Taarifa rasmi ya kusitisha mgomo kutoka chama cha madaktari 10/03/2012

Ndiyo kilichobaki kuilazimisha serikali kufanya kile tunachaamini ni haki na stahili zetu za msingi.
 
Nafahamu msimamo wenu ulikua kwamba hamtaji mazungumzo hadi mponda na huyo mama watimuliwe...sasa iweje mmeruhusu iyo stej ya pili ya mazungumzo kabla hiyo ya kuwasimamisha kutekelezwa..unless j3 jk aseme amewasimamisha tofaut na apo hatutawaelewa...ikulu juice at work!!n
huelewi nini ndugu....ww ndiyo wale mnatibiwa Appolo nn?
ww ulitaka mgomo uendelee mpaka lini labda?
 
Madaktari ndio walioshindwa na si hao Mawaziri, nna kuhakikishia hao Mawaziri wamefunga mianya ya ubadhirifu mingi kwa madaktari na ndio sababu za kuchukiwa, hakuna zaidi. Na Ikulu wakapewa taswira kwa mbali, wameelewa kuwa huwezi kuwa na dhambi halafu ukajifanya wewe ni msafi na fulani ndio mchafu wakati hujaonesha huo uchafu wake uko wapi.

Sijasikia hao MAT wakisema Mponda au Nkya kafanya hiki na hiki na hiki kibaya na ndio sababu hatuwataki. Hawana lolote zaidi ya walitaka kuficha maovu yao Na wameoneshwa, eeeeh nyie hiki nini na hiki nini na hiki nini, sasa amuweni wenyewe mnarudi kazini na kutangaza kusitisha mgomo au mnaendelea na madai yenu ya kijinga na kubakisha yale ya awali mliokubaliana na Pinda? wenyewe wakasema basi, yaishe Mzee, sisi tunabakisha yale yale, tunaomba uyashughulikie Mzee, haya mengine yote basi, tumetubu. Unacheza na Serikali?
hebu tuambie ile mashine ya dialysis aliyoiba nyoni imeenda wapi?
hebu tuambie uagizwaji wa vifaa feki ikiwemo vya kupimia ukimwi aliagiza dokta gani? kama siyo nyoni na hao kina mponda na nkya.......na wewe mapovu yanakutoka kweli kweli dili zimeyeyuka wenzako wanatolewa wizarani huna lolote daktari mzima mwizi.....bado na ww utashughulikiwa.
 
bora wameacha mgomo maana kama ni mishahara kwa muundo wa afya ulivyo na kwa hali ya nchi yetu wanalipwa vizuri kuliko kada nyingine zote. Sijui kwanini UTUMISHI wameshindwa kuliweka hili vizuri. Na kuhusu nani ajiuzulu au asijiuzulu hiyo ni pure politics. Waziri atajiuzulu kwa kauli zake. Madaktari je? Baada ya vifo vilivyotokea wataacha kazi kusafisha nafsi zao?
kwani zimechafuka vipi?....put in your mind daktari ameshashuhudia vingi sana ,endelea na maisha yako ukiumwa ukatibiwa hospitali saiv utawakuta wanachapa kazi.
 
