TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI - Maandamano ya Amani na Mkutano wa Wazi

Status
Not open for further replies.
Kwasababu mmeshajua wananchi wamechoshwa na wanaweza kuandamana kukipinga chama tawala,sasa na nyie mnakuja na maandamano ambayo nadhani ni sawa na ngozi ya kondoo ndani ni fisi.
 
Hivi kumbe wewe ni CCM? Nilikuwa sijuiiiii,,,, unauliza maandamano ya nini?

Kuwa CCM si kosa na hakumfanyi mtu asithaminiwe utu wake. Jibu hoja na wala si kusema wewe CCM au CHADEMA. Swali lililoulizwa ni la msingi kama wanafalsafa walivyosema kuwa swali la kijinga ni lile tu ambalo halijaulizwa. Tuache huu upuuzi wa kutokijubu hoja na kuanza kushambuliana kwa tofauti za itikadi
 
XFoundatiionFinalLogo.jpg

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Isambazwe Mara Moja

Alhamis, Julai 21, 2011

KUITISHWA KWA MAANDAMANO YA AMANI NA MKUTANO WA WAZI
Mahali: Uwanja wa Mwembeyanga, Temeke, Dar es Salaam
Tarehe: 1 Agosti 2011

Nikiwa kama Mtanzania, mpenda amani, raia wa KUZALIWA, Mzalendo Halisi mwenye kuipenda nchi yake, na kiongozi wa asasi-huru ya X Foundation yenye makazi yake Jijini Dar es Salaam, napenda kutoa taarifa kwamba, X Foundation inawaalika Watanzania wote waishio Dar es Salaam na kwingineko, kwamba, kutakuwa na Maandamano ya Amani na Mkutano wa Wazi, siku ya Jumatatu, Agosti Mosi, 2011, kuanzia Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Temeke hadi Uwanja wa Mwembeyanga, Temeke, Dar es Salaam. Watanzania mnaombwa kukusanyika KWA AMANI, kwenye eneo la wazi, nje ya Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Dar es Salaam, kuanzia saa 2 asubuhi. Maandamano yataanza rasmi kutoka Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Temeke, takriban saa 4 kamili hadi Uwanja wa Mwembeyanga, Temeke, na yanatarajiwa kupokelewa na Mhe. Beatrice Matumbo Shellukindo (MB, Kilindi, CCM), akishirikiana na viongozi wa vyama mbali mbali vya kisiasa na kijamii, ambao watakuwa wamealikwa kuhudhuria.

Dhumuni la Maandamano ya Amani na Mkutano wa Wazi, tukio ambalo litafanyika kwa amani, linachagizwa na Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, toleo la mwaka 1977, kama ifuatavyo:

  1. Msingi na Mustakabali: Serikali na Watu, Sheria ya 1984, Na. 15, ib. 6, kama ifuatavyo:
8.-(1) Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni Nchi inayofuata misingi ya demokrasia na haki ya kijamii, na kwa hiyo -
(a) wananchi ndio msingi wa mamlaka yote, na Serikali itapata madaraka na mamlaka yake yote kutoka kwa wananchi kwa mujibu wa Katiba hii;
(b) lengo kuu la serikali litakuwa ni ustawi wa wananchi;
(c) Serikali itawajibika kwa wananchi;
(d) wananchi watashiriki katika shughuli za Serikali yao kwa mujibu wa masharti ya Katiba hii.

  1. Uhuru wa Mawazo: Uhuru wa Maoni, Sheria ya 1984, Na. 15, ib. 6, kama ifuatavyo:
18.-(1) Bila ya kuathiri sheria za nchi, kila mtu yuko huru kuwa na maoni yoyote na kutoa nje mawazo yake, na kutafuta, kupokea na kutoa habari na dhana zozote kupitia chombo chochote bila ya kujali mipaka ya nchi, na pia ana uhuru wa mawasiliano yake kutoingiliwa kati.

  1. Uhuru wa Kushirikiana na Wengine: Sheria ya 1984, Na. 15, ib. 6, kama ifuatavyo:
20.-(1) Kila mtu anastahili kuwa huru, bila ya kuathiri sheria za nchi, kukutana na watu wengine kwa hiari yake na kwa amani, kuchanganyika na kushirikiana na watu wengine, kutoa mawazo hadharani, na hasa zaidi kuanzisha au kujiunga na vyama au mashirika yaliyoanzishwa kwa madhumuni ya kuhifadhi au kuendeleza imani au maslahi yake au maslahi mengineyo.

