RaiaMbishi
JF-Expert Member
- Jan 18, 2012
- 252
- 124
Hii ina faida kadhaa:
Muhimu ni kwamba itapunguza rushwa wakati wa uchaguzi wa NEC ambapo ilikuwa rahisi mno kuwahonga wajumbe wa mkutano mkuu wa taifa ambao walikuwa wanakusanyika Dodoma Kupigia kura wajumbe 80 wa NEC. Kama tunavyofahamu, Ili mtu uwe na uhakika wa kura nyingi za NEC au Ushinde mchakato wa kugombea urais kupitia CCM, ni lazima ukamate wajumbe kutoka kanda ya Ziwa na Zanzibar, huku ukiokoteza okoteza kwenye mikoa iliyobakia. Kabla ya mabadiliko haya ya katiba ya CCM, ilikuwa rahisi sana zamani kubeba mamilioni yako na kwenda Mwanza ili ukapande treni na wajumbe kutoka mikoa ya Mara, Shinyanga, Kagera na Mwanza, kuelekea nao kwa treni Dodoma. Kazi yako kubwa humo njiani ilikuwa ni kuwanunulia Konyagi na Biskuti za kutosha pamoja na kuwapa posho za kujikimu wakifika Dodoma.
Kwa vile wajumbe kutoka Zanzibar huwa wanaenda Dodoma dakika za mwisho kutokana na ukaribu wa Zanzibar na DSM/Dodoma, chini ya utaratibu wa zamani, ukishamaliza mkakati wako wa kanda ya ziwa, unahamia kwa wajumbe wa Zanzibar ambapo wao pia unaandaa manoti yako na kwenda Zanzibar ili pia ukapande nao boti la kuja DSM, kisha kusafiri nao kwenye mabasi kuelekea Dodoma. Wajumbe waliobakia kutoka mikoa mingine, aidha wapambe wako (wabunge kutoka mikoa husika) wanakufanyia kazi ya kuokoteza wajumbe wa hapa na pale, au shughuli hiyo unaifanya mwenyewe ukifika Dodoma kwa kuwatembelea wajumbe hao kwenye gesti zao na vilabu vya pombe nyakati za usiku na kusambaza bahasha huku ukiwanunulia madumu tosha ya chibuku.
Chini ya utaratibu huu mpya, ina maana haya yote hayatawezekana tena, kwani tofauti na zamani, inabidi aidha ‘to risk' ugombee katika nafasi zile kumi za bara ambazo zina vigogo wa kila aina, pengine hamsini wenye majina mazito an wasio na kashfa, au ukagombee wilayani, lakini huko, chama tayari kimetoa indication kwamba hakitaki wabunge kujirundikia vyeo, hivyo wabunge wengi wa sasa hawatapita uchaguzi wa NEC huko wilayani kwani candidates wengi wilayani watatumia silaha hiyo kuwamaliza wabunge watakao jaribu gombea nafasi za NEC wilayani kwa kusema kwamba wanaenda kinyume na nia nzuri ya CCM kupunguza vyeo vingi kuwa chini ya mtu mmoja n.k. Wabunge wa CCM wana mtihani mgumu sana chini ya utaratibu huu mpya, kwani wengi wao walikuwa wanapata posho nyingi sana kutoka kwa wanasiasa wenye nia ya Urais 2015, kwasababu wabunge wengi walikuwa ni wajumbe wa NEC, na pia by default wajumbe wa mkutano mkuu wa taifa.
Nadhani pia utaratibu wa kumpata mgombea urais kupitia CCM nao utabadilishwa siku za hapo mbeleni, ili wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Taifa ambao ndio wapiga kura kwa nafasi hiyo, wasilazimike kukusanyika kwenye treni na mabasi kuelekea Dodoma kwa ajili ya shughuli hiyo, kwani kufanya hivyo kutawapa mwanya wagombea wenye pesa nyingi kufanya vitu vyao kwa urahisi. Nadhani wajumbe hawa watabakia katika mikoa yao na CCM itakuja na utaratibu ambapo wagombea Urais watatembezwa na chama katika mikoa yote ili kwenda kujieleza mbele ya wajumbe, mgombea mmoja baada ya mwingine, halafu CCM kutanganza siku maalum ya wajumbe mikoani kote kupigia kura moja tu kuchagua nani wanadhani anafaa kuwa mgombea wa kiti cha Urais.
Inawezekana wanasiasa wenye pesa ndani ya CCM wakafanikiwa ‘to bypass' vizingiti hivi vipya, lakini kwa hili CCM inastahili pongezi kwani ili wanasiasa wa aina hii wafanikiwe, itabidi wajipange kweli kweli, vinginevyo watabainika kwa urahisi sana na kamati mpya ya nidhamu, TAKUKURU n.k.