Dkt. Mwakyembe: Nimekerwa sana na msimamo wa Jeshi la Polisi juu ya afya yangu

Hii nchi iko corrupted haki imekuwa vigumu kupatikana. Yaani inasikitisha kuona mtu anatoa taarifa kuwa kuna genge linataka kuondoa uhai wake halafu polisi wanasema leta ushahidi! kweli polisi imekuwa mahakama.
 
naona hili jeshi la polisi limekosa uelekeo, kwa kutetea haki za mafisadi wachache
Si kukosa uelekeo.
Wako kwenye njia sahihi.
Kama wabeba mitutu wanahakikisha nchi inaliwa bila hata sauti kutoka.
 
Yaani aliyembambikia mtoto wa Mengi madawa ndo kapewa rungu la kuchunguza tuhuma za mwakyembe hii ni sawa na fisi kupewa ulinzi wa bucha ya nyama au kima shamba la mahindi

Ametukumbusha ile issue ya Mengi!hivi mbwembwe zote zile kwenye vyombo vya habari ziliishia wapi?
 
Vita imeanza ndani ya ccm,ndani ya nchi.......Je watamwacha hai Mwakyembe bila kuitoa roho yake...time will tell
 
Mwakyembe umerogwa tu? Hakuna ushahidi wa maana unaonyesha umekuwa poisoned ! Maelezo yako marefu hayathibiyishi lolote kuhusu sumu! Hivyo vichocheo kwenye bone marrow ni abnormalities za kawaida katika mwili wa binadamu!
 
Mwakyembe,
Style yako nimeipenda hadi sasa, kukaa kimya hadi taarifa ya Apollo itolewe,
Hawa Polisi naona hawakusoma huu mchezo ndio maana Manumba amekurupuka vibaya,
Endelea kusubiri hiyo taarifa ili itakapotolewa ukweli wote utajulikana,
Walidhani labda umekaa kimya unawaogopa labda, kumbe ni mbinu ya mapambano!
 
Unapoona vyombo vya usalama vinacheza na maisha ya raia wake ujue nchi imefika mahali pabaya sana ni suala la muda tu kabla wananchi hawajafikia hatua ya kudai haki zao.Tanzania kupitia bunge waunde tume yenye lengo la kulifumua jeshi la polisi na kuliunda upya ili liweze kututendea haki waTanzania.Ni aibu kubwa viongozi wakuu wa jeshi la polisi kukubali kutumia kijinga na wanasiasa ambao wana laana ya waTanzania.

Ni matumani yangu viongozi wa dini,asasi za kiraia watapaza sauti zao ili wale wote waliohusika kwa namna moja au nyingine na uovu huu wanafikishwa mahakamani haraka bila kuchelewa.
 
Mwakyembe ni tatizo kubwa zaidi ya hao Polisi anaowatuhumu. Kumbe anayo taarifa ya awali ya ugonjwa wake, kama mwanasheria ameshindwa nini kuitisha uchunguzi binafsi wa jinai kuhusu tatizo lake? Hata sasa baada ya Polisi kuonesha "udhaifu" katika uchunguzi wao, kwanini Mwakyembe asiombe msaada wa wataalamu wa nje waliobobea katika upelelezi wafanye uchunguzi upya? Anaogopa nini?
Siwapendi watu walalamishi, lakini huyu amenikera zaidi na ukiwa makini hata faida ya kuwa msomi haionekani!

...tunakoelekea sasa tutegemee kuiona ripoti ya ugonjwa wake kwenye magazeti, kitu ambacho si kizuri sana!

Mkuu, hapo kwenye nyekundu panahusika. Kama alivyosema Mwakyembe, na sio kwa sababu kasema tu bali ndivyo ilivyo kule watu wanakojua dhamana zao, wajibu wa polisi kama walinzi wa raia na mali zao, ni kutafuta ushahidi na wala sio kusubiri kupelekewa ushahidi. Kama unalikataa hilo, sitotafautisha kuwaza kwako na hili jeshi letu "tukufu".

Mwakyembe kama raia wa nchi, kama ulivyo wewe, mimi na wengineo, tungetegemea kupata ulinzi kutoka kwa polisi ambao Watanzania wote tunawalipa mishahara yao "in exchange of their duties and responsibilities". Mwakyembe kama raia na mwanasheria, pamoja na kuwa na taarifa za awali za ugonjwa wake, hana wajibu wa kuomba msaada wa wataalamu wa nje kufanya uchunguzi, kwani ni dhahiri kuwa hata baada ya yote hayo kukamilika, aende kushitaki wapi katika mfumo huu uliooza?