  1. Kila raia anayo haki na uhuru wa kushiriki kwa ukamilifu katika kufikia uamuzi juu ya mambo yanayomhusu yeye, maisha yake au yanayolihusu Taifa.

  1. Ulinzi wa Mali ya Umma: Sheria ya 1984, Na. 15, ib. 6, kama ifuatavyo:
27.-(1) Kila mtu ana wajibu wa kulinda mali asilia ya Jamhuri ya Muungano, mali ya Mamlaka ya Nchi na mali yote inayomilikiwa kwa pamoja na wananchi, na pia kuiheshimu mali ya mtu mwingine.

  1. Watu wote watatakiwa na sheria kutunza vizuri mali ya mamlaka ya nchi na ya pamoja, kupiga vita aina zote za uharibifu na ubadhilifu, na kuendesha uchumi wa taifa kwa makini kama watu ambao ndio waamuzi wa hali ya baadaye ya taifa lao.

Kutokana na mustakabali huu, mimi, nikiwa Raia wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ninao uhuru, haki na wajibu wa kuzingatia masharti haya yaliyotajwa hapa juu, kama ifuatavyo:

  1. Jamhuri ya Muuungano wa Tanzania imekuwa katika hali ya jumla ya kuyumba kwa uchumi wake, kuanzia mnamo mwaka 1994, wakati janga la nakisi ya nishati ya umeme lilipoikumba Jamhuri kwa mara ya kwanza, na kusababisha athari mbaya za kiuchumi
  2. Wizara ya Nishati na Madini ndiyo taasisi kuu ya Serikali ya Tanzania, ambayo, kwa mujibu wa Ibara ya 8-(1) ya Katiba, ibara ndogo ya (b), inatamkwa kwamba "wananchi ndio msingi wa mamlaka yote, na Serikali itapata madaraka na mamlaka yake yote kutoka kwa wananchi kwa mujibu wa Katiba hii", kwa hiyo, Wananchi ndio wenye mamlaka ya mwisho ya kuamua mustakabali wa utendaji wa viongozi wa Wizara hiyo, ambayo ni taasisi yao, wao wakiwa wenye kutoa "madaraka na mamlaka" kwa Serikali.
Kwa msingi huo mkuu, pamoja na misingi mingine iliyotajwa hapo juu, ninao uhuru, haki na wajibu wa kuitisha Maandamano ya Amani na Mkutano wa Wazi, kwa lengo la kuwashinikiza viongozi watendaji wakuu wa Wizara ya Nishati na Madini, yaani, Waziri, Naibu Waziri na Katibu Mkuu, kujiuzulu mara moja, ili kuwezesha utendaji wa Wizara hiyo kutendeka kwa ufanisi zaidi, kwani imeonekana dhahiri kwamba, katika kipindi cha uongozi wao wa Wizara hiyo, kipindi cha kwanza kikiwa cha 2005-2010, na cha pili kikiwa 2010-2015, hali ya ugavi wa nishati ya umeme imezidi kuwa mbaya kiasi cha sio tu kuathiri uchumi wa nchi, lakini pia, kuathiri vibaya zaidi maisha na mustakabali wa Watanzania kwa ujumla.

Kutokana na usimamiaji mbovu wa utendaji wa Wizara, pamoja na mipango mizuri iliyowekwa hapo awali, na pia, kutosikiliza maoni ya Wabunge, hususan maoni ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya inayohusika na sekta ya nishati, viongozi hawa walioteuliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dk. Jakaya Mrisho Kikwete, wamepuuza kabisa ushauri wa wataalam na wabunge, na katika utendaji wao mbovu, wameitia hasara kubwa Jamhuri hii, hivyo kusababisha upotevu wa mabilioni ya Shilingi, sio tu kutokana na Serikali kukosa kukusanya mapato kutokana na shughuli mbali mbali za uzalishaji kutoka kwenye viwanda, vingi ambavyo sasa vimefungwa, lakini pia, Serikali kukosa kukusanya mapato kutoka kwa wajasiriamali wadogo na wakati, hivyo kushindwa kujiendesha kwa ufanisi mzuri zaidi.