kiufupi mkuu mgomo huo mlichemka ile mbaya, kwani mlikuwa hamjaambiwa kuwa hatoondoshwa pale, majibu ya raisi hayajapingana na ya pinda. Pinda alisema madai ya kuwaondosha waziri na naibu wake yanashughulikiwa na serikali wala hakusema kuwa serikali imesema haitowaondosha pale. Jaziba na ukurupukaji wa kuona kuwa hamkosei ndio imewafanya mchukiwe na jamii, ndio maana hapo kwenye tamko lako umeanza kujitetea kwa jamii. Nyie madaktari ndio mnaoomba rushwa na sio Haji mponda, nyie ndio mnajifanya mko busy tunapokuja kwenye hospitali kupata huduma, nyinyi ndio wengi mnamiliki vituo vya afya,nyinyi ndio mnao kuwa mnawaelekeza wagonjwa wakanunue dawa kwenye farmacy zenu, nyie madaktari ndio mnaotoa mimba, nyie madaktari ndio mnaowauzia wagonjwa damu, yaani jamii ikipima makosa ya Hadji mponda na nyie, yaani nyie ndio mlipaswa kuondoshwa wote ila basi tu, nyie madaktari hamwajibiki vile inavyopaswa kwani mnafanya kazi zaidi ya hospitali moja hali ya kuwa nyie ni waajiliwa wa serikalini na mmesomeshwa bure na serikali, nyie madaktari ndio baadhi yenu huchukua dawa kwenye vituo vya serikali wanakofanyia kazi na kupeleka kwenye vituo vyao wanavyomiliki, sasa nataka mniambie je haya yote na mangine mengi tu mnayajua nyinyi wenyewe,kama yale ya muhimbili,mwananyamala na kungineko mnakojua wenyewe mlikuwa mnayafanya kwa sababu ya Hadji Mponda??? hasa wewe raisi uliyekuwa kinara wa kutangaza migomo nakushauri sana rudi kwa mola wako ukatubu ukweli wa kutubu kwani usidhani Mungu atakuacha ivi ivi kwa yaliyotokana na ujeuri wa cheo hicho. Kila unalolifanya kaka ujue linarekodiwa na mbele za Mungu utaulizwa. Kwahiyo kafanye toba ya kweli. na kama hamkuwa na chuki binafsi kwa waziri basi hamna sababu ya kumchukia ivo vyote kwani kama mnaona kafanya makosa basi jueni kuwa na yeye ni binadamu. ivi nyinyi ni wasafi kiasi gani mpaka mseme hamtotoa ushirikiano wa kibinafsi wala wa kiutendaji? ivi nyie Mungu nanyi akisema hatowasamehe makosa yenu mnayoyatenda kila kukicha mtafanya nini? kama Mungu mwenyewe Muumba wa mbingu na aridhi na vyote vilivyomo anasamahe je iweje nyie, ivi rais wa MAT huo ujeuri hasa unautoa wapi? mrudie Mungu wako ukatubu kwani duniani sisi ni wa kupita tu.
wewe unatibiwa na Maji marefu nini?
tunawaelekeza wakanunue dawa ....kwanini hospitalini hazipo?
 
Wewe nawe? Taarifa ni hiyo hapo juu, makubaliano yepi tena? ni very simple. Karibuni, wakapigwa gahwa kwa juisi ya tende, baada ya kumaliza wakaambiwa haya leteni hoja zenu, wakaongea wao tu kumaliza, wakaambiwa haya tazameni hii, kila mmoja akapewa faili lake aone mwenyewe, walipomaliza kutazama wakaulizwa? Je,, bado mnaendelea na madai yenu mapya? wakasema hapana Mzee. Kikwete akawaambia haya rudini kazini na mkawatangazie Watanzania, wakawa hawajui waje kuwaambia nini wenzao waliowatuma Ikulu, leo wakawaambia uongo mtupu na hao wenza ndio wakasema kama ni hivyo basi Nkya hatumtaki na tutangaze kuwa ni adui yetu yeye pamoja naMponda. Shock waliyokuwa nayo toka walipotoka Ikulu wakakubaliana tu wenzao kwani wana uhakika kuwa hao wenzao hawajui yaliojiri Ikulu.

Hao jamaa toka wametoka Ikulu, mambo waliyooneshwa huko kwenye mafaili yao, hawajapata usingizi mpaka dakika hii. Amini usiamini, hakuna zaidi kilichojiri.

Usione kelele za humu JF tumeachiwa tupayuke ukaona Serikali haipo, ipo tena inatujuwa kuliko tunavyojijuwa sisi wenyewe. Kalagabaho.
they negotiate for 6 hours hlf ww unaleta porojo zako hapa......imekula kwako ulaji ndiyo kushnehi saiv.
 
This is amazing coz i wonder what happens 2 MAT leaders walivyokutana na JK ikulu, inaonyesha JK ana kipaji cha aina yake kuweza kuwashawishi madaktari kusitisha mgomo bila masharti yoyote,na kuahidiwa madai yao yatashughulikiwa....kuna ukweli wowote hapo?Na hili swala la kumkataa Waziri na Naibu wake wamwachie JK na Pinda...wao ndo watajua nini cha kufanya...
 
