Taarifa Kwa Wadau Wa Hakimiliki Na Cosota

Msanii

Platinum Member
Jul 4, 2007
22,548
29,620
COSOTA inapenda kuwatangazia Wadau, Wanachama wake na wale wote waliosajili kazi za Muziki na Filamu COSOTA, kwamba tarehe 18/07/2008, kutakuwa na hafla ya kutoa rasmi gawio la tano la Mirabaha. Shughuli hiyo itafanyika katika ukumbi wa Dar es salaam International Conference Centre ulioko PPF Tower.
Mgeni rasmi katika hafla hiyo atakuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda, Biashara na Masoko Dkt. Stergomena L. Tax.
Kwa taatifa hii wanachama na wadau wote wa Milki Ubunifu mnaalikwa kuhudhuria hafla hii itakayoanza saa 3:00 asubuhi.
Karibuni sana.
Imetolewa na:-
Afisa Mtendaji Mkuu,
Chama cha Hakimiliki Tanzania,
S.L.P 6388,
Dar es salaam.
Simu: +255-22-2125981
Nukushi: +255-22-2125982
Barua pepe: cosota@intafrica.com
Tovuti: www.cosota-tz.org
 
Mmefikia Wapi Na Swala La Ze Commedy!!haki Lazima Itendeke Kwa Wasanii Wachanga!
 
Aaaaah mnawanyenyekea wenye mshiko malizeni issue za Ze comedy watu tuanze kuburudika.
 
Mimi nataka kusajili post zangu hapa...

Hiyo Mirabaha wahusika wakuu wana taarifa nayo na wanaelewa ni kitu gani na wanafahamu ni kwa nini wanapa? Achana kwanza na maana halisi ya hilo neno Mrabaha... Ama ndio katika Kuvutia Umati ili kuficha madhambi maana mpaka leo sijui kama Cosota ipo kwa ajili ya nani... Wasanii ama?
 
Back
Top Bottom