Kwa kuzingatia Masharti yaliyowekwa kwenye Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Ibara ya 27-(1) na (2), ninao uhuru, haki na wajibu wa kulinda mali ya umma, ikiwa ni pamoja na uchumi wa Jamhuri, lakini pia, kwa kuzingatia Ibara ya 18-(1) na 20-(1) na (2), ninao uhuru, haki na wajibu wa kutoa maoni yangu, na pia kushirikiana na watu wengine katika kutoa maoni hayo, ikiwa ni pamoja na kwenye hadhara, kupitia, kwa mfano, maandamano ya amani na mikusanyiko ya wazi, nikiwa na uhuru wa kutoingiliwa kati kwenye mawasiliano hayo ya amani.

Leo, Alhamis, Julai 21, 2011, ninatamka, kwa faida ya Watanzania wote, kwamba, ifikapo tarehe 1 Agosti 2011, sisi Watanzania, tutakusanyika kwa amani na tutaandamana kwa amani, kama ilivyotajwa hapo juu, na tutafanya mkutano wa wazi na wa amani, ili kuweka bayana maoni na hisia zetu kuhusu janga hili kuu lililoifika nchi yetu.

Tuhuma zinazowakabili watendaji hawa, wa kutaka kutoa hongo ya takriban Shilingi Bilioni Moja za Kitanzania, zitazungumziwa kwa undani na watu wenye taarifa kamili zaidi kwenye mkutano huo utakaofanyika Mwembeyanga, Temeke. Tunatoa maombi ya ushirikiano mwema kwa Watanzania wote katika maandalizi ya maandamano hayo na mkutano huo, ili kuleta ufanisi mzuri zaidi, kwani, penye umoja kuna nguvu, na penye wengi hapakosi mazuri.

Watu wote wenye nia nzuri na nchi yetu wanaombwa kuwasiliana nami kwa njia ya simu na/au barua pepe kama inavyoainishwa hapa chini. Mimi ni mhamasishaji, ninao uhuru, haki na wajibu huo, lakini mustakabali wa nchi yetu ni wetu wote, bila kujali itikadi zetu za kisiasa, au imani zetu za kidini, au rangi za ngozi zetu au makabila yetu, kwani, Tanzania ni moja, ni yetu wote, kila mtu anayeitwa Mtazania ana haki ya kuitetea na kuilinda nchi yake, akishirikiana na wenzake.

Asanteni kwa Ushirikiano wenu.

MwanaHaki

Simu selula: +255-786-019019 na +255-786-019019

Barua pepe: misterx@qi.co.tz

Haihitaji kuwa Mwana CCM kuona kuwa hayo maandamano hayana malengo yakini, soma vizuri katika utangulizi ambapo ndipo palitakiwa na lengo la maandamano. Tukishabikia kila ujinga wote tutaonekana wapuuzi hata mambo ya maana tunayoyata nayo yatawekwa katika kundi la upuuzi
 
Watanzania tumegubikwa na tamaduni ya kukurupuka na kuendeshwa na matukio siku zote, rais ambaye ni mtulivu ambaye anajua kupanga ni kuchagua huwa asilani hana papara rais amekuwa akitumia muda mwingi kusafiri huku na huko kutafuta ni jinsi gani ataweza kusaidia changamoto zinazowakabili watu wake. Tusiwe tunafikiri kwa kutumia ubongo na sio ufahamu kama vile tunavyo wakshifu wengine kuwa wanatumia matumbo kufikiri tukiwa tuna maanisha wanafikiri kwa njaa.

Rais Kikwete ameonekana akiwa bega kwa bega na watu wake katika mambo mbalimbali yanayokabili hali ya maisha ya kila siku, alikuwepo mkapa shutuma nyingi zilielekezwa juu yake ni mbabe, sio msikivu, dictator nakadhalika lakini leo hii wale watu hao kwa fikra zilezile wanadiriki kumkashifu muheshimiwa rais kwa tuhuma nzito na kubwa kabisa lakini tunajua agenda zao, wanatumiwa na uma wa wezi na wenye uchu wa madaraka.