Tusimwone Mwakyembe tu kuwa ni msomi, tuwaone mamilioni ya Watanzania ambao si wasomi, si manaibu mawaziri, si wabunge, si matajiri...hawa waende wapi? Unataka kusema kuwa ili kutetea na kupata haki yako nchi lazima uwe msomi?

Maswali ni mengi lakini hakuna jawabu? Ikiwa Mkuu unazo, tuwekee hapa ili hata "muathirika wa mabomu ya Mbagala na Gongolamboto, mafuriko, giza la kudumu, mgomo wa madaktari..." waelewe waende wapi wakafanye upelelei ili kupata haki zao.
 
Mwakyembe ni tatizo kubwa zaidi ya hao Polisi anaowatuhumu. Kumbe anayo taarifa ya awali ya ugonjwa wake, kama mwanasheria ameshindwa nini kuitisha uchunguzi binafsi wa jinai kuhusu tatizo lake? Hata sasa baada ya Polisi kuonesha "udhaifu" katika uchunguzi wao, kwanini Mwakyembe asiombe msaada wa wataalamu wa nje waliobobea katika upelelezi wafanye uchunguzi upya? Anaogopa nini?


Siwapendi watu walalamishi, lakini huyu amenikera zaidi na ukiwa makini hata faida ya kuwa msomi haionekani!

...tunakoelekea sasa tutegemee kuiona ripoti ya ugonjwa wake kwenye magazeti, kitu ambacho si kizuri sana!

Wewe bwana umesoma vema hii habari? Mwakyembe bado yupo kwenye uchunguzi na anaendelea na matibabu, uchunguzi ukishakamilika ataongea nini kinamsibu, sio akurupuke tu kama walivyokurupuka hao polisi, na sijui wanam cover nani hapo. MWakyembe alishasema akitoka India mara ya pili atazungumzia kinacho msibu.
 
mnamuua mtu hamsemi ukweli mnataka atulie duuu hiii nchi raisi sana kuiongoza aiseee!

Mkuu nchi sasa ina run under the 'LAW OF THE JUNGLE - STRUGGLE FOR EXISTENCE ASSURES SURVIVAL OF THE FITTEST'

Ukiangalia kuanzia taarifa ya IGP kuhusu wizi wa EPA kuwa 'NCHI ITAYUMBA' wezi halisi wakikamatwa mpaka kwenye issue za uhalifu. Inaonesha kuwa kila mtu sasa anaogopa na kuhofia maisha yake. IGP anaogopa kuagiza uchunguzi wa suala la mwakyembe kwa kuhofia na yeye atakuwa target, JK anaogopa kuagiza kwa kuhofia yaleyale na Manumba nae anakubali kutoa taarifa za uwongo ili mradi tu aonekane haingilii masilahi ya kundi la mafia waliomuwekea sumu Mwakyembe. Kweli tunahitaji katiba ambayo itampunguzia nguvu rais na kuweka kila kitu mikononi mwa wananchi. Hii itapunguza woga. Ukiangalia historia ya vifo vy utata vya waliokuwa WAKEMIA WAKUU - Dr V Fupi(RIP) na Dr Ernest Mashimba(RIP). Utaona kuwa nchi hii inatawaliwa na kundi la uhalifu wa hali ya juu na viongozi tulio nao ni vivuli tu na hawana ubavu wa kupambana na hawa jamaa. Kazi ya Manumba ilikuwa ni kupambana na kundi hilo, huwezi kukubali kuwa Generali jeshini halafu ukawa unaogopa kifo cha risasi - ukiwa hivyo unakuwa Coward. Matamshi ya Manumba ni sawa na ' waiving of white flag' to criminals afraiding to be their target.

NAFIKIRI JESHI LA POLISI LIVUNJWE TUWAKABIDHI KAZI HII JWTZ WALAU KWA MIAKA MITANO KUPAMBANA NA VITA DHIDI YA KUNDI HILI. TENA KUMUWEKA NA JK KWENYE NAFASI SALAMA ILI NAE ASIOGOPE UPELEKWE MUSWADA BUNGENI WA KUTOA MADARAKA HAYO RASMI ILI IWE NI KAZI YA WANANCHI NA SI YA MTU MMOJA.
 
Back
Top Bottom