivu kwani inuma sana.
Pole sana
 
Pole sana kwa yaliyokufika, Mungu atatoa haki kwa kila mmoja kwa matendo yake,
Mungu azilaze roho za wazazi wako mahala pema peponi.
 
Habari za kuhuzunisha sana hizi. Pole sana Mkuu. Mungu akupe moyo wa uvumilivu na awalaze mahali pema peponi wazee wetu.

Na hayo majambazi Mungu na ayalaani.
 
POLE SANA NDG..BWANA AMETOA NA BWANA AMETWAA,JINA LAKE LIHIMIDIWE!Wasamehe hao majambazi waliotenda hayo,....Mungu atawapunish mwenyewe
 
Ndugu wa JF, Salaam,

Nasikitika kuwafahamisha kuwa wazazi wangu usiku wa kuamkia tarehe 2 May 2011 walivamiwa na majambazi wasiojulikana WAKAWAUA WAZAZI wangu wote kwa kuwachoma visu huko Muganza, Rulenge, Ngara.

Nimasikitiko makubwa sana.

Pole sana kaka, Mungu akupe amani na ulinzi wake, pia akujaze faraja yake iliyo kuu
 
Dah... this is really a sad news!!

Pole sana, nakuomba tu shikamana, omba nguvu za Mungu na support zote za duniani ili uwasamehe na kuwasahau hao wauwaji... lakini usisahau tukio wala wazazi

Hatujui tumeandikiwa nini, lakini habari kama hizi ni za kutia simanzi sana, sana, sana, sana tu!!
 
Lo hi habari ya kusikitisha sana tena sana. hawa warundi watatumaliza. Mingu akutie nguvu. RIP wazazi
 
Ndugu wa JF, Salaam,

Nasikitika kuwafahamisha kuwa wazazi wangu usiku wa kuamkia tarehe 2 May 2011 walivamiwa na majambazi wasiojulikana WAKAWAUA WAZAZI wangu wote kwa kuwachoma visu huko Muganza, Rulenge, Ngara.

Nimasikitiko makubwa sana.

pole sana bwana ametoa na bwana ametwaa
 
Pole sana Mkuu, mtegemee Mungu utashinda kwa sababu yeye atakupa nguvu ya kushinda maumivu na majaribu yote ya kipindi hiki. Inaumiza sana kufiwa na mzazi, achilia mbali wazazi wote wawili kwa mara moja, lakini Mungu atakuvusha
 
Pole sana mkuu! Mungu awape nguvu wewe na ndugu zako kukabiliana na msiba huo mzito.

Majambazi ni kero sana!
 
Back
Top Bottom