Tanzania ni kisiwa cha Amani na Utulivu, kama unabisha leo hii njoo burundi uone nini kinachoendelea, Asilani tutalinda amani na utulivu wa nchi hii kwa nguvu hata kwa tone la mwisho la damu kama itatupasa kufanya hivyo.

Tumekuwa wepesi wa kulaumu na kuendeshwa na matukio haya swala la UMEME, je unafikiri kama raisi akitatua tatizo la umeme matatizo mengine yatakuwa yameeisha kwa mfano, vifo vya kinamama na watoto, elimu, maji, masoko ya biashara kwa wakulima wetu, ajira kwa watu wetu tunakurupuka kwa mihemuko ya kisiasa.

Fikra sahihi huja pale mwanadamu, anapotumia na kufikiri nnje ya boksi kwa kuangalia na mbinu nyingine mbadala ambazo zinaweza zikasaidia kutatua matatizo.

Raisi hafurahi kuona kuwa nchi inakuwa gizani, huitaji kuwa na degree ya chuo kikuu kudadaviua hili, la hasha hali ya uchumi wetu ndio inayosababisha yote haya yanayojitokeza kwa sasa. Rais amekuwa akitumia muda mwingi kutumia Muda wake kuwaza kuhusu mtoto yule anayekufa kwa kansa tandahimba, mzee yule anayekosa chakula leo masieda mbulu, na mama yule aliyeko mwandiga kigoma, ambae anajifungua akiwa anamsubiri nesi ambaye yuko kwenye foleni nmb kupokea mshahara wake.

Rais nasema ndio anayefaa kuongoza nchi hii kwasababu anatumia uelewa wa wananchi wake kuzungumzia hali ya maisha, kwa mfano ni wangapi mlioku humu kwenye jamii forum mnao amini kukua kwa uchumi ni hata kuwa na gari, kwani uongo mwaka themanini ni wangapi wetu waliokuwa wanamiliki magari, leo hii ooh magari sio kukuwa kwa uchumi rais hafikirii angetatua tatizo la foleni, Je rais kama angeshauriana na Magufuli na kusema parking mjini kwa siku ni shilling elfu ishirini si mngeandamana uchi nyie mnaokuwa wepesi kulalamika??? Faini iliposomwa laki tatu badala ya hamsini mlipanua midomo mpaka kimeo kikaonekana.

Rais kikwete ndio anayeweza kuongoza nchi hii, kuna baadhi ya wananchi wanao ona umeme ni anasa NDIO pia sisi tunaongozwa na huyo huyo mnao muona hafai kwetu tatizo sio umeme, HATUNA MAJI je kila mtu akianza kumuambia rais arudi safarini alipoenda KUHEMEA kwa ajili ya watu wake je mambo mengine yatatatulika??? Kwani ni asilimia ngapi ya wananchi wenye access ya umeme???? Hapa watu wanatumia kila nafasi kupayuka hasa kwa miitikio ya kisiasa, Angekuwa Dr Slaa rais angefunga vinu vya nuclear vizalishe umeme au angeangalia juu mwenyezi Mungu alete mvua????

Kikwete wewe ndio unaofaaa sisi asilimia 80% tuishio vijijini wewe ndio rais wetu, tunakutambua na kukuunga mkono na yote ufanyayo ni kwa ajili yetu, rais haendi ulaya kufanya shopping ya chakula ndani, wala nguo za kuvaa anenda kwa lengo moja tu la kutafuta jinsi ya kutimiza AHADI ya maisha bora kwa kila Mtanzania.

Rais kikwete ndio anayefaa kuongoza Tanzania, Mungu mpe afya na hekima ya kuendelea kutatua matatizo ya watu wako, ningekuwa na namba ningekutumia sms ya kukupongeza.

MAISHA BORA HAYAJI KWA KULALA, MAJUNGU NA MAANDAMANO AMKA FANYA KAZI TANZANIA ITAJENGWA NA MWANANCHI MMOJA MMOJA:
 
bado unatarajia ufumbuzi wa matatizo ya tanzania kutoka kwa ccm! hebu tudokeze, shelukindo alizuiwa kusema jambo lolote bungeni ili sasa aje kutuhutubia hapo m/yanga? kabla hujanishawishi weka jamvini b. shelukindo aliipataje barua iliyowalenga wakuu wa idara. mimi naona kama majukwaa ya sarakasi yanapangwa tayari kwa vikundi mbali mbali kuanza maonyesho ya sarakasi bin gimnastic.

