TANZIA: Rtd Major General Anatoli R. Kamazima amefariki dunia

Nimepata taarifa za kuuzunisha sana dakika chache zilizopita kwamba Retired Major General Anatoli Kamazima amefariki dunia ghafla usiku wa leo - kuamkia Jumatano ya Tarehe 26 Mwezi wa Tisa Mwaka 2012 kutokana na mshtuko wa moyo; Bwana alitoa, na Bwana ametwaa, Mungu amlaze mahali pema peponi Mzee wetu mpendwa Anatoli Kamazima, AMEN;

Duh.
Mungu amlaze pema ndugu Kamazima. Alikuwa kiongozi wa PCB, kabla haijabadilishwa na kuwa PCCB na kupewa Hosea
 
ndiye nani huyo?au ni mmojawapo wa hao warundi wanaojichukulia uraia kiholela nchi hii!

Makubwa tena haya inamaana maziko yatafanyika huko kwao? Dah Mwenyezi Mungu aiweke Roho ya Marehemu pahali panapostahili....

Hii nchi watu wanajua siri za watu na kuzitoa siku wanapoondoka au kuaga Dunia...
Tuasikia mengi sana baada ya vifo vya Viongozi wetu hadi pale Rushwa itakapoisha...
 
Mkuu Mchambuzi unaweza kutuwekea wasifu wa Rtd Majar General Kamazima.Wengi hatui alikuwa nani zaidi ya wadhifa wa Major General.

RIP Major General Kamazima.
 
Last edited by a moderator:
RIP Maj. Gen. Kamazima. Pole kwa mke, watoto, wajukuu, ndugu, marafiki, Watanzania wote, wanajeshi wote, wana PCCB wote, wana Kanda ya ziwa wote, wana Kagera wote, wana Bukoba wote na wana Maruku wote.

Bwana alitoa naye ametwaa, jina lake libarikiwe.
 
Makubwa tena haya inamaana maziko yatafanyika huko kwao? Dah Mwenyezi Mungu aiweke Roho ya Marehemu pahali panapostahili....

Hii nchi watu wanajua siri za watu na kuzitoa siku wanapoondoka au kuaga Dunia...
Tuasikia mengi sana baada ya vifo vya Viongozi wetu hadi pale Rushwa itakapoisha...

Kamazima ni mhaya,mzaliwa wa kijiji cha Maruku,Bukoba vijijini. Mmoja wa maafisa wa jeshi wenye nidhamu na uzalendo wa hali ya juu JWTZ limepata kuwa nao.
 
Kamazima ni mhaya,mzaliwa wa kijiji cha Maruku,Bukoba vijijini. Mmoja wa maafisa wa jeshi wenye nidhamu na uzalendo wa hali ya juu JWTZ limepata kuwa nao.
Hivi Bukoba inapakana na Burundi? manake nilisikia kuna Mbunge walimsema alivuka mpaka akaishi hadi alipogombea vyeo ndipo uhakiki ukaanza... ila hilo jina limekaa ki untanzanian
 
Dah ni habari za kusikitisha sana, poleni mke, watoto na wafiwa wote. Kwa watu wasiomfahamu Mzee Meja Jenerali Mstaafu Anatoly Kamazima, alikuwa Mkurugenzi Mkuu wa kwanza wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa nchini TAKUKURU (PCCB)>

RIP Major Kamazima. Poleni wafiwa. Kwa wale wasiomfahamu ndiye pamoja na timu yake aliyeweka mkakati wa kufungua ofisi za TAKURU katika mikoa na Wilaya. Kabla ya hapo ofisi zilikuwa kwenye kanda tu. Ndiye pamoja na timu yake alijitahidi kupanua ajira kwenye Taasisi hiyo na sasa maafisa wamekuwa wengi. Ndiye aliandaa mabadiliko ya sheria na kupanua wigo wa makosa ya rushwa.
 
Pole sana....by the way....haihusiki na vikao vya mr. dhaifu vinavyoendelea? nadhani kazi ya Mungu tu!!!!!
 
Hivi Bukoba inapakana na Burundi? manake nilisikia kuna Mbunge walimsema alivuka mpaka akaishi hadi alipogombea vyeo ndipo uhakiki ukaanza... ila hilo jina limekaa ki untanzanian

Tatizo la nchi hi4 sasa ni kutilia mashaka uraia wa kila mtu, utafika wakati hakuna mtu atakayehesabiwa kuwa ni raia halali wa nchi hii, hii ni kansa inahitaji hatua za haraka zichukuliwe. Maj. Gen. Kamazima ni mhaya wa Maruku nje kidogo ya Manispaa ya Bukoba. Ni jirani yake na Prof. Mwesiga Baregu.
 
Back
Top Bottom