JK kiboko ya njia kwani madaktari i wazalendo kabisa nimewadharau hasa mnapoanza kujibembeleza kuwa lengo lenu sio kugoma Hawa mawaziri wanawahusu nini? km sio kutumwa kisiasa
Nyie daini yenu, mkafungue vidispensari hata mwenye mimba akija watoeni
sishsngai mimi ,this is small brain kazini.
 
They didn't solve the issue! If they did, we can't tell from their statement. The Ministers are still in charge of what the doctors do, but yet they don't recognize or respect them. We can tell that the President won, which is ok, but until he removes the two Ministers, how have the doctors won? The fact that they stripped Dr. Nkya of her certificate/membership is not a big deal, because she wasn't a practing physician anyway and I doubt she is going to need her membership any time soon. I think this was a good face-saving move for the President but unfortunately for the good doctors, unless these two Ministers go, they haven't saved their own faces.
unless you wanted doctors to pursue your agenda and not theirs....if that bso imekula kwenu, we are moving on to the next step of discussion and tutashinda hii vita vizuri sana just wait and u will see.
 
RIPOTI KWA VYOMBO VYA HABARI.

UTANGULIZI
Baada ya kikao cha madaktari kilichofanyika leo tarehe 10/3/2012. Madaktari nchini kupitia chama cha madaktari Tanzania (MAT), tunapenda kutoa ufafanuzi ufuatao:

... 1. Jamii ielewe kuwa daktari kama binadamu mwingine anayefanya kazi Tanzania ana mahitaji muhimu (basic needs) na mahitaji ya kijamii (social responsibility) na hivyo si chombo cha kufanyia kazi (Machine).

2. Pia Daktari ana haki ya kupata ujira unaomfaa kutokana na kazi anayofanya na ana haki ya kuacha kazi muda wowote iwapo ataona kazi hiyo ya udaktari haimpi ujira wa kutosha na heshima ya kuendesha maisha yake.

3. Pia jamii itambue kuwa daktari anaweza kulazimishwa kurudi kazini lakini hawezi kulazimishwa kufanya kazi. Matokeo ya kulazimishwa yanaweza yasiwe mazuri kwa wale watakao hudumiwa.

4. Jamii itambue kuwa madai na hoja kuu za madaktari ni kwa ajili ya faida ya Watanzania wote,yakiwemo mazingira bora ya kufanya kazi mjini na vijijini, na kuboresha afya za watanzania kwa ujumla. Pia vifaa na dawa ziwepo mahospitalini zinakohitajika.

5. Pia tunawashukuru madaktari wote kwa mshikamano wetu tulioonyesha na tunaomba mshikamano huu uendelee daima.

TAMKO LETU:

JANA TAREHE 9/3/2012, TULIKUTANA NA MH. RAIS WA JAMUHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA MH. DR. JAKAYA MRISHO KIKWETE. TULIMWELEZA HOJA ZETU, AMBAZO ALIZIELEWA NA ALIAHIDI KUZISHUGHULIKIA KIKAMILIFU. TUNA IMANI SANA NA MH. RAIS KWAMBA HATATUANGUSHA.

KUTOKANA NA HILO, TUNAPENDA KUUTANGAZIA UMMA WA WATANZANIA KUWA TUNARUDI KAZINI RASMI KUANZIA LEO TAREHE 10/3/2012, WAKATI MHESHIMIWA RAIS AKISHUGHULIKIA MADAI YETU.

PIA WAKATI MADAI YETU YAKISHUGHUKLIKIWA TUNAPENDA KUSEMA KUWA HATUNA IMANI NA WAZIRI WA AFYA MH. DR. HAJI MPONDA NA MH. DR. LUCY NKYA, NA KUWA TUNAMSIMAMISHA RASMI UANACHAMA WA MAT MH. DR. LUCY NKYA.

MADAKTARI TUNATAMKA WAZI KUWA WAZIRI WA AFYA DR. HAJI MPONDA NA NAIBU WAKE DR. LUCY NKYA NI MAADUI WA MADAKTARI NA SEKTA YA AFYA KWA UJUMLA HAPA NCHINI NA TUNAAHIDI KUTOKUWAPA USHIRIKIANAO WA AINA YOYOTE WA KIBINAFSI AU WA KIUTENDAJI.