Mkuu

Hili liko wazi. Barua imepatikana kutoka kwa wadau, wazalendo kama wewe, ambao wamechoshwa na hila na ghilba za watendaji wabovu serikalini. Kumbuka, Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge, inayohusika na masuala ya nishati, Januari Makamba, alitangaza rasmi kwamba kuna baadhi ya wabunge ambao anawatuhumu kupokea rushwa kutoka kwa wizara hiyo. Huenda naye anahusika na upatikanaji wa barua hiyo. Hicho ni kielelezo tosha cha kuthibitisha madai ya Januari Makamba. Kaka Jogi, hebu soma alama za nyakati. Hapa hakuna suala la siasa. Kama ingekuwa hivyo, wabunge wa CCM wangeikubali bajeti ya wizara hiyo. Mbona wameikataa? Kuna siasa gani hapo? Au hamtaki wawajibike kwa wananchi waliowachagua na kuwatuma?
 
Watanzania tumegubikwa na tamaduni ya kukurupuka na kuendeshwa na matukio siku zote, rais ambaye ni mtulivu ambaye anajua kupanga ni kuchagua huwa asilani hana papara rais amekuwa akitumia muda mwingi kusafiri huku na huko kutafuta ni jinsi gani ataweza kusaidia changamoto zinazowakabili watu wake. Tusiwe tunafikiri kwa kutumia ubongo na sio ufahamu kama vile tunavyo wakshifu wengine kuwa wanatumia matumbo kufikiri tukiwa tuna maanisha wanafikiri kwa njaa.

Rais Kikwete ameonekana akiwa bega kwa bega na watu wake katika mambo mbalimbali yanayokabili hali ya maisha ya kila siku, alikuwepo mkapa shutuma nyingi zilielekezwa juu yake ni mbabe, sio msikivu, dictator nakadhalika lakini leo hii wale watu hao kwa fikra zilezile wanadiriki kumkashifu muheshimiwa rais kwa tuhuma nzito na kubwa kabisa lakini tunajua agenda zao, wanatumiwa na uma wa wezi na wenye uchu wa madaraka.

Tanzania ni kisiwa cha Amani na Utulivu, kama unabisha leo hii njoo burundi uone nini kinachoendelea, Asilani tutalinda amani na utulivu wa nchi hii kwa nguvu hata kwa tone la mwisho la damu kama itatupasa kufanya hivyo.

Tumekuwa wepesi wa kulaumu na kuendeshwa na matukio haya swala la UMEME, je unafikiri kama raisi akitatua tatizo la umeme matatizo mengine yatakuwa yameeisha kwa mfano, vifo vya kinamama na watoto, elimu, maji, masoko ya biashara kwa wakulima wetu, ajira kwa watu wetu tunakurupuka kwa mihemuko ya kisiasa.

Fikra sahihi huja pale mwanadamu, anapotumia na kufikiri nnje ya boksi kwa kuangalia na mbinu nyingine mbadala ambazo zinaweza zikasaidia kutatua matatizo.

Raisi hafurahi kuona kuwa nchi inakuwa gizani, huitaji kuwa na degree ya chuo kikuu kudadaviua hili, la hasha hali ya uchumi wetu ndio inayosababisha yote haya yanayojitokeza kwa sasa. Rais amekuwa akitumia muda mwingi kutumia Muda wake kuwaza kuhusu mtoto yule anayekufa kwa kansa tandahimba, mzee yule anayekosa chakula leo masieda mbulu, na mama yule aliyeko mwandiga kigoma, ambae anajifungua akiwa anamsubiri nesi ambaye yuko kwenye foleni nmb kupokea mshahara wake.

Rais nasema ndio anayefaa kuongoza nchi hii kwasababu anatumia uelewa wa wananchi wake kuzungumzia hali ya maisha, kwa mfano ni wangapi mlioku humu kwenye jamii forum mnao amini kukua kwa uchumi ni hata kuwa na gari, kwani uongo mwaka themanini ni wangapi wetu waliokuwa wanamiliki magari, leo hii ooh magari sio kukuwa kwa uchumi rais hafikirii angetatua tatizo la foleni, Je rais kama angeshauriana na Magufuli na kusema parking mjini kwa siku ni shilling elfu ishirini si mngeandamana uchi nyie mnaokuwa wepesi kulalamika??? Faini iliposomwa laki tatu badala ya hamsini mlipanua midomo mpaka kimeo kikaonekana.

