Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Hii inadhihirisha Pinda si lolote, si chochote.
Nasema hivi kwa sababu, tangu Jan amewahadaa madaktari, mara vitisho, mara tunajipanga, .... huku wananchi wakiendelea kufa. Angemwambia tu tangu wakati huo bosi wake kuwa suala hilo hawezi kulishughulikia, hana nguvu ya ofisi...Nawapongoza madaktari kwa hatua hiyo. Natumaini JK hatawaangusha watanzania.
Pia ni matumaini yetu kuwa Mponda na Nkya wataachia ngazi, bila kusubiri kufukuzwa. Mungu awabariki na wote mlioshirikiana nao katika kulifikisha zoezi hili hapa.
Kenya, Chadema, Madaktari!
Ama kweli JK ni moto wa kuotea mbali! Mkishajipeleka kumuona tu lazima mlainike wenyewe!
Hongera sana JK..wewe ni DR kwa ukweli!
Nimewapenda madaktari upeo. I support you. Ujumbe umetumwa na nina uhakika umefika "loud and clear"
Nafahamu msimamo wenu ulikua kwamba hamtaji mazungumzo hadi mponda na huyo mama watimuliwe...sasa iweje mmeruhusu iyo stej ya pili ya mazungumzo kabla hiyo ya kuwasimamisha kutekelezwa..unless j3 jk aseme amewasimamisha tofaut na apo hatutawaelewa...ikulu juice at work!!n
JK amechelewa mno kutoa suluhu mpaka baada ya pande zote kusuguana hadi zimechoka. Pili ni dalili kuonyesha kuwa yeye anafanya kazi peke yake pasipo kushishirikiana na Pinda ili jamii imuone Pinda ni dhalili. Hii ni hatari kiuongozi. Kama angeona Pinda hana uwezo basi angejadiliana na Madaktari bila kumtuma Pinda
And that is how the magic brain of the doctor works!!!
JK kiboko ya njia kwani madaktari i wazalendo kabisa nimewadharau hasa mnapoanza kujibembeleza kuwa lengo lenu sio kugoma Hawa mawaziri wanawahusu nini? km sio kutumwa kisiasaWaliomkimbia bungeni walimfuata ikulu wakanywa juice na pilau, nakumbuka kauli ya katibu wao "Eti mweshimiwa rais watu wanasema nilikukimbia... teh teh teheeee...... ".
Waliikataa rasimu ya katiba wakaikubali ikulu.
JK ni mwiba, hoja yao kuu madaktari ilikuwa mponda na nkya wapigwe chini! wamerudi kimyaaaa......
Mwasi, kwani mwanzo alikuwepo?. Si alikuwa safarini!. Mara ya pili alikuwepo?.Si alikuwa Mlima Kilimanjaro!. Karudi, si kawaita Ikulu na kumaliza mambo!. Sometimes the end, justifies the means!. Mgomo umeisha!, tusonge mbele!.
ni kama vile viongozi wa chadema walipoalikwa chai na juice pale ikulu na kuhidumiwa na JK basi mpaka leo hatuoni zile kelele tena! hekima itawale kwanza ili tushinde!
Tamko mlilotoa linaviashiria vya U-LOOSER!!
linafanana na yale majigambo wa watu waoga kwamba. umenipiga huku mtaani siku ukija kwetu utaniona!!
mkuu we mchungaji au?unafikiri unamjua sana Mungu kuliko watu wengine wote?nakushauri hii homily yako wapelekee family yako kwanza....who doesnt know kwamba duniani tunapita?wewe ndio lusekelo nini?kiufupi mkuu mgomo huo mlichemka ile mbaya, kwani mlikuwa hamjaambiwa kuwa hatoondoshwa pale, majibu ya raisi hayajapingana na ya pinda. Pinda alisema madai ya kuwaondosha waziri na naibu wake yanashughulikiwa na serikali wala hakusema kuwa serikali imesema haitowaondosha pale. Jaziba na ukurupukaji wa kuona kuwa hamkosei ndio imewafanya mchukiwe na jamii, ndio maana hapo kwenye tamko lako umeanza kujitetea kwa jamii. Nyie madaktari ndio mnaoomba rushwa na sio Haji mponda, nyie ndio mnajifanya mko busy tunapokuja kwenye hospitali kupata huduma, nyinyi ndio wengi mnamiliki vituo vya afya,nyinyi ndio mnao kuwa mnawaelekeza wagonjwa wakanunue dawa kwenye farmacy zenu, nyie madaktari ndio mnaotoa mimba, nyie madaktari ndio mnaowauzia wagonjwa damu, yaani jamii ikipima makosa ya Hadji mponda na nyie, yaani nyie ndio mlipaswa kuondoshwa wote ila basi tu, nyie madaktari hamwajibiki vile inavyopaswa kwani mnafanya kazi zaidi ya hospitali moja hali ya kuwa nyie ni waajiliwa wa serikalini na mmesomeshwa bure na serikali, nyie madaktari ndio baadhi yenu huchukua dawa kwenye vituo vya serikali wanakofanyia kazi na kupeleka kwenye vituo vyao wanavyomiliki, sasa nataka mniambie je haya yote na mangine mengi tu mnayajua nyinyi wenyewe,kama yale ya muhimbili,mwananyamala na kungineko mnakojua wenyewe mlikuwa mnayafanya kwa sababu ya Hadji Mponda??? hasa wewe raisi uliyekuwa kinara wa kutangaza migomo nakushauri sana rudi kwa mola wako ukatubu ukweli wa kutubu kwani usidhani Mungu atakuacha ivi ivi kwa yaliyotokana na ujeuri wa cheo hicho. Kila unalolifanya kaka ujue linarekodiwa na mbele za Mungu utaulizwa. Kwahiyo kafanye toba ya kweli. na kama hamkuwa na chuki binafsi kwa waziri basi hamna sababu ya kumchukia ivo vyote kwani kama mnaona kafanya makosa basi jueni kuwa na yeye ni binadamu. ivi nyinyi ni wasafi kiasi gani mpaka mseme hamtotoa ushirikiano wa kibinafsi wala wa kiutendaji? ivi nyie Mungu nanyi akisema hatowasamehe makosa yenu mnayoyatenda kila kukicha mtafanya nini? kama Mungu mwenyewe Muumba wa mbingu na aridhi na vyote vilivyomo anasamahe je iweje nyie, ivi rais wa MAT huo ujeuri hasa unautoa wapi? mrudie Mungu wako ukatubu kwani duniani sisi ni wa kupita tu.