TANZIA: Rtd Major General Anatoli R. Kamazima amefariki dunia

hivi mnavyoandika R.I.P Kamazima huko alipo anawasoma au ni ushambenga wa kiswahili wa kuiga kila kitu? acheni mbwembwe ndugu , kifo ndio mwisho wa safari ya mapambano ya hapa duniani, kilichobaki ni muhusika kupeleka hesabu zake kwa muumba , hizo R.I.P zenu hazisaidii kitu na wala muhusika hazisomi
Halo tuta ku-RIP kabla hujafa.
Na siku ukifa bado utapata RIP zaidi!
 
Huyu ni yule aliyekuwa DG wa kwanza wa kikosi cha kupambana na rushwa,na alikuwa askari wa cheo cha Gen kabla ya kuteuliwa kuwa mkuu wa pcb
 
Nilimfahamu kupitia mwanye anayeitwa Michael,poleni ndugu jamaa na marafiki,na Taifa kwa ujumla.

RIP Major General Kamazima.
 
Pomzika kwa Amani Former DG- of PCCB Utakumbukwa katika mengi tunakuombea Punziko la milele Major General KAMANZIMA umefanya mengi sana katika utumishi wa umma na ulio tukuka Mungu hakupe pumziko la milele.
 
R.I.P jirani, utakumbukwa kwa ucheshi wako na kujichanganya kwako na watu wa level zote kimaisha. Utumishi wako kazini utakumbukwa daima.
 
Rais Kikwete akitoa pole kwa mjane na ndugu wa Meja Jenerali Mstaafu Anatoli Kamazima leo nyumbani kwa marehemu Tegeta, Dar es Salaam.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete amemtumia salamu za pole Mkuu wa Majeshi Jenerali Davis Mwamunyange kufuatia kifo cha Meja Jenerali Anatory Ruta Kamazima (Mstaafu) aliyefariki jana tarehe 25 Septemba, 2012 katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili.



Kamazima.jpg
 
Rais Kikwete akiongea na Brigedia Jenerali Mstaafu Tindamanyire, ndugu wa hayati Meja Jenerali Mstaafu Anatoli Kamazima, leo nyumbani kwa marehemu Tegeta, Dar es Salaam. Kulia kwa Rais ni Mkuu wa Majeshi Jenerali Davis Mwamunyange na Mnadhimu Mkuu, Luteni Jenerali, Samwel Albert Ndomba. Marehemu Kamazima, ambaye amefariki dunia usiku wa kuamkia leo Jumatano ya Tarehe 26 Septemba, 2012 kutokana na mshtuko wa moyo, alikuwa Mkurugenzi Mkuu wa kwanza wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa nchini (TAKUKURU).


KAMAZIMA 2.jpg
 
Pomzika kwa Amani Former DG- of PCCB Utakumbukwa katika mengi tunakuombea Punziko la milele Major General KAMANZIMA umefanya mengi sana katika utumishi wa umma na ulio tukuka Mungu hakupe pumziko la milele.

Nchi hii ingepata watu aina ya Kamazima ngazi za juu ktk uongozi wa kisiasa ingekua imesonga mbali ktk maendelen. Alikua kiongozi wa kuzaliwa!
 
Aliongoza takukuru ya zamani enzi hizo ikiitwa pcb. Haikuwa na meno hadi hata baada ya kuitwa pccb, bado ni kiini macho tu.
 
Kibirizi wewe sio Kibilizi maana mimi Kibirizi naijua hakuna wajamja mtu kama wewe. Wewe ni Inside Man
 
kweliiiiii ulisema tutakukumbuka Major General Kamanzima ningumu kusahaulika jeshini na kwingineko kamanda wangu wa ukweli umenifunza uzalendo na kuwatumikia vyema wananchii wa tanzania pumzika kwa amani, TPDF Uliweka misingi imara kiutendaji.
 
Nimepata taarifa za kuuzunisha sana dakika chache zilizopita kwamba Retired Major General Anatoli Kamazima amefariki dunia ghafla usiku wa leo - kuamkia Jumatano ya Tarehe 26 Mwezi wa Tisa Mwaka 2012 kutokana na mshtuko wa moyo; Bwana alitoa, na Bwana ametwaa, Mungu amlaze mahali pema peponi Mzee wetu mpendwa Anatoli Kamazima, AMEN;

Innaa Lillahi wainnaa ilayhi Rajiuun
 
R.I.P General&the former pccb Director General!

at least umejaribu kufahamisha huyu General ni nani zaidi, maana nilitaka kuuliza mzee Kamazima mbali na kuwa kamanda alikuwa ni nani pia nchi hii? RIP former PCCB director
 
Back
Top Bottom