Rais kikwete ndio anayeweza kuongoza nchi hii, kuna baadhi ya wananchi wanao ona umeme ni anasa NDIO pia sisi tunaongozwa na huyo huyo mnao muona hafai kwetu tatizo sio umeme, HATUNA MAJI je kila mtu akianza kumuambia rais arudi safarini alipoenda KUHEMEA kwa ajili ya watu wake je mambo mengine yatatatulika??? Kwani ni asilimia ngapi ya wananchi wenye access ya umeme???? Hapa watu wanatumia kila nafasi kupayuka hasa kwa miitikio ya kisiasa, Angekuwa Dr Slaa rais angefunga vinu vya nuclear vizalishe umeme au angeangalia juu mwenyezi Mungu alete mvua????

Kikwete wewe ndio unaofaaa sisi asilimia 80% tuishio vijijini wewe ndio rais wetu, tunakutambua na kukuunga mkono na yote ufanyayo ni kwa ajili yetu, rais haendi ulaya kufanya shopping ya chakula ndani, wala nguo za kuvaa anenda kwa lengo moja tu la kutafuta jinsi ya kutimiza AHADI ya maisha bora kwa kila Mtanzania.

Rais kikwete ndio anayefaa kuongoza Tanzania, Mungu mpe afya na hekima ya kuendelea kutatua matatizo ya watu wako, ningekuwa na namba ningekutumia sms ya kukupongeza.

MAISHA BORA HAYAJI KWA KULALA, MAJUNGU NA MAANDAMANO AMKA FANYA KAZI TANZANIA ITAJENGWA NA MWANANCHI MMOJA MMOJA:

Kila siku mnakaa na kufirikira MAJI, MAJI, MAJI!

Haya, ngoja nikupe baadhi ya rasilmali za nishati hapa nchini.

  1. Ardhi Joto (Hot Springs/Geysers) - chanzo ambacho hakina ukomo, wala hakihitaji manunuzi, hakina kina cha urefu wala ufupi, mapana wala membamba, kiko tuuuu! Uganda wanatumia nishati hii
  2. Biogas (Gesi Baolojia) - hii inazalishwa kwa wingi mno, nyumbani (mijini na shambani, kwenye kinyesi cha binadam na wanyama, na pia mabaki ya chakula), kwenye viwanda vinavyotumia bidhaa za mazao yatokanayo na kilimo, kama vile sukari na pia hupatikana kwenye mabaki ya miti, kwenye viwanda vya mbao, na kadhalika
  3. Upepo - hapa hakuna mjadala, maana upepo uko bwerere, kuanzia Same hadi Makambako, sembuse Singida, Kilimanjaro International Airport, na kadhakika (Chuo Kikuu cha Dar es Salaam walifanya utafiti tangu 1967, Ramani ya Upepo ya Tanzania imesharejewa zaidi ya mara tano, inapatikana, sehemu zote zenye upepo wa kutosha zinajulikana)
  4. Gesi Asilia - Kule Mnazi Bay, Mtwara, kuna uwezekano wa kuingiza kwenye Mtandao wa Taifa wa Umeme, sio chini ya Mega Watt 300, iwapo serikali itaridhia mpango wa kujenga miundombinu ya kusafirisha umeme kutoka Mnazi Bay hadi Dar es Salam au Makambako, ambapo pengine ni karibu zaidi
Sasa, baada ya kukupatia mifano michache iliyopo hapo juu, bado utaongelea suala la maji? Kama ni maji, mbona mawimbi ya bahari nayo yanaweze kutumika kuzalisha umeme, na teknolojia hii inatumika India na kwingineko zaidi ya miaka 20 sasa? Uliona wapi maji yanaisha baharini?

