Taarifa ya Afisa Uhusiano wa hospitali ya Muhimbili 03/07/2012

Kiganyi

JF-Expert Member
Apr 30, 2012
1,242
765
220px-Coat_of_arms_of_Tanzania.svg.png

WIZARA YA AFYA NA USTAWI WA JAMII INAWATANGAZIA MADAKTARI WOTE WANAOFANYA MAFUNZO KWA VITENDO (INTERNS), WALIOPEWA BARUA ZA KURUDISHWA KWA KATIBU MKUU WIZARA YA AFYA NA USTAWI WA JAMII, WANATAKIWA KURIPOTI MAKAO MAKUU YA WIZARA YA AFYA NA USTAWI WA JAMII IFIKAPO SIKU YA IJUMAA TAREHE 6 JULAI, 2012.

IMETOLEWA NA:

KITENGO CHA MAWASILIANO YA SERIKALI

3/07/2012

Taarifa ya Afisa Uhusiano wa hospitali ya Muhimbili kuhusu hali ya huduma ilivyo leo

03/07/2012

Taarifa niliyopata kutoka kwenye Kurugenzi ya Tiba, Kurugenzi ya Upasuaji, Kurugenzi ya Tiba Shirikishi na Kurugenzi ya Uuguzi ni kama ifuatavyo;

Kurugenzi ya Tiba: Huduma zimeendelea kutolewa kwa kiwango cha kati wagonjwa ni wachache wanaokuja kutibiwa.

Idara ya Tiba, Madaktari Bingwa wote na Registrar wote wamefika kazini na wanafanya kazi. Interns 11 wamefanya kazi. Major ward round zimefanyika. Kliniki zote za leo zimeendelea kufanya kazi pia cliniki za mchana zitafanyika.

Idara ya watoto, Madaktari Bingwa wote wapo na wanafanya kazi wapo wadini wanaona wagonjwa. Changamoto ni kwamba inabidi pia wafanye kliniki za wagonjwa wa nje na wanajitahidi kufanya hivyo.

Idara ya magonjwa ya nje.
Registrars na Daktari Bingwa wote wapo na wanafanya kazi.

Idara ya magonjwa ya afya ya akili
, Madaktari Bingwa wote wamefika kazini . Bada ya wagonjwa wote kupelekwa wodini, walionwa na madaktari. Wagonjwa katika kitengo hiki ni wengi ukilinganisha na idadi ya madaktari bingwa, lakini kliniki zimeendelea kufanyika kwa kiwango cha kati. Kiliniki ya wagonjwa wajidunga imefanyika.

Idara ya magonjwa ya dharura
, Registrar wote wamesaini lakini wliofanya kazi ni wawili tu. Daktari Bingwa yupo na anafanya kazi.

Idara ya mazoezi ya viungo
, Wafanyakazi wote wapo na wanafanya kazi.

Kurugenzi ya Upasuaji:
Huduma za upasuaji zinafanyika lakini siyo sawa na jinsi zilivyokuwa zinafanyika kabla ya mgomo kwani wagonjwa ni wachache kwenye baadhi ya kliniki na baadhi ya kliniki wagonjwa wanakuwa wengi. Wagonjwa wa upasuaji walioko wodini wanaonwa japo ni wachache ukilinganisha na hali ilivyokuwa. Baadhi ya huduma za upasuaji (operations) zimefanyika ingawa wagonjwa ni wachache kwa vile idadi ya wagonjwa wanaokuja kliniki au waliolazwa kwa ajili ya upasuaji ni wachache.

Huduma za Tiba Shirikishi: Vipimo vya maabara na vile vya uchunguzi wa radiolojia vinaendelea kufanyika kama kawaida ingawa idadi ya vipimo vimepungua ukilinganisha na kabla ya mgomo. Idara ya famasia pia inafanya kazi kama kawaida. Idadi ya wagonjwa wanaoandikiwa dawa ilipungua ukilinganisha na kabla ya mgomo.

