Taarifa rasmi ya kusitisha mgomo kutoka chama cha madaktari 10/03/2012

vimon

Senior Member
Apr 3, 2008
183
195
RIPOTI KWA VYOMBO VYA HABARI.

UTANGULIZI
Baada ya kikao cha madaktari kilichofanyika leo tarehe 10/3/2012. Madaktari nchini kupitia chama cha madaktari Tanzania (MAT), tunapenda kutoa ufafanuzi ufuatao:

... 1. Jamii ielewe kuwa daktari kama binadamu mwingine anayefanya kazi Tanzania ana mahitaji muhimu (basic needs) na mahitaji ya kijamii (social responsibility) na hivyo si chombo cha kufanyia kazi (Machine).

2. Pia Daktari ana haki ya kupata ujira unaomfaa kutokana na kazi anayofanya na ana haki ya kuacha kazi muda wowote iwapo ataona kazi hiyo ya udaktari haimpi ujira wa kutosha na heshima ya kuendesha maisha yake.

3. Pia jamii itambue kuwa daktari anaweza kulazimishwa kurudi kazini lakini hawezi kulazimishwa kufanya kazi. Matokeo ya kulazimishwa yanaweza yasiwe mazuri kwa wale watakao hudumiwa.

4. Jamii itambue kuwa madai na hoja kuu za madaktari ni kwa ajili ya faida ya Watanzania wote,yakiwemo mazingira bora ya kufanya kazi mjini na vijijini, na kuboresha afya za watanzania kwa ujumla. Pia vifaa na dawa ziwepo mahospitalini zinakohitajika.

5. Pia tunawashukuru madaktari wote kwa mshikamano wetu tulioonyesha na tunaomba mshikamano huu uendelee daima.

TAMKO LETU:

JANA TAREHE 9/3/2012, TULIKUTANA NA MH. RAIS WA JAMUHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA MH. DR. JAKAYA MRISHO KIKWETE. TULIMWELEZA HOJA ZETU, AMBAZO ALIZIELEWA NA ALIAHIDI KUZISHUGHULIKIA KIKAMILIFU. TUNA IMANI SANA NA MH. RAIS KWAMBA HATATUANGUSHA.

KUTOKANA NA HILO, TUNAPENDA KUUTANGAZIA UMMA WA WATANZANIA KUWA TUNARUDI KAZINI RASMI KUANZIA LEO TAREHE 10/3/2012, WAKATI MHESHIMIWA RAIS AKISHUGHULIKIA MADAI YETU.

PIA WAKATI MADAI YETU YAKISHUGHUKLIKIWA TUNAPENDA KUSEMA KUWA HATUNA IMANI NA WAZIRI WA AFYA MH. DR. HAJI MPONDA NA MH. DR. LUCY NKYA, NA KUWA TUNAMSIMAMISHA RASMI UANACHAMA WA MAT MH. DR. LUCY NKYA.

MADAKTARI TUNATAMKA WAZI KUWA WAZIRI WA AFYA DR. HAJI MPONDA NA NAIBU WAKE DR. LUCY NKYA NI MAADUI WA MADAKTARI NA SEKTA YA AFYA KWA UJUMLA HAPA NCHINI NA TUNAAHIDI KUTOKUWAPA USHIRIKIANAO WA AINA YOYOTE WA KIBINAFSI AU WA KIUTENDAJI.

SOLIDARITY FOREVER.
RAIS(MAT)