Kaka, hebu kaa chini na wanawake, wajasiriamali, waliokopa mikopo toka Access Bank, Benki ya Wanawake Tanzania, SACCOS zao na kwingineko, halafu jaribu kuongea nao, kuhusu unayoyasema, kama watakuelewa. Unazungumzia suala la afya? Huko hospitalini madaktari watafanya namna gani upasuaji bila kuwapo na umeme chumba cha upasuaji? Dawa zinazohitaji kuhifadhiwa kwenye majokofu zitahifadhiwa kwa namna gani bila ya umeme, hata ule wa jua?

I REST MY CASE!

./Mwana wa Haki
 
imeshapata kibali toka inteligensia ya nchi? maana hii ndiyo section ambayo jamaa wana peform excellent. Ili kama sivyo basi tujiandae kuja na chupa za maji ya uhai.

Watoe au wasitoe kibali, tutaandamana kwa amani. Niko tayari kupigwa mabomu ya machozi na kuwekwa ndani, kwa ajili ya KUITETEA na KUILINDA nchi yangu dhidi ya MAFISADI!

Sijali itikadi yoyote ile ya kisiasa, KWA HILI!
 
Kama maandamano basi yaandaliwe na taasisi za kiraia; hapo tutakuja wote. Lakini haya ya Wanasiasa vigeugeu kutegemea na maslahi ya wakati huo mara zote tutakuwa hatua moja mbele na kurudi nyuma hatua 2.

Wapi Taasisi za Kiraia? Sio vi-NGO vya mifuko kuhgawana posho, tunataka taasisi za kiraia waamshe bango utaona moto wake utakapofikia.
 
Soma tena kataja sema kajificha kwenye chama usika ila nadhani ni ccm maana ofisi ya mkuu wa wilaya mmmmmmm

Tunaowataka waondoke madarakani ni MAKADA wa CCM. Sasa hapo kama kuna kujificha, sijui inakuwaje. Hebu someni vizuri na kufanya uchambuzi, KABLA YA KUANDIKA UROJO!
 
Mh Beatrice Shellukindo ni YUDA ESKARIOT - period!

Na alivyo mufilisi wa moral na akili atajitokeza hadharani na kujidai yeye ni mtetezi wa wanyonge! wale wale walio -mfix mume wake ndio wanaomlisha! How low of her!
 
Kaka, rudia kusema. Kila kitu kimewekwa bayana, au unataka "nukuu"?

Kwa msingi huo mkuu, pamoja na misingi mingine iliyotajwa hapo juu, ninao uhuru, haki na wajibu wa kuitisha Maandamano ya Amani na Mkutano wa Wazi, kwa lengo la kuwashinikiza viongozi watendaji wakuu wa Wizara ya Nishati na Madini, yaani, Waziri, Naibu Waziri na Katibu Mkuu, kujiuzulu mara moja, ili kuwezesha utendaji wa Wizara hiyo kutendeka kwa ufanisi zaidi, kwani imeonekana dhahiri kwamba, katika kipindi cha uongozi wao wa Wizara hiyo, kipindi cha kwanza kikiwa cha 2005-2010, na cha pili kikiwa 2010-2015, hali ya ugavi wa nishati ya umeme imezidi kuwa mbaya kiasi cha sio tu kuathiri uchumi wa nchi, lakini pia, kuathiri vibaya zaidi maisha na mustakabali wa Watanzania kwa ujumla.

Kutokana na usimamiaji mbovu wa utendaji wa Wizara, pamoja na mipango mizuri iliyowekwa hapo awali, na pia, kutosikiliza maoni ya Wabunge, hususan maoni ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya inayohusika na sekta ya nishati, viongozi hawa walioteuliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dk. Jakaya Mrisho Kikwete, wamepuuza kabisa ushauri wa wataalam na wabunge, na katika utendaji wao mbovu, wameitia hasara kubwa Jamhuri hii, hivyo kusababisha upotevu wa mabilioni ya Shilingi, sio tu kutokana na Serikali kukosa kukusanya mapato kutokana na shughuli mbali mbali za uzalishaji kutoka kwenye viwanda, vingi ambavyo sasa vimefungwa, lakini pia, Serikali kukosa kukusanya mapato kutoka kwa wajasiriamali wadogo na wakati, hivyo kushindwa kujiendesha kwa ufanisi mzuri zaidi.