Kurugenzi ya Uuguzi
Huduma za uuguzi zimeendelea kutolewa kwa kiwango cha kawaida.

Imetolewa na;
Aminiel Buberwa Aligaesha

Afisa Uhusiano Mwandamizi
Julai 3, 2012
 
[h=2]Taarifa ya Afisa Uhusiano wa hospitali ya Muhimbili kuhusu hali ya huduma ilivyo leo[/h]03/07/2012

Hahahaaaa
Hawa toka jana wametungiwa cha kutangaza, nadhani wanatangaza at gunpoint.
Napatwa na kicheko miye!
Wanawataka ma-interns wa nini?
Leo wanaonekana dili eeh?
Haya bana! Werevu mwingi mbele giza.
 
WIZARA YA AFYA NA USTAWI WA JAMII INAWATANGAZIA MADAKTARI WOTE WANAOFANYA MAFUNZO KWA VITENDO (INTERNS), WALIOPEWA BARUA ZA KURUDISHWA KWA KATIBU MKUU WIZARA YA AFYA NA USTAWI WA JAMII, WANATAKIWA KURIPOTI MAKAO MAKUU YA WIZARA YA AFYA NA USTAWI WA JAMII IFIKAPO SIKU YA IJUMAA TAREHE 6 JULAI, 2012.

IMETOLEWA NA:

KITENGO CHA MAWASILIANO YA SERIKALI

3/07/2012

Kitengo cha mawasiliano ya serikali kiko wapi, na kinaongozwa na nani?
 
Aminieli ni sawa na Tarek Aziz waziri mmoja enzi za Sadam Hussein. Waliopo MNH wanajua kinachoendelea yeye anajitahidi kutoa taarifa za kuhadaa umma kuwa kila kitu kipo shwari ndani ya hospitali.
 
Kumbe wameshatambua kwamba uwajibikaji ni kitu mujimu na hakuna haki bila wajibu.
 
Jana niliwaambia hivi:

Usanii mtupu, porojo nyiiiingi, madai yenyewe haya:

Hivyo basi Madaktari Bingwa tumeamua kuacha kufanya kazi ambayo haiendani na kiapo cha Madaktari mpaka hapo Serikali itakapokubali kurejesha interns wote na kufungua meza ya Majadiliano yenye nia ya dhati ya kumaliza mgogoro.
Madaktari bingwa wajanja sana, maana hao interns na registrars wameshatangaza kurudi kazini na wamesema kwa sasa wataendelea na majadiliano na wanamheshim Rais na hawataki kuingia kwenye ubishi na Rais.

Madaktari Bingwa wanatumia uzoefu wasije kuonekana wao hawakuwaunga mkono hawa madaktari uchwara walioamua kurudi kazini leo.

Bongo Bingo.

Link: https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...bili-watangaza-mgomo-rasmi-9.html#post4165977

Kwi kwi kwi teh teh teh!
 
...kwa akili ya kawaida tu,ukiona taarifa zinatolewa kwa wingi mahali ambapo upatikanaji wa hizo taharifa kabla ulikuwa wa taabu na nadra,jua moja kwa moja ukweli katika hizo taharifa zilizopatina kwa ghafla ni wakutafuta kwa tochi...
 
Kuna walakini ni hizi taarifa zinazotolewa kuhusu mgomo wa madaktari na kinachoendelea.
 
Huamini macho yako kwa unayoyasoma, tumia miguu yako uende Muhimbili halafu utujuze zaidi, au huamini na miguu yako?
 
Hahahaaaa
Hawa toka jana wametungiwa cha kutangaza, nadhani wanatangaza at gunpoint.
Napatwa na kicheko miye!
Wanawataka ma-interns wa nini?
Leo wanaonekana dili eeh?
Haya bana! Werevu mwingi mbele giza.

Naona unajichekesha wakati wenzako wanalia.
 
Kweli kuna bidii sana kwa serikali kuficha maovu na kujipanga....kama wangetumia nguvu ile kupata mwafaka wangepata but sasa ni rat race
 
Back
Top Bottom