TAARIFA: Maandalizi ya Heshima za mwisho na Mazishi ya Mh Bob N. Makani

Mkuu Kimbunga kumbe umeanza harakati za siasa siku nyingi, huyu Mzee Makani nilikuwa namkubali sana nakumbuka wakati anagombea ubunge pale Shinyanga Mjini nilifika pale kwenye mikutano yake uwanja Kambarange na Ngokoro.

Ritz,

Ili kumtendea haki kwa kumkubali zaidi...do the obvious: Vua gamba vaa gwanda!
 
Aisee,kumbe ritz ulikuwepo na ulishuhudia jinsi Mzee Bob Makani alivyomchachafya 'Ng'wana Derefa'?na uliona jinsi CCM ilivyoanza kuchakakachua kura siku nyingi?..eeh pale ni NGOKOLO-sio Ngokoro (Wasukuma hawana 'R'). Unakumbuka pia picha yake (bango) la Bob lilivyokuwa limesheheni CV nzito (ingawa lilikuwa black and white)?Unakumbuka alivyokuwa akivuta umati wa watu na msisimko katika mikutano yake? Hiyo ilikuwa miaka ya tisini(Then watu wanasema mageuzi Shinyanga yameanza juzi!!).

Nilikuwepo mkuu nilikuwa nimeweka kambi kule Maganzo si unajua tena kazi za Maganzo, nilikuwa nakuja sana mjini watu walikuwa wanampenda sana Bob Makani, mkutano wake pale uwanja wa Shycom watu walijaa sana, mwaka jana nimepita apo Shinyanga naona uwanja wa Shycom watu wamevamia.
 
Nawapa pole wadau wote wa CDM alianzisha chama makini ametuachia uridhi tosha kwa taifa hatuku sahau lamba chadema ife
 
Ritz hivi huwa unapumzika wewe kweli?

By the way sometimes unaongeaga point...tatizo lako tu ni pale u-magamba unapokupofusha macho!

Kupumzika vipi mkuu? Mie nikipata muda naingia JF ukitaka kuangalia watu kama hawapumziki nenda MMU au Chit-Chat watu wanalala JF...angalia idadi ya post zangu na muda niliyojiunga JF..kuna watu wana miezi miwili JF wana post 10.000.
 
mikoa ya kaskazini ni kilimanjaro,arusha,manyara,tanga ni mkoa wa pwani ya kaskazini mwa tanzania upooo! shinyanga sio kaskazini,tuache malumbano,twende msibani.
 
Back
Top Bottom