Tuendelee! Asante kwa hoja zenu, maana kwenye hoja ndipo mustakabali utakapopatikana. Hili halihitaji chama, kwani, hata wana-CCM nao wanaathirika na janga hili la umeme.
 
Haya maandamano yanaweza kua na nia njema tu,
ila sasa hukuona wageni wengine wa kuwaita kwenye haya maandamano zaidi ya huyu.
Huyo mgeni wako uliomuita ukweli haaminiki yuko upande gani.
Zaidi alishatutusi sisi ma-great thinkers (bofya linki hii hapa chini)
https://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/149843-mbunge-wa-kilindi-aipaka-jamiiforums.html
Shark,
Kumbe na wewe umeliona hilo, eeh? Hawa watu wa CCM ni watu wa ajabu sana. Sakata la kutembezwa bahasha kwenye kamati ya madini na nishati ilifichuliwa kwa mara ya kwanza kabisa na John Mnyika, wa Chadema, ambaye alikataa kuchukua hiyo bahasha na kuuliza hizi ni bahasha za nini. Sasa ghafla wana CCM, pamoja na huyo mama anayemtetea Lowasa kuwa si fisadi, wanachukua credit na kujitafutia umaarufu wa fasta fasta kama mkombozi wa Watanzania. Hatudanganyiki!
 
Haya maandamano yanaweza kua na nia njema tu,
ila sasa hukuona wageni wengine wa kuwaita kwenye haya maandamano zaidi ya huyu.
Huyo mgeni wako uliomuita ukweli haaminiki yuko upande gani.
Zaidi alishatutusi sisi ma-great thinkers (bofya linki hii hapa chini)
https://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/149843-mbunge-wa-kilindi-aipaka-jamiiforums.html

Asante kwa hoja yako, lakini soma vizuri hapa nilipoandika (in bold):
Maandamano yataanza rasmi kutoka Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Temeke, takriban saa 4 kamili hadi Uwanja wa Mwembeyanga, Temeke, na yanatarajiwa kupokelewa na Mhe. Beatrice Matumbo Shellukindo (MB, Kilindi, CCM), akishirikiana na viongozi wa vyama mbali mbali vya kisiasa na kijamii, ambao watakuwa wamealikwa kuhudhuria.

Viongozi wa vyama mbali mbali vya kisiasa na kijamii ni wengi, sijasema Mama Shellukindo atakuwa peke yake. Eboooo! Umetumwa?
 
Kama maandamano basi yaandaliwe na taasisi za kiraia; hapo tutakuja wote. Lakini haya ya Wanasiasa vigeugeu kutegemea na maslahi ya wakati huo mara zote tutakuwa hatua moja mbele na kurudi nyuma hatua 2.

Wapi Taasisi za Kiraia? Sio vi-NGO vya mifuko kuhgawana posho, tunataka taasisi za kiraia waamshe bango utaona moto wake utakapofikia.

Samahani, ashakum si matusi, lakini "The X Foundation" ni taasisi ya aina gani? Nina mashaka na ELIMU YAKO! Maana umeshindwa kubaini kwamba muandaaji si chama cha kisiasa. Na NANI aliyesema kwamba hata RAIA hawezi kuandaa maandamano? Kwani Katiba inasemaje, au wewe hujaisoma vizuri katiba? Katiba haijasema kwamba hali kama hii lazima iandaliwe na NGO. Mbona hizo taasisi za Kiraia unazozitaka wewe hazijatoa tamko lolote unalolitaka wewe, MPAKA SASA?

Sema kingine, lakini una lako jambo. Nakutazama kwa jicho la tatu! Nenda kawaite hao wenye hizo taasisi za kiraia, unazozitaka wewe, maana hata wewe pia ni taasisi ya kiraia, ila bado hujajua. LOL
 
Asante kwa hoja yako, lakini soma vizuri hapa nilipoandika (in bold):

Viongozi wa vyama mbali mbali vya kisiasa na kijamii ni wengi, sijasema Mama Shellukindo atakuwa peke yake. Eboooo! Umetumwa?
Naona wewe ndiye uliyetumwa. Hao viongozi wa vyama mbalimbali vya kisiasa wanaweza kuwa Cheyo na Mrema na Dovuta. Sterring bado atakuwa ni Shelkukindo. Hatudangayiki!
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom