Taarifa kwa Wanajukwaa la Elimu.

Kurzweil

JF-Expert Member
May 25, 2011
6,622
8,397
Kwanza kabisa nawaomba radhi kwa kuweka kitu tofauti na maudhui ya jukwaa, lakini imenibidi kufanya hivi ili kuokoa jukwaa letu tukufu.

Siku za hivi karibuni wameibuka wadau ambao wanamlengo wa kushusha hadhi ya jukwaa kwa Thread zao zisizo na tija. Mfano mtu anaandika Helloooo then ukifungu hukuti kitu, au mwingine anaweka heading ya TCU NEWS, BREAKING NEWS, TCU WATOA MAJINA. NA HEADINGS NYINGINEZO ZENYE KUAMSHA HISIA. LAKINI UKIFUNGUA HUKUTI CHOCHOTE CHA MSINGI.

Pia kuna wenzetu wenye tabia ya kuweka Thread ambazo tayari zipo, pia nadhani si uungwana.

Ndugu zangu katika kulinusuru jukwaa hili ni vema utakapo kutana na thread za namna hii kuireport kwa mods ili iondolewe na si kuendelea kuicomment.
Pia thread hizi zinatia hasira nakupelekea BAN kwa baadhi ya wajumbe.

NAPENDA KUOMBA RADHI KWA MARA YA PILI KWA KUIWEKA POST HII MAHALA HAPA.
AHSANTENI.
 
Hii Forum inabidi ibadilishwe jina iitwe Secondary students forum, nasikitika pale malalamiko ya HESLB yatakavo kuwa mengi hapa baada ya majina kutoka.
 
Nadhani utakua ni uungwana tukiweka thread moja ambayo itakua Sticky na itumike kwa post zote za TCU na HESLB.
 
acheni umbea kwani wakiweka inawahusu nini

Tatizo lako unakurupuka. Mimi nimetoa pendekezo kama ni mwenyeji hapa utakuashaidi wa thread uchwara mfano mtu anaandika tcu news then ndhani hakuna kitu. Ila kwakua ni mgeni pole sana.
 
kweli kaka maana jana nimetoka kula BAN kutokana na watu fulanifulani kupost vitu ambavyo viko ndani ya jukwaa la elimu..!! Itakuwa vyema sana tukiwa tunapeana vitu current na pia ukimuoona mtu keshatupia thread kuhusiana na kitu sio lazima na wewe ui-copy ili kujitafutia umaarufu.!!

NOTE: kumbuka kuwa tuko hapa kuelimishana na sio kujaza vitu vya kijinga ndani ya hili jukwaa usema kweli New comer's MNABOAAAAAAAAAAÄAAA !!
 
Jamani tushirikiane kuokoa hadhi ya jukwaa letu. Sio watu kama MAJUTO tayari kashasema tuache umbea. Dah tutafika kweli?
 
Mfano Thread yenye heading hii.
TCU, kiroho
safi!
Ya bwana Pokofame
 
Mtoa hoja ameongea vizuri:ila wadau wengi wana ubinafsi kias kwamba wanafanya forum iwe kama ina stratification,sio mzuka fanyeni mambo kisomi-
 
ebana ulisemalo ni kweli tupu, coz kuna raia zinapenda tu kujaza kurasa bila kua na point za msingi, mtu anaandika TCU sasa hewani, alafu ukicheki unakuta empty , kwa kweli wana jf tubadilike.
 
Ni kweli watu wanarudiarudia threds lakini nina huakika kabisa kila thred inautofauti toka kwa nyingine hivyo ziko ambazo zinaeleweka xana, zinazoeleweka kias na zisizo eleweka kabisaaa, xaxa sioni vbaya tukiwa na thread hizi zote xo wewe ambaye unaona azikufai achana nazo nenda kwenye threads zikuafaazo, NAWASILISHA
 
acha unafiki wewe, kwan kuna ubaya gani ukipewa taarifa moja na watu zadi ya mmoja
 
Aisee jamaa yuko sawa mf m2 anaweka uzi ambao unashindwa hata kuchangia kwa kukosa maana haswa ya uzi,2badilike jaman tukomboe jukwaa hili.
 
Swala la kuzungumzia newkama naona n kwamba m2 anakua ana2oshea na ukzingatia hakuna alye zalwa anajua so akuna alye zaliwa ndan ya jf kwa hyo hzo n sifa 2 humu hakuna anayelipwa(haliitajk jbu)
 
Swala la kuzungumzia newkama naona n kwamba m2 anakua ana2oshea na ukzingatia hakuna alye zalwa anajua so akuna alye zaliwa ndan ya jf kwa hyo hzo n sifa 2 humu hakuna anayelipwa(haliitajk jbu)

unaogopa jibu eah kwa vile unajuwa umeandika mzoga wa fisi
 
Back
Top Bottom