shekinahpres
Member
- Oct 9, 2014
- 22
- 5
Katiba hii inakithi viwango kabisa. Sema watu huwa hawaridhiki tu. Lakini katika hali halisi katiba tuipigieni kura ya ndiyo
Ningekuwa nilitumia kura yangu kumchagua huyu jamaa ningehama nchi, sijawahi kuona raisi dhaifu kama huyu. Nadhani anatetea ulaji wa kuendelea kuchagua hawara zake kuwa mawaziri bila kuzuiwa na bunge. Pia anatetea kutoshtakiwa kwa wizi alioufanya kupitia kwa mwanae Riziwani. Katiba ya wananchi ilitaka raisi ashtakiwe na pia akifanya uteuzi lazima bunge lithibitishe na kuidhinisha kwanza. Anatetea kutokwenda jela au The Hague, ngoja ije huku tuwakomeshe.
Kwanini unahisi Ulukolokwitanga hana akili?toa sababuHuna akili
Hah hah ha ha ha,mjue Kikwete anasoma comments zenu naamini anacheka kama mimi hapaKikwete ni kiherehere
Hiyo rasimu kwa upande wa pili ni ilani ya uchaguzi next yrKm raisi anawza kuongea ivo wakat kina mamilion ya watanzania wenye akili timam na wengine ni wasomi wanaojua kipi knafaa na kipi hakifai, basi didhan km ni mtu aliyestahili kua katka hyo nafasi. Katba kutaja makundi yote ya wananchi sio hoja ya msingi wala sio sababu ya kuwafanya watanzania wanaojielewa wardhke. Mbona marekani ni muungano wa nchi zaid ya 50 na wana serikali moja tu...na pia ni taifa lenye katba fubi zaid daunian, wana katba ina sura 6 tu..
Lakn mbna hatuskii wasanii wala aknamama au wakilima wakilalamika?? Inamaana hyo katiba imetaja makund yote ya wananch wa marekani?? Suala la msingi ambalo watanzania wanaojielewa wanalilalamikia ni suala la muundo wa serikali na jinsi wabunge wanavojipa uhuru zaidi. Hayo ndio mambo ya msingi ambayo yanajenga. Sasa mkikaa mnajadili mambo ya wanawake bungeni kua 50 kwa 50 na wanaume, wakat hata wanawke wenyew hawaamin km wanaweza kumudu hzo nafasi, km sio ushabik hao waliopendekeza katba wanafuta ni nn hasa??!! Watanzania tuamke.
Katiba tuliyonayo sasa imejaa haki za binadamu lakini tunashuhudia watu hawazipati. Kutamka makundi katika katiba hakuifanyi I we bora ikiwa tu hakuna uhakikisho wa kupata haki makundi husika. Kuna vifungu tayari katika katiba vinazuia kudai haki Hizo za makundi! Je uzuri wake ni up?
Jumatatu itatoka taarifa nyingine ya kukanusha kuwa Kurugenzi ya mawasiliano Ikulu si SHIIDA.CHEZEA SALVER WEWEKirugenzi ya Mawasiliano Ikulu ni shiida!
Tusijadili katiba. Tujadili kwanza huu uandishi. Ni kweli ni wa ikulu?THEUNITED REPUBLIC OF TANZANIA
DIRECTORATEOF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS
TAARIFAKWA VYOMBO VYA HABARI
KamaKatiba Inayopendekezwa ni mbaya, hiyo nzuri ikoje?
auliza Rais Kikwete
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikweteamewashangaa watu wanaodai kuwa Katiba Inayopendekezwa ni mbaya,akiuliza kuwa kama Katiba hiyo ni mbaya basi hiyo nzuri ikoje?
Aidha,Rais Kikwete amesema kuwa Katiba inayojali makundi yote ndani yajamii, kama ilivyo Katiba Inayopendekezwa, kamwe haiwezi kuwa Katibambaya.
Rais Kikwete ameyasema hayo nyakati tofauti leo, Ijumaa, Oktoba 10, 2014,wakati alipozungumza na wananchi katika maeneo mbali mbali ya Mkoa waMwanza, ambako anafanya ziara ya siku tatu ya kikazi kukagua nakuzindua miradi ya maendeleo.
Akizungumza na mamia kwa mamia ya wananchi mjini Kisesa ambako ameweka jiwe lamsingi la ujenzi kwa kiwango cha lami na Barabara ya Usagara-Kisesa,Rais Kikwete amewataka wananchi kuwapuuza watu wachache wanaodai kuwaKatiba Inayopendekezwa ni mbaya na badala yake wajiandae kuipigiakura ya kuikubali wakati ukiwadia.
Sijui katiba nyingine duniani ambayo inajadili makundi yote ndani ya jamiikama hii Katiba Inayopendekezwa. Hakuna aliyeachwa wavuvi wamo,wajane wamo, wafanyabiashara ndogo ndogo wamo, akinamama lishe wamo,wakulima wamo, wafugaji wamo .kila mtu yumo. Akinamama ndio usisemekabisa wao wamepata hata asimilia 50 kwa 50 ndani ya Bunge.
Ameongeza Rais Kikwete: Hivi katiba mbaya inakuwa kama inayopendekezwa nakama hii inayopendekezwa ni mbaya sasa hivi nzuri ikoje?
Rais Kikwete amewambia wananchi: Watakuja watu kuwashawishi kuwa KatibaInayopendekezwa ni mbaya, wasikilizeni lakini tumieni akili yetu,kama ile hadithi ya mbayuwayu. Jiandaeni tu kupiga kura na kuungamkono Katiba Inayopendekezwa kwa sababu hii ni Katiba nzuri sana.
Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu,
DAR ES SALAAM.
10 Oktoba, 2014
TThese people,wanaweza kukanusha hata kama waliandika waoNasubiri ikulu ikanushe hii taarifa na kama ni wao wameandika basi hiki kitengo kinadhalilisha ikulu ya Tanzania. Huu ni upuuzi kutoka ikulu ya kikwete.
Why waandike namna hii?