SOLIDARITY FOREVER.
RAIS(MAT)


Nyongeza

  1. PIA MADAKTARI KAMA WATAALAM WALIOSOMEA FANI ZINGINE MFANO ENGINEERS,WANASHERIA WALIMU NK WAMESOMESHWA NA SERIKALI KWA RUZUKU KWANI MADAKTARI PIA NAO NI WADAIWA WA LOAN BOARD KAMA WALIVYO HAWA WATALAAM WA FANI ZINGINE TENA UKIFUATILIA UTAGUNDUA KUWA MADENI YA MADR NI MAKUBWA ZAIDI YA HATA HAWA WA FANI ZINGINE HIVYO SERIKALI NA JAMII HUSIKA WAACHE UPOTOSHAJI USIOKUWA NA MSINGI
  2. WITO WA KWENYE FANI YA AFYA SI WA MADR TU HATA KIAPO CHA MADR KINAONESHA HILI KUWA SERIKALI NA WANANCHI PIA WANAHUSIKA KATIKA KUDUMISHA KIAPO HIVYO UPANDE MMOJA UKIVUNJA KIAPO BASI KINAVUNJIKA RASMI KWA PANDE ZOTE KWANI UDUMISHAJI WAKE UNATEGEMEA PANDE HIZO MUHIMU.
  3. MADAKTARI WALILAZIMISHWA KUGOMA NA SERIKALI KWA SERIKALI KUTAKA KUWAACHIA JUKUMU LA KUTOA HUDUMA YA AFYA BILA YA "KUWEZESHWA " ILI HALI SERIKALI NDIO YENYE JUKUMU LA KUTOA HUDUMA YA AFYA KWA WANANCHI KIKATIBA...
    HIVYO MADAKTARI WANARUDI KAZINI,LAKINI WANANCHI WAELEWE KUWA VITU VINGI MUHIMU VILIVYOKUWA VIKIDAIWA BADO HAVIJATIMIZWA ,ILA NI KWA IMANI KUWA SERIKALI ITAYAPA UZITO STAHILI HAYA MATATIZO NA KUBORESHA HUDUMA YA AFYA KADIRI IWEZEKANAVYO KWA NIA YA DHATI KWANI MAZINGIRA YA KAZI BADO YATAKUWA NI MAGUMU NA HATARISHI KWA WATUMISHI WA AFYA PIA WAGONJWA WENYEWE.
Nawapongeza madaktari kwa uamuzi wenu wa busara kurudi kazini,pia naunga mkono kilichotajwa hapo juu nijuavyo mimi
HAKUNA SOKO LA BEI NAFUU KWA AJILI YA WANAOFANYA KAZI YA WITO,HAKUNA SHULE YA BEI NAFUU (LABDA YEBOYEBO) KWA AJILI YA WATOTO WA WENYE WITO;HAKUNA MABASI YA KUWAPELEKA KAZINI WENYE WITO BILA KULIPA NAULI n.k Kwa hiyo tusiwakandamize madokta kwa kisingizio cha wito.Ebu watu wote tuwajibike kuijenga tz,kila mtu anuie kuijenga nchi na siyo kundi dogo kulilazimisha lifanye kazi kwa niaba ya wengine.Hoja ya kusema waganga hawawahurumii watz maskini haina nguvu coz aliyewafanya watz kuwa maskini amewajibishwa? kwa nini wahurumiwe na waganga na siyo serikali yenye dhamana.Mwisho nisema wale waliopoteza maisha ktk sakata hili serikali ijenge mnara na kuweka majina yao waunganishwe na mashujaa(HERO) waliofia haki za nchi hii.
 
mkuu we mchungaji au?unafikiri unamjua sana Mungu kuliko watu wengine wote?nakushauri hii homily yako wapelekee family yako kwanza....who doesnt know kwamba duniani tunapita?wewe ndio lusekelo nini?

Hiyo ni jeuri, na siku zote jeuri ni sifa za kishetani. Umeambiwa mrejee Mungu upate kutubu
 
Back
Top Bottom