Nyongeza

  1. PIA MADAKTARI KAMA WATAALAM WALIOSOMEA FANI ZINGINE MFANO ENGINEERS,WANASHERIA WALIMU NK WAMESOMESHWA NA SERIKALI KWA RUZUKU KWANI MADAKTARI PIA NAO NI WADAIWA WA LOAN BOARD KAMA WALIVYO HAWA WATALAAM WA FANI ZINGINE TENA UKIFUATILIA UTAGUNDUA KUWA MADENI YA MADR NI MAKUBWA ZAIDI YA HATA HAWA WA FANI ZINGINE HIVYO SERIKALI NA JAMII HUSIKA WAACHE UPOTOSHAJI USIOKUWA NA MSINGI
  2. WITO WA KWENYE FANI YA AFYA SI WA MADR TU HATA KIAPO CHA MADR KINAONESHA HILI KUWA SERIKALI NA WANANCHI PIA WANAHUSIKA KATIKA KUDUMISHA KIAPO HIVYO UPANDE MMOJA UKIVUNJA KIAPO BASI KINAVUNJIKA RASMI KWA PANDE ZOTE KWANI UDUMISHAJI WAKE UNATEGEMEA PANDE HIZO MUHIMU.
  3. MADAKTARI WALILAZIMISHWA KUGOMA NA SERIKALI KWA SERIKALI KUTAKA KUWAACHIA JUKUMU LA KUTOA HUDUMA YA AFYA BILA YA "KUWEZESHWA " ILI HALI SERIKALI NDIO YENYE JUKUMU LA KUTOA HUDUMA YA AFYA KWA WANANCHI KIKATIBA...
    HIVYO MADAKTARI WANARUDI KAZINI,LAKINI WANANCHI WAELEWE KUWA VITU VINGI MUHIMU VILIVYOKUWA VIKIDAIWA BADO HAVIJATIMIZWA ,ILA NI KWA IMANI KUWA SERIKALI ITAYAPA UZITO STAHILI HAYA MATATIZO NA KUBORESHA HUDUMA YA AFYA KADIRI IWEZEKANAVYO KWA NIA YA DHATI KWANI MAZINGIRA YA KAZI BADO YATAKUWA NI MAGUMU NA HATARISHI KWA WATUMISHI WA AFYA PIA WAGONJWA WENYEWE.
 
JK ameahidi kuwafukuza kazi Mponda na Nkya? Au ameahidi hadi lini atakuwa ameshayashuhulikia madai yetu? Atatumia utaratibu gani kuyashuhulikia, atatumia wale MADALALI (wahuni) wa Pinda?
 
Tamko mlilotoa linaviashiria vya U-LOOSER!!
linafanana na yale majigambo wa watu waoga kwamba. umenipiga huku mtaani siku ukija kwetu utaniona!!
 
Baada ya Gahwa na Juisi za tende, hizo ni ngonjera. Ukweli unabaki kuwa ukweli, madai yenu mliahidiwa pia kushughulikiwa na Pinda na yanashughulikiwa, kwa hilo hamna jipya.

Nyinyi mlikazania Mponda na Nkya wafukuzwe kazi, sasa yamewashinda ngonjera imedilika na kuwa kama watoto wadogo mnakuja eti Nkya kafukuzwa uanachama wa MAD na Mponda na Nkya ni "maadui wa madaktari" "hatuwapi ushirikiano|, Huo ni utoto na ujinga.

Mkubali tu kuwa mliyoyakuta Ikulu hamkuyategemea na yamewanyamazisha na Mponda na Nkya wanadunda kama Waziri na Naibu Waziri. Huyo ndio Jakaya Mrisho Kikwete, kaweza kuwaunganisha Wapemba na Waunguja itakuwa nyinyi?

Umewashuka.
 
Mimi naona wameharakia, mgomo ungeendelea mpaka uchaguzi wa Arumeru uishe.
 
JK ameahidi kuwafukuza kazi Mponda na Nkya? Au ameahidi hadi lini atakuwa ameshayashuhulikia madai yetu? Atatumia utaratibu gani kuyashuhulikia, atatumia wale MADALALI (wahuni) wa Pinda?

Tamko ndio hilo, na hasira huzioni humo? unauliza nini kisichoeleweka hapo, you do not have even to read between the lines.
 
Hii inadhihirisha Pinda si lolote, si chochote.
Nasema hivi kwa sababu, tangu Jan amewahadaa madaktari, mara vitisho, mara tunajipanga, .... huku wananchi wakiendelea kufa. Angemwambia tu tangu wakati huo bosi wake kuwa suala hilo hawezi kulishughulikia, hana nguvu ya ofisi...Nawapongoza madaktari kwa hatua hiyo. Natumaini JK hatawaangusha watanzania.
Pia ni matumaini yetu kuwa Mponda na Nkya wataachia ngazi, bila kusubiri kufukuzwa. Mungu awabariki na wote mlioshirikiana nao katika kulifikisha zoezi hili hapa.
 
Back
Top Bottom